Blood of Jesus
JF-Expert Member
- Sep 19, 2016
- 4,486
- 8,098
Tunapambana kutafuta hela hekeheka za kufa mtu, halafu mtu huyu akishajenga nyumba ya kuishi anaona amemaliza ndoto yake aliyokuwa anaipigania anapunguza mapambano.
Hapo yeye anatafuta hela ya kula tu basi. Niwakumbushe kujenga si maendeleo bali ni hitaji la lazima tupambane zaidi tupate maendeleo.
1 Timotheo 6 (Biblia Takatifu)
¯¯¯¯¯¯¯¯¯¯
⁶ Walakini utauwa pamoja na kuridhika ni faida kubwa.
⁷ Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu;
⁸ ila tukiwa na chakula na nguo tutaridhika na vitu hivyo.
⁹ Lakini hao watakao kuwa na mali huanguka katika majaribu na tanzi, na tamaa nyingi zisizo na maana, zenye kudhuru, ziwatosazo wanadamu katika upotevu na uharibifu.
¹⁰ Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi.