Kwa kweli haya mabenki bila kuyafikisha mahakamani, yataendelea na huu wizi. Wanatamba wametengeneza faida kumbe ni kwa kuwaibia wateja.
Fikiria muamala mmoja wanaiba kama sh 2,000 hivi. Mwezi mmoja ukitoa pesa yako kupitia ATM 10m, ina maana watakuwa wamekuibia = 10,000,000÷400,000 = 25×2,000=50,000. Wakifanya hivyo kwa wateja 10,000; watakuwa wamefanikiwa kuiba = 50,000×10,000 = 500,000,000 kwa mwezi. Kwa mwaka, watatengeneza bilioni 6.
Kuna benki nyingine, siitaji jina kwa sababu waliomba sana msamaha. Wao kwenye miamala miwili ya jumla ya shilingi laki 8, nilitoa kwenye ATM kutoka kwenye account yangu ya dola, walinikata tozo dola 2,700. Yaani nilitoa laki 8, halafu tozo ikawa zaidi ya shilingi milioni 6. Yaani system yao ikawa inazikata dola kama shilingi. Baada ya kulalamika, walirudisha baada ya siku 5.