Watanzania wengi wanaamini CHADEMA ni chama cha Wachagga ndio maana wanamuunga Lisu kuondoa mzizi wa fitna

Kuna watu wanawachukia Wachaga hata bila sababu.

Mchaga kufanikiwa utasikia ametoa kafara, ni mwizi na blah blah kibao.

Mchaga akienda kwao utasikia ameenda kutambikia mizimu.

Utakuta mtu mzima JF analeta mada kuwa wanawake wengi Wachaga ni wajane na anatoa ushauri kabisa kuoa Mchaga ni kulitafuta kaburi.

Itoshe kusema kuwa wale watu wenye mtazamo wa kuwa CHADEMA ni chama cha Wachaga ni watu walewale wenye chuki na Wachaga zisizo na sababu.
Hapana shida sio hiyo
Shida ni Kweli Mbowe anakomaa yeye na John Mrema miaka nenda rudi kwann wao tuu...
 
Hii Ngoma CHADEMA haichomoi nakuambia.
Kuchomoa kwao ni Mbowe akae pembeni Jambo ambalo haliwezekaniki.

Tupo hapa.

Yaani kwa kifupi 2025 ACT ndio habari ya Mjini.
Mtaji mdogo wa pesa waliobakiwa nap CHADEMA wautumie vizuri
Hawachomoi kwani walichomeka nini?

Haya maneno sio mageni,yameanza kuimbwa kitambo kabla hujaijua jf

Lisu ataanza kutangatanga kuanzia mwezi ujao.
Kashtukiwa mapema sana
 
huo wimbo umeanza enzi za jpm bado chadema ipo.
Kampeni za 2010 ulikua hujazaliwa?

Wakati Chacha Wangwe analalamika uchaga ndani ya chama ilikua kipindi cha JPM?

Issue ya uchaga ndani ya Chadema imeanza tangu zamani, na ni kweli Chadema kuna ukabila na ukanda.
 
Mpo salama!

Watanzania wanaamini Wachagga ni watu wote wanaotokea Kilimanjaro na Arusha bila kujali mikoa hiyo inamakabila mengine kama Wapare, Wameru, Wambulu, Wamasai, Wachagga na Wasambaa kidogo.

Sio ajabu hata wakisikia John Mnyika, au Halina Mdee licha ya kuwa ni Wapare hao ila Watanzania utawakuta wakitoa maoni Yao wakisema hao ni Wachagga.

Ukiende kwenye page ya Mange Kimambi ambaye yupo upande wa Mbowe, ukifuatilia maoni ya watu kwenye page hiyo utaona wakimhusisha Mange Kimambi na Uchagga ilhali Mange sio mchaga Bali Mpare.

Utasikia wakimwambia Mange Kimambi, ninyi Wachagga wabaguzi Sana kwa vile ni mchaga mwenzako ndio maana unamuunga Mkono.

Hoja ya ukabila ndani ya CHADEMA inapaswa ifutwe kiivitendo hicho ndicho Watanzania wanataka.

Sio ajabu watu wa kanda ya ziwa, kusini, na kanda ya Kati wanamuunga Mkono Tundu Lisu.

Inajulikana kuna uhusiano wa karibu baina ya Wachagga na watu wa kanda ya mashariki ambayo ni Pwani yote.

Ngoja tuone
Ukiondoa ukabila, mbowe kachokwa, mbowe akipita chadema itakuwa imewavunja moyo vijana wengi wapenda mabadiliko
 
..mimi nataka Mbowe asichaguliwe, lakini sio kwasababu za KIKABILA.

..Mbowe ameipeleka Chadema kila mahali hapa nchini na sio sahihi kumshambulia kuwa amejenga chama kwa ajili ya Wachaga.

..Tanzania kumekuwa na kampeni ya muda mrefu dhidi ya Wachaga.

..Kuna wanasiasa wa CCM ambao walipoona wanazidiwa maarifa na wanasiasa toka Kilimanjaro walitumia ukabila kupambana nao.

..Sasa hali hiyo ni ama ilifanikiwa huko zamani, au iliachwa bila kukomeshwa, matokeo yake imekuwa ni jambo la kawaida katika siasa za Tanzania.

..Katika zama hizi kumshambulia au kumtuhumu Mchaga au mtu wa Kilimanjaro imekuwa ni jambo linalovumilika katika jamii yetu. Hayo ni mazoea mabaya ambayo yanayobomoa umoja wetu wa kitaifa.

..Sio sahihi kuwafanya ndugu zetu toka mkoa wa Kilimanjaro wajisikie sio sehemu ya Watanzania wote.
 
Mpo salama!

Watanzania wanaamini Wachagga ni watu wote wanaotokea Kilimanjaro na Arusha bila kujali mikoa hiyo inamakabila mengine kama Wapare, Wameru, Wambulu, Wamasai, Wachagga na Wasambaa kidogo.

