Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

English medium social skills wanazo ila kwa watu wa class yao

Watu wao wa karibu wa kucheza nao ku socialize ni watoto wa wabunge mawaziri,wafanyabiashara wakubwa nk hupeana happy birthdays nk

Huwezi waona wana socialize na maskini ndio maana huwaoni huko mitaani wakicheza rede kama watoto wa uswahilini na hata kuoa au kuolewa wanaenda na class yao sio ya uswahilini

English medium ni njia mojawapo ya kupandisha class ya mtoto.aondokane na uswahiliswahili wa mitaani
 
Km.wtt walishapata msingi skuli za EM ukiwapeleka Kayumba wanatusua tu kama kawaida.
Mie pia nna mpango huo. Nasubiri wajivute walau mpk la 7 Insha'Allah
Hii idea nnayo zamani tu
 
Ni kweli sometimes kuna haja ya kujitoa mhanga kuvunja ile vicious cycle of poverty ya kuzunguka na watu masikini kua na marafiki masikini kuoa watoto wa masikini kuzaa watoto masikini kua na wajukuu masikini, kwasababu matajiri una mahara pakuwakuta na ku-socialise nao isipo kua kuenda kwenye shule za private English medium
 
Mzazi akishakosa pesa za kulipa ada EM ataanza kujifariji kuwa kidumu na ufagio ni kuzuri sana na ndio maana mtu kama alikuwa masikini kiasi gani akishapata pesa za kutosha utamkuta anaanza ku-google kuhusu madhara ya kula ugali, dagaa kauzu na tembele
 
Kwani anasoma EM maisha yote? Si miaka 7 tu?!, wacha tupambane kujenga msingi imara wa nyumba ya kisasa.
Sekondari tutawarudisha huku kayumba.
Primary wacha tuumizane huku EM maana mtoto akiwa mdogo ndio muda muafaka wa kumjenga kimtazamo tofauti
 
Wakati flani nimiwa mwalimu nilienda kusimamia mitihani shule ya binafsi. Ulikuwa mtihani wa kidato cha pili. Watoto kama 78 hivi katika hiyo shule binafsi. Matokeo yao yalikuwa division one wote. Wkt huo nafundusha serikalini na kidato hichohicho watoto 260 kulikuwa na division one 8, two 15, three 30, four 45 waliobaki zero.

Mytake. Uandishi wa essay(maelezo) ya hoja wale watoto 78 walikuwa smart mno. Mtoto anamwaga lugha ya malkin kurasa 2 hadi 3.

Kule kwangu wale watoto wenye division one waliotokea EM wanamwaga lugha vema, sasa njoo hawa wa kuanzia division 3 huku kwetu, yaan mtoto kuuganisha sentence hawezi. Page moja haifiki hata katikati na wanaishia kukopi maswali na majibu ya uongo kujazia essays.

Anaempleka mwanae EM anampa mtaji mwanae..wengine endeleeni kukejeli.
Watoto wenu ndio wale mkiondoka duniani, hawana foundation. Walimu 50 wa serikalini utakuta anayefanya kwa moyo mmoja ni 5. Hawa ndio husaidia sana.

Private walimu 50 makanjanja utakuta 3 hadi 5 hawa ni ndg na jamaa wa Mkurugenzi wa shule.

Fuja pesa nunua magari na kunywa bia ili mwanao akasome kwa kumsubiri Mama samia acheke.

Walimu asilimia 98 wale senior wanamajumba yao, wanaishi vzr na watoto wao wanawapeleka EM kwa kawaida wakistaafu hawana ufahari. Mungu awabariki walimu wote wa EM na Government mimi mawaita maafisa elimu
 
Sasa najiuliza mateso yote hayo ya Nini wakati hata Kayumba wanaweza soma vizuri tu na Chuo wakafika kama.wanavyo fika wengine.
 
Wahindi wanaishi nyumba za kupanga za National Housing na wanasomesha watoto shule za bei mbaya

Mtu kuwa anapanga nyumba haina maana kuwa ni maskini
Usijifananishe na wahindi. Wenzako wengi wao nyumba za babu Zao zilitaifishwa wakati wa Nyerere. Alafu kingine wengi wao hapa ni Foreigners ulitegemea wajenge?

Kibongo bongo usipokuwa na nyumba ni kiashiria bado unajitafuta


Kweli Kabisa
 

Uzi ufungwe!
 
