Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Watendaji Wizara ya Fedha wasimamishwa kazi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha

Sisi wenye mishahara ya laki sita tunatamani kufika huko kwenye mishahara ya kuanzia 1.5M pamoja na posho na marupurupu kibao tutulie tufanye kazi kama wendawazimu, KUMBE TUMBO LA BINADAMU HALITOSHIBA MPAKA SIKU LINAINGIA KUBURINI.


VIONGOZI WA JUU FANYENI KWANZA HAKI NA USAWA KWENYE MISHAHARA ILI NCHI IENDELEE UNYONYAJI KWENYE MISHAHARA NI MBAYA SANA.
 
Wasisaahau pia mbunge wa arusha mjini , wa kuchaguliwa na wananchi alikuwa na yeye kwenye mdundiko wa kugombea BWANA ....safaari hii wananchi wa arusha wamepatikaana na mcheza vigodoro ..wanaume wa arusha ..oyeee
 
Ukiwa nje ya mchezo utasema wafukuzwe kazi. Ila ukweli ni kwamba kila mtu anapiga anapo pata mwanya.Ajali kazini
 
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi Mkaguzi Mkuu, Mkaguzi Msaidizi na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Fedha. Amefanya hivyo ili kupisha Uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya Fedha za Umma.

Ametoa agizo kwa Mkurugenzi wa TAKUKURU, ACP Salum Hamdun kufanya uchunguzi. Tuhuma mojawapo inayokabili ni malipo ya Milioni 251 yaliyofanyika Machi 31, 2021 yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi na waliohusika.

======

Waziri mkuu wa Tanzania, Kassim Majaliwa amewasimamisha kazi mkaguzi mkuu, mkaguzi msaidizi na baadhi ya watendaji wa Wizara ya Fedha na Mipango kupisha uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha za umma zinazowakabili.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri mkuu iliyotolewa leo Mei 28, 2021 inaeleza kuwa katika kikao kazi na waziri wa fedha na mipango, katibu mkuu, manaibu katibu wakuu na watendaji waandamizi wa wizara hiyo mkoani Dodoma jana, Majaliwa amemuagiza mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na kupambana na Rushwa (Takukuru), Salum Hamdun kufanya uchunguzi kuhusu tuhuma hizo na ikithibitika si za kweli wahusika warejeshwe kazini.

Majaliwa amezitaja tuhuma hizo kuwa ni malipo yaliyofanyika Machi 31, 2021 kupitia vocha 30 ya Sh251 milioni yakielezwa kuwa ni malipo maalum bila kutaja kazi maalum ni nini na nani aliifanya.

Amebainisha kuwa siku hiyo hiyo pia zililipwa Sh198.8 milioni kwa madai kuwa ni posho ya honoraria.

Mtendaji mkuu huyo wa Serikali amesema Aprili 8, 2021 watumishi 27 wa wizara hiyo walilipwa Sh44.5 milioni za posho ya kazi maalum ya wiki nne na Aprili 13, 2021 zililipwa Sh155.2 milioni kwa watumishi 68 ikiwa ni posho ya kazi maalum ya wiki tatu.

Pia Aprili 30, 2021 zililipwa Sh43.9 milioni kwa ajili ya kuandaa mpango wa kuhifadhi mazingira na siku hiyohiyo zililipwa Sh14.4 milioni kwa ajili ya siku ya wanawake.

Inaeleza kuwa fedha nyingine Sh43 milioni zililipwa siku hiyo na kufanya jumla ya malipo yaliyolipwa siku hiyo kuwa Sh101.8.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa Meimosi, 2021 zililipwa Sh184.1 milioni na mchana wa siku hiyo zikalipwa Sh264 milioni zikiwa ni malipo ya kazi maalum.

"Sisi tulikuwa Mwanza tunasherehekea siku ya wafanyakazi duniani nyinyi hapa ndani mnalipana posho,” amesema Majaliwa.

Inabainisha kuwa Mei 3, 2021 zililipwa Sh146.5 milioni kwa watumishi 125 zikiwa ni malipo ya kuandaa mpango kazi wa manunuzi kazi ambayo ni sehemu ya majukumu yao ya kila siku na siku hiyohiyo zililipwa Sh171.2 milioni kwa ajili ya kuandaa nyaraka za Bunge.

Taarifa hiyo imemnukuu Majaliwa akisema Sh155 milioni zililipwa kwa baadhi ya watumishi zikiwa ni posho yakuandaa miongozo wakazi.

"Yaani hii kazi ya ukaguzi inalipwa kwenye maeneo manne, huu ni utaratibu wa wapi? Mnazidi kutupunguzia imani, na sijaongelea eneo la kuhamisha mafungu na utaratibu kuhamisha fedha kisha mnakwenda kuzichukua huko mlikozihamishia,” amesisitiza Majaliwa.

Amewataka watendaji wa wizara hiyo kujenga uaminifu kwa wanaokusanya mapato kwa kufanya kazi kwa uaminifu na kuwatahadharisha kuwa watakaoendekea kucheza na fedha za umma hatua kali zitachukuliwa dhidi yao huku akiwapongeza wafanyakazi wenye weledi.