Sio ajabu hata wakisikia John Mnyika, au Halina Mdee licha ya kuwa ni Wapare hao ila Watanzania utawakuta wakitoa maoni Yao wakisema hao ni Wachagga.

Ukiende kwenye page ya Mange Kimambi ambaye yupo upande wa Mbowe, ukifuatilia maoni ya watu kwenye page hiyo utaona wakimhusisha Mange Kimambi na Uchagga ilhali Mange sio mchaga Bali Mpare.

Utasikia wakimwambia Mange Kimambi, ninyi Wachagga wabaguzi Sana kwa vile ni mchaga mwenzako ndio maana unamuunga Mkono.

Hoja ya ukabila ndani ya CHADEMA inapaswa ifutwe kiivitendo hicho ndicho Watanzania wanataka.

Sio ajabu watu wa kanda ya ziwa, kusini, na kanda ya Kati wanamuunga Mkono Tundu Lisu.

Inajulikana kuna uhusiano wa karibu baina ya Wachagga na watu wa kanda ya mashariki ambayo ni Pwani yote.

Ngoja tuone
Shida Moja ya wachaga ni ubinafsi uliopitiliza,kutojali utu na maslahi ya wenzao.............wakina mangi meli walitaka Wadai uhuru wa kilimanjaro peke yake,
Wakati wakina Sykesa na wazee wa Dr es salaam walimpokea kwa moyo mmoja kijana kutoka Butiama awe muwakilishi wa kudai uhuru Kwa maslahi ya nchi,
hii nchi imeongozwa na itaongozwa na watu kutoka ukanda wa Pwani kwa zaidi ya 90%,sababu ya kutokua na roho mbaya iliyopitiliza
 
..Mangi Meli aliishi enzi za kina Mkwawa, Mirambo, na wavamizi wa Kijerumani.

..Sio sahihi kumlinganisha na wanasiasa wa zama za kudai Uhuru wa Tanganyika.

..Na kuhusu harakati za kudai uhuru wa Tanganyika wako Wachaga wengi walishiriki kwa kuunga mkono chama chaTanu.

..Hata baada ya uhuru wako Wachaga wametumikia nchi kwa uzalendo na uadilifu wa hali ya juu ktk maeneo mbalimbali.
 
Mareale alienda UN kudai uhuru wa kina nani?
 
..Mwalimu Nyerere na Mangi Marealle kwa pamoja waliunga mkono uhuru wa Tanganyika walipokwenda UNO.

..Naamini kuna upotoshaji ulifanyika kwa malengo ya kumdhoofisha Thomas Marealle kwasababu alionekana ni tishio kwa watawala.

..upotoshaji huo ndio umezaa ubaguzi dhidi ya Wachaga, na jamii nzima ya watu wanaotokea Kilimanjaro, Arusha, na Manyara.

..Mimi nampinga Mbowe lakini sio kwasababu za KIKABILA. Naamini tatizo ni uwezo wake umepungua.

..hoja kuhusu Mangi Marealle na uhuru wa Tanganyika hii hapa chini.

..mimi nataka Mbowe asichaguliwe, lakini sio kwasababu za KIKABILA.

..Mbowe ameipeleka Chadema kila mahali hapa nchini na sio sahihi kumshambulia kuwa amejenga chama kwa ajili ya Wachaga.

..Tanzania kumekuwa na kampeni ya muda mrefu dhidi ya Wachaga.

..Kuna wanasiasa wa CCM ambao walipoona wanazidiwa maarifa na wanasiasa toka Kilimanjaro walitumia ukabila kupambana nao.

..Sasa hali hiyo ni ama ilifanikiwa huko zamani, au iliachwa bila kukomeshwa, matokeo yake imekuwa ni jambo la kawaida katika siasa za Tanzania.

..Katika zama hizi kumshambulia au kumtuhumu Mchaga au mtu wa Kilimanjaro imekuwa ni jambo linalovumilika katika jamii yetu. Hayo ni mazoea mabaya ambayo yanayobomoa umoja wetu wa kitaifa.

..Sio sahihi kuwafanya ndugu zetu toka mkoa wa Kilimanjaro wajisikie sio sehemu ya Watanzania wote.
Propaganda hizi ni za ccm lakini utashangaa wao wenyewe hawajafunga ofisi zao Uchagani wawaache Wachaga na chama chao Chadema.
 
Mareale alienda UN kudai uhuru wa kina nani?
Huelewi Historia, Tanganyika kabla ya wakoloni zilikuwa ni Kingdom, hata Kilwa ilikuwa ni dola yenye sarafu yake, tatizo ccm imewajaza ujinga Watanzania wengi hawajui lolote, soma sera ya majimbo ya Chadema utaelewa.
 
Back
Top Bottom