Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Ulikuwa unalipa shilingi ngapi na kwa kuwa "umeiokoa" hiyo pesa unaiwekeza kwenye nini? Inaweza ikawa sasa ni pesa ya kwendea saluni na mashindano ya simu kali.
 
Mkuu mpeleke chanja shule za maana acha janja janja mtani.

Tanzania hii hizo shule za maana ziko wapi?

Mimi najua mtoto shule yake ya Kwanza ni nyumbani.

Ingawaje, nakubaliana na wazo kuwa mtu ampeleke mtoto kwenye shule ya level yake ya kiuchumi
Ila hayo mambo ya elimu sijui Bora hayo Mimi siyaamini Sana.

Labda kama kingereza ndio Elimu
 
Mtoto wako wa English Medium anaenda kuishia UDSM kama wa Kayumba. Wakimaliza hapo wote wanakuwa products za UDSM. Nobody gives a fu.ck where he went in Nursery/Primary school.
Unaota unajua ushindani wa mtu kujiunga na UDSM? Lazima mtoto.awe amefaulu sana Form four na form six kwa mpigo

Wengi wa kayumba huwa si rahisi kuingia UDSM sababu ufaulu wao huwa kiwango cha chini sana form sababu ya msingi mbovu wa kiingereza wanaishia tu kusoma vyuo vikuu vingine vya kata sio UDSM
 
Kuna mtu kasema "Kila mtu aishi kulingana na uwezo wake." Huyo yuko sahihi hayo maelezo mengine ni kama kupangiana maisha.

Anayetaka kumpeleka mtoto kayumba sawa, anayempeleka English Medium sawa. Ni sawa na kula mchicha huku mwingine kuku na wote tunakula chakula kinaingia tumboni baadae chooni ila tofauti ipo.

Uzuri au utamu wa kitu uko kwa mlaji
 
kwanini msiwafundishe huko ulipo wewe, hizo shule za EM walimu wametoka Ulaya au ni watanzania wenzio?
 
Uwekezaji usio na Tija huo.
Mtu kipato cha kubangaiza, nyumba ya kupanga, Hana Kiwanja, kila mwaka atoe Milioni Moja unusu kwa EM ati Elimu BoraπŸ˜‚πŸ˜‚

Wabongo bhana
Wahindi wanaishi nyumba za kupanga za National Housing na wanasomesha watoto shule za bei mbaya

Mtu kuwa anapanga nyumba haina maana kuwa ni maskini
 
Umaskini ni kitu kibaya sana. Hivi unawezaj kumpangia mtu mzima mfumo wa maisha yake ktk kulea familia yake. Unapata wapi nguvu za kumuonea huruma wakati hajawahi kukuomba ada ya mtoto wake.

Hizi story sijui za English medium au kayumba ni maamuzi ya mtu binafsi wala mhusika hashirikishi Wana jamii forum wala ukoo wake iweje umuonee huruma. Kila mbuzi ale kwa urefu wa kamba yake.

Kuna mmoja hapo juu kasema eti madaktari na ma engineer kwani wametoka wapi akimaanisha wametoka kayumba. My friend, hao ingawa wote ni professionals lakini uwezo wa uelewa wao ni tofauti hata km ni kada moja. Waliotoka forodhani secondary watatambulika tu kwa uwezo wao na wa kayumba watajulikana tu

Hoja za namna hii huletwa na short minded people na wasio na uwezo wa kutosha kifefha. Wakati wewe unawaza kujenga nyumba ya room 2/3 tena kwa taaaabu na kwa muda mrefu mwenzio anawaza kujenga ghorofa tena kwa miezi kadhaa tu. Sasa huyu utasemaj anaharibu fedha kujenga ghorofa kisa wewe unajenga Kinyumba cha room 2/3 kwa miaka 4.

What's good for you should remain good for you, and what's good for others should remain good for others. People cannot live homogeneous, and in any society classes are inevitable. Msituchoshe na mada wengevu.

Said: BANDOKITITA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…