Ni jambo lililodhahiri kwa wengi, juu ya nani ni watekaji na wauaji wa watu wanaowakosoa watawala. Bahati mbaya sana hawa wafuasi wa shetani, wanafanya kila jitihada kuubariki uovu wao kwa kwenda kwenye nyumba za ibada ili kuuficha au kuuhalalisha uovu wao. Na hawa ndiyo mara nyingi wakienda kwenye nyumba za ibada, wanataka wapewe muda wa kuhutubia kanisani, na wakipewa nafasi, kazi kubwa wanayofanya ni kuwasifia watu wao waliopo kwenye Syndicate yao ya utekaji na mauji ya wanaoikosoa Serikali na watawala.
Hata kama viongozi wa dini hawawezi kuwaadhibu hawa watu, lakini kuwaruhusu hawa watu wa kiwango cha juu kabisa cha uovu kuuhalalisha ushetani wao makanisani na misikitini, ni kufuru kubwa dhidi ya Muumba wetu wa HAKI.
Hapo zamani nilishuhudia Kanisa Katoliki likigomea kutoa ushirikiano kwa waovu wanaotaka kuhalalisha uovu wao kwa kujikamanisha na Kanisa.
Bila ya kujali, hao watu wana uwezo wa kutoa pesa kiasi gani kwaajili ya maendeleo ya Kanisa, Kanisa linatakiwa kujitenga na hawa watu. Hawa watu waruhusiwe kuja kanisani pale tu wanapoamua kwenda kuutubu uovu wao na kutaka kumrudia Mungu wa haki. Vinginevyo, wabakie huko huko, waendelee kumkumbatia shetani wao wanayemtumikia kwa nguvu zao zote.
Kanisa litakuwa linafanya kosa kubwa sana kujishikamanisha na hawa waovu ambao wanajaribu hata kutaka kuwaua viongozi wa dini wanaokemea uovu au makosa yanayotendwa na watawala.
Hawa waovu wapokelewe na kanisa kwaajili ya toba, na siyo kwaajili ya kuhalalisha au kuubariki uovu wao.