Watatu jela maisha kwa kukutwa na kemikali za kutengeneza ‘Smart Gin’, ‘Double Kick’

Watatu jela maisha kwa kukutwa na kemikali za kutengeneza ‘Smart Gin’, ‘Double Kick’

Kwa Ulaya hawa wangesaidiwa wakaanzisha kiwanda halali, bongo wanafungwa maisha!
Ulaya ipi unayoiongelea hapa? unajua kua kitendo chao hicho kinahatarifa afya za watumiaji?
Hiyo ni criminal offence of forgery,inawezekana kabisa kuna watu wanateseka na maradhi au wengine wameshakufa kwa kunywa hizo pombe fake.
 
Badala ya kuwafunga jela, wangetolewa figo zao ili wapewe wagonjwa walioharibika figo kwa pombe huko mahospitalini
 
Acha wafungwe.
Ungeona vijana wakinyakyusa wanavyoharibiwa na k vant feki huku Kimara mwisho ungemnunulia huyo Hakimu soda.
1. Acha wafungwe kihalali na sio wafungwe kwa kukandamizwa. Kufungwa maisha hakumrekebishi tena mtu bali inakuwa ni last alternative kwa wale waliokubuhu na walio sugu hawawezi tena kujirekebisha na tena uwepo wao uraiani ni tishio kwa usalama wa Raia wengine.
2. Sio kweli. Vijana unaowasemea, hao wameharibika kwa Unywaji wa gongo na energy na ulaji hafifu (Chips dume) kwa muda mrefu.
3. Hakimu aliyehusika hajaonesha Umahiri wake kwani yule Hakimu wa Iringa aliyetoa adhabu 22 yrs kwa aliyekutwa na kg.12 za nyama pori alitumia sheria ipi ambayo huyu anayewahukumu kifungo cha maisha ameshindwa kuipata? Inaelekea huyo Hakimu ni mvivu na hataki kujiongeza au ni Hakimu mkatili asiye na huruma utadhani hiyo Ethanol ilikuwa ni mali yake iliyoibiwa.
 
Je, ni sheria hiyo hiyo inayoruhusu upande mmoja na kubana kwa wengine? Kama ishu ni kutokuwa na Kibali, Je, adhabu iliyoainishwa ni kifungo cha maisha? Mbona yule mama aliyekamatwa na nyamapori alihukumiwa 22 yrs. Yeye ilikuwaje kwani alikuwa na kibali cha kumiliki hiyo kg. 12 nyama pori?
Huyo Hakimu hakuweza kutumia weledi hata kidogo. Wenye viwanda au TRA wamepata hasara kubwa kiasi gani hata Jamhuri (Polisi na Hakimu) kuona ni halali hao ndg. Wafungwe maisha?
hawa wamekutwa na nyara pia wamekutwa na kosa la kuhatarisha uhai ushaona tofaut sasa!
yaani hawa wahuni huko kwenye vifungu vya sheria tafsiri zake wanajikuta mpaka kwenye kesi za madawa ya kulevya ni mwanasheria mzuri na mlungura tu vingeweza kuwachomoa
 
Mkuu leo napingana na wewe. Hawa hawana tofauti na wauwaji kwakuwa wameharibu maisha ya vijana wengi sana kwa kuwanywesha sumu.
1.Maisha ya Vijana wengi yameharibika kwa vijana hao kuwa wakaidi, wakorofi na kutozingatia ushauri wanaopewa. Wanakwenda kunywa hayo mavitu kwa hiari yao wenyewe.
2. Ipo changamoto kubwa sana kwa sasa hv hapa nchini ya Ukosefu wa Ajira. Jambo hili la ukosefu wa ajira limepelekea vijana wengi baada ya masomo kuwa Idle. Hii inawaletea msongo wa mawazo (sonona au stress) na kwa ujinga wao hao vijana hawasikii tena ushauri ila wamekaza shingo na wanaona kwenda kujilipua( Ulevi) ndo ufumbuzi.
Ethanol sio sumu. Ingekuwa ni sumu, basi watu wengi sana (wote wanaokunywa Kilevi) wangelikuwa wameuawa na sumu hiyo. Lakini ukizingatia "Too much of anything is harmful" ndo mana hata wale wanywaji wa siku zote akizidisha hudhurikai.e. hiyo-hiyo pombe/kilevi huwa ni sumu kwake.
 
