Mi niliwahi kuambiwa nisipambane kupita kiasi, maisha hayana shukrani kila siku linazuka jipya, unaweza kuchanganyikiwa, nami nikayaacha maisha kama yalivyo.
Niliambiwa utapambana sana lakini hutoenda na kitu kaburini, nikaambiwa wengi unao waona hata matajiri hufariki wakiyaacha mabilioni benki, tena mwingine alisema wapo ambao hata wakiugua wanaona shida kutumia peza zao wenyewe kujitibu wakihofia zitakwisha na wakipona wataanza upya, au kufilisika kabisa.
Niliambiwa fanya kazi tekeleza unachokihitaji, Ridhika na ulichonacho, usitafute ziada utakufa siku si zako.
Niliambiwa utajiri ni bahati, siyo kitu unaweza kukipambania, dunia hii hujaiumba wewe, walikuwepo wakafariki wakaiacha, uliikuta na utaiacha, duh.
Hapa mnaanza kunichanganya tena, kwamba tuendeleze mapambano, ya nini kama nimetosheka na sehemu nilipo?