Watanzania wenye vipato vya chini wanao somesha English Mediums wanateseka hadi nawaonea huruma

Hivi unajua pale Udsm wanafunzi wengi wametokea Kayumba?

Alafu Kayumba Akiwa kichwa ujue ni kichwa kweli.

Mchukue kichwa wa Kayumba aliyepata One ya 7 alafu mchukue wa St. Aliyepata one ya 7 waweke waparangane Uone kama huyo wa St ataambulia chochote.

Pale Udsm au nenda Mzumbe Waliosoma EM hupata wakati mgumu Sana kukabiliana na mazingira ya chuoni.
 
Sahihi kabisa mkuu halafu huyo hajasoma Udsm . Tulio soma UD tunamshangaa
 
Sio kupangiana maisha Kaka ,shida ni kuwa wanasumbua Sana muda huu kutaka tuwakope na bado kulipa mpaka uanze kutaja mizimu ya ukoo ndiyo anaogopa.

Sasa kwanini tusiwashauri maana Sasa tumewachoka Sana hawa jamaa.
 
Nakubaliana na wewe, lakini ni bora huko EM angalau atapata hata hiko kidogo Kwa maana ya Lugha, confidence na kidogo kilichopo kwenye mtaala.
Huyu wa EM anayesoma darasa lenye watoto 20 akawa sawa na anayesoma kwenye darasa lenye watoto 200.
Huyu wa EM ambaye at least mchana anapata lunch ya kueleweka hawezi kuwa sawa na huyu ambaye anashinda njaa kutwa nzima.

Lakini kwanini watu wanakimbilia EM, naamini ni katika hali ya kutapatapa baada ya shule za serikali kuwa na hali mbaya( kuzidiwa + maslahi duni ya walimu).
 
Kayumba vipaji maalumu ndio wengi hujiunga na UDSM waliosoma shule za vipaji maalumu kama Mzumbe,Kibaha tabora nk

Nje ya kutoka shule za vipaji maalumu wachache sana huingia UDSM kutoka shule za serikali
 
Point muhimu sana.
 
Muongo wewe nimesoma Udsm na sijapita shule hizo
 
Uko sahihi

Halafu pita nje ya madarasa ya shule za Kayumba watoto mwalimu kama hajaingia wanapiga makelele hatari utafikiri wako kilabuni hata kama kuna mtoto anataka ajisomee hawezi

Lakini pita shule za private watoto unakuta wako kimya utafikiri.darasa halina wanafunzi wanajisomea wamefunzwa nidhamu kuwa kama mwalimu hajaingia wafanye nini na wanatii

Kayumba mazingira ya mtoto hata kujisomea mwenyewe kama mwalimu hajaingia sio rafiki tofauti na English medium
 
Kayumba vipaji maalumu ndio wengi hujiunga na UDSM waliosoma shule za vipaji maalumu kama Mzumbe,Kibaha tabora nk

Nje ya kutoka shule za vipaji maalumu wachache sana huingia UDSM kutoka shule za serikali
Kimbia kwenye kibatani Cha "DELETE" Futa haraka Sana haya maneno kabla hawajaja wenye PHD na masters zao na wamepita hapo jalalani Ila wametoka shule za kawaida .

Nakupa mbinu ya kufuta maana hao hawapendi kumfokea mtu kwa kiswahili utapigwa kingereza Cha kuchambwa kutoka Uingereza ya mbali mpaka utakoma kwa maneno yao kuntu
 
Uko sahihi

Halafu pita nje ya madarasa ya shule za Kayumba watoto mwalimu kama hajaingia wanapiga makelele hatari utafikiri wako kilabuni hata kama kuna mtoto anataka ajisomee hawezi

Ulitaka wafanye Nini mkuu? Watoto wanatakiwa kufurahia utoto wao na sehemu ya kufurahia utoto wao ni shuleni
Lakini pita shule za private watoto unakuta wako kimya

This is child abuse. Watoto wanatakiwa kuwa na furaha muda wote. Acheni kuwatesa watoto wenu
urafikiri.darasa halina wanafunzi wanajisomea wamefunzwa nidhamu kuwa kama mwalimu hajaingia wafanye nini na wanatii

Kayumba mazingira ya mtoto hata kujisomea mwenyewe kama mwalimu hajaingia sio rafiki tofauti na English medium
 
Sio kupangiana maisha Kaka ,shida ni kuwa wanasumbua Sana muda huu kutaka tuwakope na bado kulipa mpaka uanze kutaja mizimu ya ukoo ndiyo anaogopa.

Sasa kwanini tusiwashauri maana Sasa tumewachoka Sana hawa jamaa.
Kwenye utu uzima majibu huwa ni rahisi tu, "Sina ningekuwa nayo ningekusaidia."

Kitendo cha kumpeleka mtoto St Kayumba inamaanisha umejipima huwezi ghalama za huko. Hiyo inamaanisha hata uwezo wa kukopesha si kwa watu wa medium ni wa watu wa St Kayumba. Akija wa huko hakopi 200,000 au 400,000 anakopa 50,000 au 30,000. Unaanzaje kukopesha mtu akalipe ada ya medium school wakati wa kwako yuko Kayumba? Utakuwa uiinga. Kopesha kulingana na uwezo.
 
Kayumba vipaji maalumu ndio wengi hujiunga na UDSM waliosoma shule za vipaji maalumu kama Mzumbe,Kibaha tabora nk

Nje ya kutoka shule za vipaji maalumu wachache sana huingia UDSM kutoka shule za serikali
Upo sahihi Mkuu! Inawezekana alikuwa anamaanisha hao wanaotoka Kayumba wapo wengi UDSM bila kujali wanasomea Fani gani! Lakini ukweli ni kwamba kwa zile fani ambazo zina ushindani mkubwa kuzipata na asilimia kubwa na wanaochaguliwa kusoma fani hizo wanatoka Private schools
 
Muongo wewe nimesoma Udsm na sijapita shule hizo
Itakuwa enzi zile shule chache za private na enzi ambazo UDSM ilikuwa ikichukua hadi waliopata division three kusoma

Sasa hivi division three hakanyagi UDSM

Wanachukua wakali hasa division mtu awe na one na two kali form four na six kwa mpigo

Ila wengi waingia pale ni wenye division one form four na six

Enzi zako za somba somba sasa hivi hazipo UDSM
 
Ulitaka wafanye Nini mkuu? Watoto wanatakiwa kufurahia utoto wao na sehemu ya kufurahia utoto wao ni shuleni
Shule za private zinakuwa na ratiba ya michezo sio kucheza darasani na kupiga makelele darasani

Kayumba hata darasa la saba kama mwalimu hajaingia makelele yapo palepsle
 
Kaka sijakuelewa vizuri unaninang'a Mimi au hawa jamaa wa English Medium ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…