Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Kwaiyo wewe unatakaje?unataka Rais anayefatilia watendaji wake au huyu tuliyenaye anayeshinda kwenye kioo anajipodoa utafikiri anatafuta mchumba,hapa atuna Rais tuna picha ya Rais tu,juzi tu tuliona Waziri mkuu anafukua madudu hapo UDAT mpaka akasimamisha watendaji wake,akabaki Mkurugenzi ambaye waziri mkuu,akuwa na uweza naye wa kutengua, akasema anampereka kwa Rais maana yeye ndiye alikuwa na mamlaka naye, mpaka sasahivi hatuoni chochote,yule Mkurugenzi bado yupo pale pamoja na madudu yote yale.Hapa atuna Rais tuna rais wa kutafuta wawekaji tu.
Mkurugenzi ashaondolewa wewe jamaa, Mkurugenzi mpya kateuliwa huu uteuzi wa juzi pamoja na jamaa wa Takukuru, nyie ndio walewale mnakurupuka tu kukashfu au kusifia bila hata kufuatilia kinachoendelea
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
hii habari imeniudhi sana. hivi hao mbwa bado wapo ofisini badala la selo/sero?
 
Huyu mzee naye huwa simwelewi hata kidogo ndiyo maana anapambana kupaka nywele rangi aonekane ni kijana maana ndiyo akili yake imeishia hapo kwa vidosho, watu wanapakua mabilioni akina Lugola, Makonda, Sabaya, Mnyeti n.k lakini ndiyo kwanza anacheka nao.
hayo hayaondoi uhalali wa hili alilolifanya.
 
Si tulikubaliana kuwa tunataka hela mtaani?
Hii ndio njia nzuri na haraka. Tatizo wabongo hatujui tunataka nini.
Rest in peace MAGUFULI!
 
Huyu nae ni sukuma gang.
Atulie km vp amfate mwendazake!
Walisikika vichaa fulani huko mtaa wa jamii forum.
 
Nikifikiri wapishi wa biriani/pilau ndio huonjaga kujua chungu kimeiva au la? Kumbe na fedha nazo zinaonjwa kujua ziko tayari kuingia kwenye mzunguko mkuu huko mitaani.
 
Kwa hivyo haujarejea!!!?
Urejee kutoka wapi? Kama ulikuwa hujui hayo masalia yake ni kwamba yanaendeleza tu wizi uliokuwepo!

Wakati wa yule shetani nani angethubutu kuhoji? Si afadhali ya sasa kwani hata Majaliwa ana ujasiri wa kuhoji!

Kwa ufahamisho zilikuwa zikichotwa labda zaidi ya hizo kwa amri/kauli yake!
 
Inapofika mahali waziri mkuu anaongea mambo ambayo waziri wa hiyo wizara angeongea maana yake huyo waziri hafai...tatizo mama yuko bize mitandaoni
Bora wa busy mitandaoni kuliko yule aliyekuwa anakesha kuangalia shilawadu na futuhi
 
So jumla sh ngapi??
Kwa mahesabu ya haraka haraka kama zinakaribia ama ni bilioni 2 [emoji849]

Halafu utakuta kesi inaisha kiholela.. Baadaebwanakuja kupiga kelele tuwe wazalendo tulipe kodi kwa manufaa ya taifa letu, kumbe ni kwa manufaa ya mtumbo ya wachache
 
tunaomba iwaunganishe Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango na aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha ( sasa yupo Wizara ya Viwanda ) Dotto James kwani hawa ndiyo wanawajibika zaidi Kimaamuzi na siyo hawa Wakaguzi ambao Kimsingi naona ni kama mnawaonea tu kwa Gharama za Kuwaogopa akina Mpango na Dotto.
👍🤝👏
 
Siku tutakapoamua kuachana na kuyachekea matukio kama haya, huo ndio utakaokuwa mwanzo wa nchi yetu kupiga hatua za uhakika na haraka kuelekea kwenye maendeleo halisi ya nchi yetu.

Najaribu tu kukumbuka mfano halisi hapa:

Baadhi ya raia wa China wanapokuja hapa kwa sababu zao mbalimbali, na wengine kwa matembezi ya muda mfupi tu, wanatumia mwanya huo kuona kama wanaweza kutengeneza hela nyingi kwa haraka haraka kwa kutumia mianya wanayoiona hapa kuwaruhusu kufanya hivyo.

Hawa watu wanapokuwa huko kwao hawathubutu kamwe kujihusisha kwenye mambo wanayotufanyia wakiwa hapa. Bila shaka wanao uelewa mzuri sana kinachoweza kuwatokea wakiyafanya hayo wakiwa huko kwao.

Nasi tunahitaji kuzijaribu hizo njia wanazotumia China kuondoa uozo wa aina hii hapa kwetu.

Nayasema haya kwa moyo safi kabisa bila ya kutishwa wala kutetereshwa na kelele nyingi zinazoambatana na kutekeleza adhma hiyo hapa kwetu.
Dah.... Mkuu umeandika kwa hisia Kali Sana.... Kamwe uongo unaoendelea haiwezi kuushinda ukweli uliosimama...
"Ukitaka kula lazima uliwe kidogo" - Julai Kilo [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji2960]
 
Kwa mahesabu ya haraka haraka kama zinakaribia ama ni bilioni 2 [emoji849]

Halafu utakuta kesi inaisha kiholela.. Baadaebwanakuja kupiga kelele tuwe wazalendo tulipe kodi kwa manufaa ya taifa letu, kumbe ni kwa manufaa ya mtumbo ya wachache
Ukimuona polisi wa Usalama Barabarani anahangaika juani na madereva lazima ujue kuna mabosi wanakula kivulini. Hivyo ndivyo utawala wa mwendazake ulivyokuwa. Na hii ni Wizara ya Fedha Hazina tu, huko kwingine ndio kulikuwa labda balaa zaidi. Sasa tusubiri ya TRA na BOT!
 
Back
Top Bottom