Nawasalimu sana kwa jina la JMT yetu pendwa!
Baada ya mheshimiwa raisi kuagiza fedha za IMF kwenda kwenye elimu na kujenga madarasa ili watoto wa kidato cha kwanza mwakani wasipate tabu ya kusubiri, na TAMISEMI kazipangia bajeti na kuzigawa, kazi imeanza huku chini (wilayani). Viongozi (wakurugenzi na maafisa elimu) wakiibuka na 'majuhudi' kibao ya kutaka kufanya 'maajabu' ili wawe wa mfano. Bahati mbaya sana, 'majuhudi' yao hayo, yanaenda kuwaangukia na kuwaumiza watendaji na zaidi wakuu wa shule.
Kwa siku chache tu, kuna halmashauri fulani, kwa wakati tofauti, tayari wakuu wa shule wameambiwa (of course kuamrishwa) yafuatayo:
1. Darasa lililolengwa likamilike lakini ni lazima na kitu kingine kitokee (yaani wahakikishe wameanzisha kitu kingine pia k.v boma, ofisi, choo n.k kutoka katika fedha hizo hizo)
2. Madarasa yawekwe marumaru (tiles)
3. Bati ziwekwe za msouth
4. Madirisha ya aluminium
5. Mfumo wa umeme wote ukamilike
Barua za kuwakabidhi fedha hizo zinaandaliwa kwenda kwa wakuu hao kwa majina yao na atakayeshindwa kukamilisha majengo hayo kwa viwango tajwa kazi anayo. Ikumbukwe kuwa fedha zilizotolewa ni Tsh. milioni 20 tu kwa chumba kimoja cha darasa. Hapo sidhani kama watendaji na wakuu hawa watakuwa na ujanja mwingine wowote zaidi ya kurudi kwa wanakijiji kuwaambia wajitolee.
AISEE! Kujitolea kipindi hiki ni vigumu kuliko maelezo, siajabu kijiji cha watu 2000 wakajitolea watu 7 tu tena kwa siku mbili tu.
Wakuu wa shule kiukweli kazi wanayo. Huku mitihani ya kitaifa, kule ujenzi uliyoongezewa maagizo. Dah!!!