Wateja wa Mabenki chukueni tahadhari kubwa, kuna wizi kwenye tozo na commission zao

Ndugu wana-JF, kumbe tulipoambiwa kuwa eti Serikali imesikia kilio cha wananchi kuhusu tozo, na hivyo kuamua kupunguza, inaelekea ilikuwa ni hadaa kubwa. Sikuwa na kawaida ya kuomba bank statement kama hakuna sababu ya msingi. Safari hii, kuna account yangu moja iliyopo CRDB Bank ambayo huwa naitumia kwa matumizi yangu yangu binafsi, nikaamua niombe bank statement. Nilichokutana nacho, nimeshangaa sana.

Kuna wizi au unafanywa kwa makusudi au system zao zimefeli, na hivyo zinawaibia wateja. Japo kwa kweli kufeli kwa system siamini sana kwa sababu sehemu zote imekuwa ni kuibiwa kwa mteja, hakuna ambapo ama mteja amekosa kukatwa tozo au fees.

Kwa mfano, siku 1 ambapo nilitoa sh 400,000 kwenye ATM, nilikatwa cash withdraw commission mara 1, TMS government levy mara 3, VAT mara 5, kwa muamala huo huo mmpja wa shiliko laki 4, mnaweza kuangalia kwenye hiyo bank statement.

Hizi pesa kwa sababu zinakuwa ni kiasi kidogo, unaweza kuwa unakatwa bila ya wewe kutambua. Nina imani siyo mimi pekee, kuna uwezekano mkubwa wengi wanafanyiwa mambo haya.
Sawa kabisa hata mie wananikataga mara 2 mbili hata hizo tozo
 
Vuta statement ya miaka mitano uone?
Natafuta wakili Kibatala aniambie hapo tunapiga ngapi? Tuanze mchakato

Kwa kweli haya mabenki bila kuyafikisha mahakamani, yataendelea na huu wizi. Wanatamba wametengeneza faida kumbe ni kwa kuwaibia wateja.

Fikiria muamala mmoja wanaiba kama sh 2,000 hivi. Mwezi mmoja ukitoa pesa yako kupitia ATM 10m, ina maana watakuwa wamekuibia = 10,000,000÷400,000 = 25×2,000=50,000. Wakifanya hivyo kwa wateja 10,000; watakuwa wamefanikiwa kuiba = 50,000×10,000 = 500,000,000 kwa mwezi. Kwa mwaka, watatengeneza bilioni 6.

Kuna benki nyingine, siitaji jina kwa sababu waliomba sana msamaha. Wao kwenye miamala miwili ya jumla ya shilingi laki 8, nilitoa kwenye ATM kutoka kwenye account yangu ya dola, walinikata tozo dola 2,700. Yaani nilitoa laki 8, halafu tozo ikawa zaidi ya shilingi milioni 6. Yaani system yao ikawa inazikata dola kama shilingi. Baada ya kulalamika, walirudisha baada ya siku 5.
 
Nadhani shida sio maBank shida ni watawala wetu wanaotaka kuvuna wasipopanda ..wee humsikii yule Waziri anaefanyaga kazi ya uafisa habari wa mitandao ya simu?....tungekuwa na watawala wanaojali watu wao wasingekuwa wanaweka makodi ya hovyo hovyo

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Ulivyowauliza walikupa jibu gani ?

Nadhani huo ndio utakuwa mwanzo mzuri; yaani hatua ya kwanza...
 
Ndugu wana-JF, kumbe tulipoambiwa kuwa eti Serikali imesikia kilio cha wananchi kuhusu tozo, na hivyo kuamua kupunguza, inaelekea ilikuwa ni hadaa kubwa. Sikuwa na kawaida ya kuomba bank statement kama hakuna sababu ya msingi. Safari hii, kuna account yangu moja iliyopo CRDB Bank ambayo huwa naitumia kwa matumizi yangu yangu binafsi, nikaamua niombe bank statement. Nilichokutana nacho, nimeshangaa sana.

