Watanzania wenzangu sasa ni wakati wa kuwa makini na wanasiasa wanafiki, waongo na wanaotumika kucheza na akili zetu kama huyu

Watanzania wenzangu sasa ni wakati wa kuwa makini na wanasiasa wanafiki, waongo na wanaotumika kucheza na akili zetu kama huyu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Asubuhi....

"Jamani Watanzania wenzangu nafuatiliwa na Watu wa CCM na Gari zao wakiwa na Panga, Sime na Mundu huku Kura za Uwizi zikiwa zimepakiwa mniombee nisife kwani nami nina Familia na Bata nalipenda vile vile na hiki Cbama sitaki nimuachie kabisa Mtu mwingine "

Usiku....

"Nampongeza sana Mshindi wa CCM kwa Kushinda kihalali kabisa na Uchaguzi ulikuwa ni wa Huru na Haki ila Sisi TCA Patriots tunamwambia tutakutana nae 2025 "

Na bahati nzuri tu ni kwamba GENTAMYCINE sijawahi kumkubali huyu Lake Tanganyika Political Pimp ( japo ni mwana Simba SC na Liverpool FC Mwenzangu) kutokana tu na Roho yangu Kumkataa japo pia ni Mtani wangu kutoka Kabila ambalo ukikosea ukapanda nao Basi la Mkoani wao tangia alfajiri mnaondoka hadi Usiku mnafika ndani ya basi wanaongea na kubishana wao tu kwa sauti za juu kabisa na wakikukogesha na mimate yao iliyokomaa.

Na sijui kwanini Watanzania wengi (tena wasiojielewa kabisa) wanamuamini vilivyo huyu Lake Tanganyika Political Pimp wakati nikimlinganisha na Wanasiasa wanaojitambua na wanaojua wanafanya nini katika Siasa za Tanzania yeye hata katika list yangu tu ya Kumi (10) Bora hayumo.

Hivi kwa aina ya Wanasiasa Opportunists kama huyo Lake Tanganyika Political Pimp CCM (Chama ambacho GENTAMYCINE ninachokishabikia Daima) kikiwa kinashinda na Kuongoza vyema Tanzania kila mara kutakuwa na tatizo?

Upinzani Tanzania bado sana kiukweli.
 
Wewe ni mwana CCM mchumia tumbo siasa za upinzani zinakuhusu nini?

Sisi wapinzani halisi tumeuchuna wewe unawashwa washwa nini.
 
Gari moja ina watu wana mapanga !
Lakini huyu jamaa mbona kaharibikiwa kiasi hiki sasa?

Na kajiachia kabisa watu waondoe mashaka juu yake kuhusu hizi tabia zake za ajabu?

Kakata tamaa?

Ni kijana mjenga hoja mzuri sana, msomi wa kueleweka kwa kipimo chochote kile..., sasa tena imekuwaje?

Kajiachia kabisaaaaa, watu wasiwe na shaka tena yeye ni mtu wa namna gani?
 
Wewe ni mwanaccm Mchumia tumbo siasa za upinzani zinakuhusu nini?

Sisi wapinzani halisi tumeuchuna wewe unawashwa washwa nini.
Kwani ukiwa Shabiki wa Simba SC huwezi ukawa unashauri Jambo jema la Kimchezo kwa Yanga SC na hata kuwapenda baadhi ya Wachezaji wake?

Umechangia Kiuswahili na Kipuuzi sana.
 
Lakini huyu jamaa mbona kaharibikiwa kiasi hiki sasa?

Na kajiachia kabisa watu waondoe mashaka juu yake kuhusu hizi tabia zake za ajabu?

Kakata tamaa?

Ni kijana mjenga hoja mzuri sana, msomi wa kueleweka kwa kipimo chochote kile..., sasa tena imekuwaje?

Kajiachia kabisaaaaa, watu wasiwe na shaka tena yeye ni mtu wa namna gani?
Anayemuani nae ni Mpuuzi Mwenzie tu.
 
Wewe unaeshabikia CCM una tofauti gani na huyo Zitto?

We mwenyewe mara uilalamikie CCM mara uwapigie debe yaani hujui unachokita au kukipigania hivyo huna tofauti na wapinzani feki aina ya Zitto.

Nyiny ndio mnachangia kuibeba CCM.
 
Back
Top Bottom