Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Mwigulu ana Vision kubwa binafsi zaidi ya Uwaziri, Hata mwendezake aliwahi kumchana kuwa atulie afanye kazi zake mambo ya kuota Urais kila saa hayafai, Hawezi kutumikia vision mbili at a time yani Atekeleze mikakati ya wizara ya Fedha hapo hapo alinde vision ya kutaka Urais that cant be
Hata Assad pia hafai kuongoza hio Wizara abaki kuwa mshauri tu
 
Sina shaka hata kidogo Majaliwa kapelekewa tu hii taarifa!!

Lau kama Mwigulu Nchemba angekuwa ndo wa kwanza kulifahamu hili basi asingempelekea yeyote... haya yanayosomwa na PM yangesomwa na Mwigulu mwenyewe ili abebe cridit stahiki!!

Kama ndivyo, basi Mwigulu ama hakufahamu huu wizi wakati unafanyika au nae anahusika kwenye wizi huu!!

Iwe sababu ya kwanza au ya pili, SSH atathibitisha kwamba hafai kulinda maslahi ya umma endapo ataendelea kumwacha Mwigulu madarakani!!

Hilo la Mwigulu lina-apply pia kwa Katibu Mkuu wa Hadhina!! SSH atatupa picha kwamba nae ni mtu wa ovyo endapo Katibu Mkuu wa Hazina ataendelea kuwa madarakani!!

CCM wakati umefika wa kutimua uanachama viongozi wanaotokana na vyama pale inapoonekana wamehusika kwenye ushenzi kama huu.
 
1.5 billion kweli Mwigulu and team hakupata mgao? Hili ni la muhimu kuliwka wazi vinginevyo waache kusumbua watu hapa. Au nachanganya si ndiye Waziri wa Wizara ya fedha na Mipango yalikotokea maulaji
 
Wakat hela zinapigwa yeye alikuwa wizara ya ulinzi .... aliyekuwa incharge ni mpango ambaye Kwa kipind hcho alikuwa mahtuti kitandani pia , huku jiwe akiwa amekufa , kulikuwa na loophole kubwa Sana , tangu tetesi za jiwe kufa mpak mwez mei .... Wajanja wamepiga pesa chafu alaf wakatulia kama maji mtungini
 
Habari kama hizi zinasikitisha sana na kukatisha tamaa,huko bungeni kila mbunge analia na Tarura kukosa hela barabara mbovu, wengine wanaomba kodi ya uzalendo wabebeshwe wananchi. kumbe hela za kupiga zipoo telee. dah Mama asicheke nao kabisa,mwanzo mzuri,
 
Si tulikubaliana kuwa tunataka hela mtaani?
Hii ndio njia nzuri na haraka. Tatizo wabongo hatujui tunataka nini.
Rest in peace MAGUFULI!
Acha ujinga wewe! Aliyekuambia hatujui tunachotaka ni nani! Watanzania tulio wengi, tunataka Katiba Mpya ili CCM itoke madarakani kwa njia ya amani. Maana huko ndiko mchwa wanako jifichia.

Kwani huyo magufuli wako unayemlilia hapa alikuwa ni mtakatifu? Mbona na yeye alikuwa ni mpigaji tu! Unawezaje kuwa ndani ya serikali ya ccm halafu usiwe mwizi!
 
Inasikitisha sana. Wakati wanagawana Waziri wa fedha,na katibu wa wizara walikuwa wapi? Au na wao walihusika? Nchi hii inaliwa kizembe zembe sana.
Kuna kiasi cha pesa ambayo sio lazima KM aidhinishe. Wakuu wa idara katika wizara wana mamlaka ya kuidhinishe malipo hadi kiasi fulani. Sijui kwa wizara ya fedha ni kiasi gani?
 
Usikute yeye ndiye aliyeblow, hivyo hana kosa.

 
Akichoka kuangalia Shilawadu anakwenda kupanda mawe na kuota jua kama kenge, au kula mahindi barabarani. Mwendazake bora amekufa
Umesahau kujaza mafaili mezani na kupiga picha aonekane anafanya kazi, hajui kuwa boss anayejaza mafaili mezani pasipo kuyatoa ni dalili ya bosi mvivu asiyejua majukumu yake
 
Kuna kiasi cha pesa ambayo sio lazima KM aidhinishe. Wakuu wa idara katika wizara wana mamlaka ya kuidhinishe malipo hadi kiasi fulani. Sijui kwa wizara ya fedha ni kiasi gani?
Itakuwa mabilioni.watu siku mbili milioni 400, dah kufuru
 
Kwa mwendo huuu, sasa naanza kumwelewa Waziri Mkuu, tunamuomba kabisa awe mkali kwenye matumizi mabovu na ubadhirifu wa fedha za ummma, Bado wananchi wetu wanaishi kwenye dimbwi la umasikini wa kutupwa! halafu baadhi ya watumishi wanachota fedha bila hata huruma?!

Waziri wetu Mkuu tunakuomba linusuru taifa letu na watu wabadhirifu na wafujaji wa mali za umma, tubane matumizi ya serikali, tuangalie pia magari yanayo tumiwa na viongozi wetu yasiwe ya gharama kubwa. semina zisizo na tija, n.k
 
Acha ujinga wewe!
Watoke CCM waje chama gani?
Chama mbadala wa CCM kilikufa uchaguzi wa 2015. Hawa waliobaki ni bora CCM itawale milele!
 
Hasira zake zikimpanda hata kunyonga hazarani anaweza kwa jinsi waeja wa uporaji wanavyotekenya tekenya within a short time ,muda uliopita ka miezi hivi alikuwa na bado yale ya mzibiti wa hesabu za serikali kuwa kuna uharibifu n upotevu wa hela katika wizara ile,Raisi akajitutumua na kumleta waziri mpya mchapa kazi leo hii wizara ileile kunalipuka bomu ,aloo mama atauwa mtu ! Msimpandishe hasila kwanza sijahipo kumuona kucheka.Kwa hasira zinapopana bora magufuli kuliko huyu. Wakinamama hawachelewi kuchukua maamuzi magumu.
 
Tatizo pekee lilipo ni kutarajia matokeo tofauti kutoka kwa watu wale wale.

Hii nchi imekuwa kama vile viongozi ni wale wale tu wanabadilshiwa sehemu za kufanyia kazi tu.

Mama kama kweli anahitaji matokeo tofauti akae chini na kutafuta watu tofauti kabisa na makapi anayoyaweka. Na sio kama hakuna watu wenye weledi hasa na kazi zao tatizo ni kukariri majina yale yale tu.
 
Katibu Mkuu hazina anatokea mkoa gani ?
 
Inaonyesha walikuwa na njaa sana ,watakuwa ni miongoni mwa waliofurahu kifo cha magu ,yaani nj Kama mbwa wanaosubiri makubwa kwa hali na mali
Kipindi cha Magufuli ndiyo posho zisizo na kichwa wala miguu zilishamiri sana kwa sababu alipiga marufuku warsha na semina na pia kuanzishwa kwa Force Account ambako kuliwanyima wakandarasi kupata kazi za ujenzi serikalini.
 
Vyote ulivyoorodhesha vilishamiri enzi za Magufuli na alivilinda kwa nguvu zote ilimradi kuna chake amekinusa!
 
Sio kweli naona unaongea kishabiki
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…