Wateja wa Mabenki chukueni tahadhari kubwa, kuna wizi kwenye tozo na commission zao

Hizi pesa ndizo baadae ccm huchukua kiasi fulani kuendeshea mambo yao hasa chaguzi.
 
Huu wizi unaofanyika sana, na vile watu wengi hatuko makini basi hilo linafanyika kirahisi sana. Usishangae ukakuta serikali inajua jambo hili, na si ajabu ni wafaidika wa huu uhuni.
 
Baada ya tozo za madelu kuanza nilikuta CRDB wamelamba laki na kumi na tano kwenye akaunti yangu, nilivyofuatilia kwenye statement ndo nikakutana na hayo makato lukuki ambayo mengine hayaeleweki wanakata nini na yanaweza kujirudia mfululizo kabla hujatoa pesa nyingine.

Walinimbia niandike barua kwa meneja kulalamika, lakini niliona hawafuatilii chochote zaidi ya kunipotezea muda. Baada ya hapo siamini kabisa pesa zangu kukaa benki, kiasi kwamba hata ukinilipa milioni tano sasa hivi benki naweza kuvunja miguu kwenda kuichomoa.

Huu utaratibu wa madelu kuvuna pesa za watu kwenye mabenki na kwenye miamala ya simu ni utaratibu uliopitwa na wakati sawasawa na kipindi cha kodi ya kichwa ambayo Mkapa aliiondoa, eti mchumi first class....​
 
CRDB wanalalamikiwa sana kila Kona.

Kama wapo humu wasikie hili,hata Mimi haya maeneo niliyopo CRDB kila mtu anasema ni Wezi Wezi.Ushauri wangu kwao wafuate miongozo ya kazi na makato halisi kama yanavyojieleza.Watu watawakimbia kwa style hii.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…