Kuna wizi au unafanywa kwa makusudi au system zao zimefeli, na hivyo zinawaibia wateja. Japo kwa kweli kufeli kwa system siamini sana kwa sababu sehemu zote imekuwa ni kuibiwa kwa mteja, hakuna ambapo ama mteja amekosa kukatwa tozo au fees.

Kwa mfano, siku 1 ambapo nilitoa sh 400,000 kwenye ATM, nilikatwa cash withdraw commission mara 1, TMS government levy mara 3, VAT mara 5, kwa muamala huo huo mmpja wa shiliko laki 4.

Hizi pesa kwa sababu zinakuwa ni kiasi kidogo, unaweza kuwa unakatwa bila ya wewe kutambua. Nina imani siyo mimi pekee, kuna uwezekano mkubwa wengi wanafanyiwa mambo haya.
Pole sana kiongozi
 
Picha inajieleza jinsi masikini wanavyokamuliwa
Screenshot_20230213_142900_Twitter.jpg
 
Kwa kweli haya mabenki bila kuyafikisha mahakamani, yataendelea na huu wizi. Wanatamba wametengeneza faida kumbe ni kwa kuwaibia wateja.

Fikiria muamala mmoja wanaiba kama sh 2,000 hivi. Mwezi mmoja ukitoa pesa yako kupitia ATM 10m, ina maana watakuwa wamekuibia = 10,000,000÷400,000 = 25×2,000=50,000. Wakifanya hivyo kwa wateja 10,000; watakuwa wamefanikiwa kuiba = 50,000×10,000 = 500,000,000 kwa mwezi. Kwa mwaka, watatengeneza bilioni 6.

Kuna benki nyingine, siitaji jina kwa sababu waliomba sana msamaha. Wao kwenye miamala miwili ya jumla ya shilingi laki 8, nilitoa kwenye ATM kutoka kwenye account yangu ya dola, walinikata tozo dola 2,700. Yaani nilitoa laki 8, halafu tozo ikawa zaidi ya shilingi milioni 6. Yaani system yao ikawa inazikata dola kama shilingi. Baada ya kulalamika, walirudisha baada ya siku 5.
Description ya miamala hiyo hua haieleweki.
Unakutana na WVCXZ imekata 372.69.
hujui hata ni ya nini?

Kuna kitu natega hiyo 2024, mtaisikia hapa.
 
Kwa kweli haya mabenki bila kuyafikisha mahakamani, yataendelea na huu wizi. Wanatamba wametengeneza faida kumbe ni kwa kuwaibia wateja.

Fikiria muamala mmoja wanaiba kama sh 2,000 hivi. Mwezi mmoja ukitoa pesa yako kupitia ATM 10m, ina maana watakuwa wamekuibia = 10,000,000÷400,000 = 25×2,000=50,000. Wakifanya hivyo kwa wateja 10,000; watakuwa wamefanikiwa kuiba = 50,000×10,000 = 500,000,000 kwa mwezi. Kwa mwaka, watatengeneza bilioni 6.

Kuna benki nyingine, siitaji jina kwa sababu waliomba sana msamaha. Wao kwenye miamala miwili ya jumla ya shilingi laki 8, nilitoa kwenye ATM kutoka kwenye account yangu ya dola, walinikata tozo dola 2,700. Yaani nilitoa laki 8, halafu tozo ikawa zaidi ya shilingi milioni 6. Yaani system yao ikawa inazikata dola kama shilingi. Baada ya kulalamika, walirudisha baada ya siku 5.
Huu upuuzi uliletwa na Mwigulu baada kuingiza Biashara ya tozo,mimi niliamua kutoa pesa zangu Benki nikanunua viwanja na mashamba.Benki nabakiza pesa ya kula na zingine nazungusha kwenye Biashara.
Benki zetu uwizi mwingi sana!
 
Hapo Wanaosema Anaupiga Wanepatwa Butwaa, Hali Tete Sana Kama Turkey Na Syria Vile
CCcmHoyee,Hawa Watatuuwa Tunaona
 
Back
Top Bottom