Watatu jela maisha kwa kukutwa na kemikali za kutengeneza ‘Smart Gin’, ‘Double Kick’

Watatu jela maisha kwa kukutwa na kemikali za kutengeneza ‘Smart Gin’, ‘Double Kick’

Ethanol inauaje mkuu? Kwani Konyagi, K-Vant, Smart Gin N.k zinatengenezwa kwa kemikali gani?. Hawa kosa lao ni kuwa ni hiyo kemikali kinyume cha sheria, na pengine kutengeneza vinywaji bandia kwa kutumia majina ya vinywaji halisi, na pia inawezekana hawakuwa wakifuata hatua sahihi za utengenezaji, na makosa hayo mengine ya uhujumu uchumi.
 
Hapana hao ni matapeli na wapo teyari kudhuru maisha ya watu bila kujali..
Sema adhabu hiyo ni kubwa sana.
Adhabubu ni sawa na kosa walilofanya.
Bidhaa walizosambaza zimesababisha madhara kwa watumiaji wengi.
Acha walipie madhara ya kiafya waliyosababishia jamii.
 
Adhabubu ni sawa na kosa walilofanya.
Bidhaa walizosambaza zimesababisha madhara kwa watumiaji wengi.
Acha walipie madhara ya kiafya waliyosababishia jamii.
Serikali ingelikuwa na nia ya dhati ya kuwalinda raia wake. Pombe zote za bei chee hazikutakiwa kuwa mitaani. Maafisa kutoka mamlaka husika wanaujua ukweli na wameamua kula kwa urefu wa kamba zao na kuwaacha wananchi wapambane na hali zao.

Ripoti za kiutafiti toka baadhi ya majiji hapa nchini iliyofanywa na vyombo vya serikali inajua ukweli wote na ripoti wamezikalia. Wameamua kuwa kodi ni muhimu kuliko usalama wa wananchi.
 
Kwa Ulaya hawa wangesaidiwa wakaanzisha kiwanda halali, bongo wanafungwa maisha!
Kuna nchi hawa jamaa wangepigwa risasi ama kunyongwa kimya kimyaa

Madhara walokwisha sababisha ni makubwa (afya za watu, kukosesha mapato, kuharibu nembo ya biashara ya mwanzilishi etc) kuliko kuwawezesha
 
Acha uanahatakati kwenye maisha ya watu.
Kwani hizo kemikali waniiba?
Kama walinunua maana yake walikuwa na pesa

Hao ni wauaji kama wengine
Kwa Ulaya hawa wangesaidiwa wakaanzisha kiwanda halali, bongo wanafungwa maisha!
 
Jera maisha! Hv Daniel yona, na Pesambili mramba walifungwa miaka mingapi jera?
Nakumbuka Mramba kwa kesi ya ufisadi wa mambilioni ya TSh, alipewa kifungo cha nje, akawa anapelekwa hoapitsri ya mnazi, mmoja kufagia! Eti ndio adhabu,
Wakati huo V8 lake limepaki pembeni lipo silence!
Wadogo zangu Bora uibe pesa nyingi aiseee
Walihusika katika kuua watu?
 
BAADA YA KUSOMEWA ADHABU YA KIFUNGO KATIKA UTETEZI WAKE MSHITAKIWA NAMBA MOJA ALISEMA NANUKUU " MHE. HAKIMU NAANZA KWA KUMSHUKURU MWENYEZI MUNGU KWA KUNIWEZESHA KUFIKA MAHAKAMANI HAPA, PIA NINAKUSHUKURU MHE. HAKIMU KWA KUNIPA ADHABU STAHIKI KULINGANA NA SHERIA KWA KOSA NILILOTENDA, MWISHO NINAAMINI SIKUTENDA HILO KOSA KWANI USHAHIDI WA VITU VILIVYOLETWA HAPA MAHAKAMANI SIVYO NILIVYOKUTWA NAVYO", MWISHO WA KUNUKUU.
 
Wanapenda pesa za bure??
Sasa wanaenda kula na kulala kwa ratiba.
Wangese sana hao wajuba.
 
Kwa bongo hata aliyempiga shoka mtu hadharani mbele za watu na kumuua hanyongwi (wanaosaini kunyonga wanadaiwa eti kuogopa dhambi), ndio wanyongwe hawa ambao hata hatuna uhakika kama wameua mtu?
Hata mimi nimejiuliza haina mantiki hata kidogo,matumbo ya walevi yalivyokuwa sugu huwa hawafi kirahisirahisi hivyo.
Hukumu yao ilitakiwa ikizidi sana ni miaka 5 ingewatosha wakirudi uraiani watatafuta shughuli halali ya kufanya.
Yaani mafisadi wanaoiba matrilioni na kusababisha umaskini kwa watanzania milioni 6 wanajiachia tu mtaani halafu mtu anayefoji kvant/konyagi kupata senti za kula aende jela milele.
 
Nakazia hoja. Hapo inaelekea Kuna kitu nyuma ya pazia kwa Polisi, Hakimu na Adhabu waliyopewa hawa jamaa.
Hata mimi nahisi kuna kamchezo walitaka kucheza kakafeli mwishoni wakatoa adhabu kwa hasira kukomoana maana sio bure haiwezekani mtu aliyekutwa na ethanol apewe adhabu sawa na mtu mwenye murder case.
 
Back
Top Bottom