Hoja ya kitoto kabisa kwahiyo mtoto kila anachotamani unampa😁😁😁nyie ndo mnatengeneza watoto wasio na uwezo mzuri wa kufikiri na wenye kufake maisha maana hata wazazi walifake maisha.


Muandae mtoto aweze kujitambua mapema acheni porojo na hoja mufilisi kama hizi.
 
Very true. Ku-struggle kwenye maisha ni jambo la kawaida na si dhambi. Hata hizo shule tulizosoma zamani wazee walijinyima sana na ku-struggle sana. Sasa uache kumpeleka mtoto shule nzuri kisa ada inasumbua? Labda kama mtu huna kipato kwa sababu mbalimbali za kimaisha kama kupoteza kazi. Kwanza mbali na kujua kiingereza pia upeo wa watoto wa private na government schools ni tofauti kabisa
 
Fainali wakishamliza chuo hiyo class yao unayoongelea ya kufake hapo baada ya kumaliza chuo ndo huwa inaonekana vizuri wale wa BOLT na UBER wanaanza kupanda bodaboda na dalalada😁😁😁😁😀😀😀


Huku mtaani mambo ni tofauti kabisa wale waliokuwa wanajitengatenga baada ya kumaliza chuo huwa wqnakuwa kama kuku walionyeshewa😀😀😀maisha ni hatua hutakiwi kufake utadhindwa kuishi na watu.
 
Siku hizi kuna kama kaugonjwa fulani kwa wazazi wa kileo,utasikia mzazi akisema mi mwanangu awezi kuteseka kama mimi,kamwe sitampeleka kayumba!,,mara sitaki atembee umbali fulani,,ooh nitafanya kila namna asiende kayumba nk nk,, watoto wanalelewa kimayai sana na wazazi wa sampli hii,ndo hao wanaingia gharama kubwa wasizoweza kuzimudu.
 
Usijifananishe na wahindi. Wenzako wengi wao nyumba za babu Zao zilitaifishwa wakati wa Nyerere. Alafu kingine wengi wao hapa ni Foreigners ulitegemea wajenge?

Kibongo bongo usipokuwa na nyumba ni kiashiria bado unajitafuta



Kweli Kabisa
Mtibeli ukiwekeza hela sehemu sahihi hizo nyumba za national housing (NHC) mtu yoyote anakaa.

Ujenzi wa nyumba huwa ni garama sana ukitaka kuamini hii. Tafuta mtu anayejenga muulize ametumia shingapi😀😀😀wengi watajificha kwenye kivuli ooohh mimi sipigi hesabu mara oohhh ukipiga utashindwa kujenga.Ila kiukweli kabisa a standard house kiwanja kilichopimwa na barabara inayopitika mitaa imepangiliwa yaani kwa makadirio ya chini sio chini ya milioni 80 unaizika hapo. Sasa hii mishahara ya sereikali 700k mpaka 2million kuna wa kujenga hivi.Akijitahidi sana hapo atakopa na nyumba itaishia kwenye plaster.Wengi wanajenga kwenye viwanja vya 20×20 nyumba imebanana hata sehemu ya kupita kuzunguka nyumba hamna.

Wewe saivi ukiwekeza hela kwenye mashamba ya miti,mashamba ya matunda na viwanja vya low density vilivyopimwa.Ukijikita na kuwekeza kwenye bonds na hisa. Huna haja ya kujenga maisha yako yote utaishi kwenye appartment maana wewe umefanya uwekezaji sahihi unaozalisha pesa kila leo na kupanda thamani ni tofauti na ungezika hizo hela, hiyo hiyo millioni 80 kwa kujenga nyumba.Ujenzi sio uwekezaji ni upotevu wa nguvu na rasilimali.

Serikali ingeruhusu tu baadhi ya kampuni kubwa zenye mitaji ndo zijenge ili kuwe na standard ya nyumba za kuishi na kuondoa tatizo la makazi holela na viwanja ambavyo havijapimwa.Mtu akitaka nyumba ananunua au akope alipe kidogokidogo mpaka amalize mkopo.
 
Kwani anasoma EM maisha yote? Si miaka 7 tu?!, wacha tupambane kujenga msingi imara wa nyumba ya kisasa.
Sekondari tutawarudisha huku kayumba.
Primary wacha tuumizane huku EM maana mtoto akiwa mdogo ndio muda muafaka wa kumjenga kimtazamo tofauti
Mkuu hata sekondari usijaribu kuwapeleta hizi government school, mtoto mpeleke shule nzuri aelewe maisha ni furaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…