Majizi na mataperi ya taifa yame tiwa nyavuni.
Safi sana hakimu
 
hawa wamekutwa na nyara pia wamekutwa na kosa la kuhatarisha uhai ushaona tofaut sasa!
yaani hawa wahuni huko kwenye vifungu vya sheria tafsiri zake wanajikuta mpaka kwenye kesi za madawa ya kulevya ni mwanasheria mzuri na mlungura tu vingeweza kuwachomoa
Dah! umaskini wetu huu! Laiti wakipata msamaria TLS au LHRC wakachomoa; nina uhakika hao dogo hawatokaa warudie tena.
Halafu utakuta hata hayo maokoto waliokuwa wanapata ni kidogo sana.
 
Mkuu hapana wangefungwa lakini siyo maisha. Wakitoka gerezan hata kuajiriwa itakuwa ngumu kwasababu ya record yao hata kama ni wataalam.
Yan kwa kweli hiyo adhabu sio size yao. Imepitiliza mno.
 
Dah! umaskini wetu huu! Laiti wakipata msamaria TLS au LHRC wakachomoa; nina uhakika hao dogo hawatokaa warudie tena.
Halafu utakuta hata hayo maokoto waliokuwa wanapata ni kidogo sana.
kabisa mkuu wote tunafanya makosa sema tu wao wamekamatwa kosa lao kubwa lilikua ni kujitetea wenyewe, sheria zetu zina loopholes kibao zakutokea ukiwa na mtaalamu wakucheza na vifungu
 
kabisa mkuu wote tunafanya makosa sema tu wao wamekamatwa kosa lao kubwa lilikua ni kujitetea wenyewe, sheria zetu zina loopholes kibao zakutokea ukiwa na mtaalamu wakucheza na vifungu
Yes-Exactly mkuu. Ila naona bado wanayo karata moja hawajaicheza. Kukata rufaa. na kipindi cha kusubiria rufaa yao waombe wawe nje kwa dhamana. Hiyo ikikubaliwa wanaweza wakachomeka karata zingine..
 
Je, ni sheria hiyo hiyo inayoruhusu upande mmoja na kubana kwa wengine? Kama ishu ni kutokuwa na Kibali, Je, adhabu iliyoainishwa ni kifungo cha maisha? Mbona yule mama aliyekamatwa na nyamapori alihukumiwa 22 yrs. Yeye ilikuwaje kwani alikuwa na kibali cha kumiliki hiyo kg. 12 nyama pori?
Huyo Hakimu hakuweza kutumia weledi hata kidogo. Wenye viwanda au TRA wamepata hasara kubwa kiasi gani hata Jamhuri (Polisi na Hakimu) kuona ni halali hao ndg. Wafungwe maisha?
All in all
Jamhuri haijawatendea haki Hawa jamaa..
Na for sure wangekua wanawake wangetetewa mpaka Waka achiwa huru
Ila wanaume unakaa nyuma ya nondo Tena Maisha
 
Majizi na mataperi ya taifa yame tiwa nyavuni.
Safi sana hakimu
Kha! Yan Ukipambana kwa udi na uvumba ili walau uendelee kuishi (ku-survive)unaitwa tena ni majizi na matapeli- dah! ukicheza rafu unaitwa Jambazi. Ukiamua kujilipua unaitwa ww ni Teja. Ukiamua kutumia mbinu mbadala unaitwa ww ni shoga au unadanga/malaya. Ukiamua kuwa mtulivu na mtiifu kwa serikali iliyo madarakani unaitwa ww ni chawa. Mwe! Eeehee! Twiifwa nye vwanu -lekagha bee.
 
Wasumbufu sana washenzi hawa hawakwepeki mkuu.Tatizo linakuja hivi,huwezi kufa kama ulivyo lazima uwe na watoto ndio maana nasema hawakwepeki
 
Back
Top Bottom