Mpo salama!
Watanzania wanaamini Wachagga ni watu wote wanaotokea Kilimanjaro na Arusha bila kujali mikoa hiyo inamakabila mengine kama Wapare, Wameru, Wambulu, Wamasai, Wachagga na Wasambaa kidogo.
Sio ajabu hata wakisikia John Mnyika, au Halina Mdee licha ya kuwa ni Wapare hao ila Watanzania utawakuta wakitoa maoni Yao wakisema hao ni Wachagga.
Ukiende kwenye page ya Mange Kimambi ambaye yupo upande wa Mbowe, ukifuatilia maoni ya watu kwenye page hiyo utaona wakimhusisha Mange Kimambi na Uchagga ilhali Mange sio mchaga Bali Mpare.
Utasikia wakimwambia Mange Kimambi, ninyi Wachagga wabaguzi Sana kwa vile ni mchaga mwenzako ndio maana unamuunga Mkono.
Hoja ya ukabila ndani ya CHADEMA inapaswa ifutwe kiivitendo hicho ndicho Watanzania wanataka.
Sio ajabu watu wa kanda ya ziwa, kusini, na kanda ya Kati wanamuunga Mkono Tundu Lisu.
Inajulikana kuna uhusiano wa karibu baina ya Wachagga na watu wa kanda ya mashariki ambayo ni Pwani yote.
Ngoja tuone