Chanzo: Mwananchi
I FEEL SORRY FOR MWIGULU NCHEMBA , NA UJANJA WAKE WOTE HADI WAZIRI MKUU AJE AONE MADUDU KWENYE WIZARA YAKE ...INA MAANA YEYE ALIKUWA WAPI KUYAONA ....MAANA HAO WALIOTUMBULIWA ANAWAMUDU HASAAA..HAKUITAJI KUSUBIRI MAJALIWA AJE AMSAIDIE ..HUU NI UDHAIFU KWAKE .....NA ITA MCOST ..POLE YAKE ....NA NDIO ANATAKA AWE RAIS 2025/?
 
RAIS WA TANZANIA 2025 kweli watu wanaiba yuko ofisini..anaumbuliwa na waziri mkuu ..yeye alikuwa wapi kuyajua haya ......
Mwigulu apunguze siasa ..na kuzungukwa na madalali , afanye kazi , kwa mwendo huu watamtumbua ..
 
Posho ya kuandaa ripoti ya mwaka hahahaaa
Usicheke 🤣🤣🤣! Kuna mambo ya ajabu sana katika utumishi wa serikali. Ukiyachunguza kwa makini unaweza kudhani siyo watumishi bali ni wataalam washauri wa serikali.

Posho ndiyo lugha wanayoifahamu!
 
Jiwe alimpiga roba kali, kila kitu alikuwa anataka aonekane yeye, Waziri Mkuu alikuwa hana meno kabisa, alikuwa kila akitaka kugusa mahali anakutana na watu pendwa wa Jiwe, inabidi arudi nyuma. Now Mama kamwachia uwanja ajimwage atakavyo, wakati yeye anadili zaidi na mambo makubwa makubwa. Jiwe bwana, hadi madarasa na vyoo alikuwa anataka azindue yeye, alikuwa anafuatilia hadi nani kamtongoza nani kwenye ofisi mbalimbali, very stupid president
Kwaiyo wewe unatakaje?unataka Rais anayefatilia watendaji wake au huyu tuliyenaye anayeshinda kwenye kioo anajipodoa utafikiri anatafuta mchumba,hapa atuna Rais tuna picha ya Rais tu,juzi tu tuliona Waziri mkuu anafukua madudu hapo UDAT mpaka akasimamisha watendaji wake,akabaki Mkurugenzi ambaye waziri mkuu,akuwa na uweza naye wa kutengua, akasema anampereka kwa Rais maana yeye ndiye alikuwa na mamlaka naye, mpaka sasahivi hatuoni chochote,yule Mkurugenzi bado yupo pale pamoja na madudu yote yale.Hapa atuna Rais tuna rais wa kutafuta wawekaji tu.
 
Hawa viongozi wetu wanacheza tu na akili zetu! Haya ni maonesho tu yasiyokuwa na uhalisia! Mbona mengine hatuambiwi? Kwani ni wizara ya frdha tu wanalipana maposho makubwa? Ubadhirifu upo kila mahali lakini mnachagua sehemu ambayo mnajua mtawapumbaza wananchi! In fact hakuna litakaloendelea kwa sababu sheria navtsratibu zinawaruhusu kujilipa walivyojilipa! Acheni kutuchezea akili nyie!
 
Taifa linasimama kujadili pesa ambayo haItoshi kununua vx - r....

Zile b's nyingi zilizopotea ndio bac Tena?

Basi sawa
 
Kwaiyo wewe unatakaje?unataka Rais anayefatilia watendaji wake au huyu tuliyenaye anayeshinda kwenye kioo anajipodoa utafikiri anatafuta mchumba,hapa atuna Rais tuna picha ya Rais tu,juzi tu tuliona Waziri mkuu anafukua madudu hapo UDAT mpaka akasimamisha watendaji wake,akabaki Mkurugenzi ambaye waziri mkuu,akuwa na uweza naye wa kutengua, akasema anampereka kwa Rais maana yeye ndiye alikuwa na mamlaka naye, mpaka sasahivi hatuoni chochote,yule Mkurugenzi bado yupo pale pamoja na madudu yote yale.Hapa atuna Rais tuna rais wa kutafuta wawekaji tu.
Wewe inaonekana uliharibiwa kabisa na Mwendazake! Mwendazake alikuwa anafanya majukumu ya suboordinates wake kwa sababu ya ile hulka yake ya kutaka kionekana ba kusifiwa yeye tu. Mawaziri walikuwa hawana kazi! Mwendazake alikuwa abafanya kazi zaxwaziri mkuu.

Kufuatilia mambo madigomadogo ya kisekta sio kazi ya rais wa nchi! Hizo ni kazi za waziri mkuu na mawaziri wake. Unamkumbuka Lowasa akiwa waziri mkuu? Hivyo ndivyo waziri mkuu anapaswa kuwa! Waziri mkuu nfiye anapaswa azunguke huko na huko nchi nzima akihakikisha mipango ya serikali inatekelezwa! Sio kazi ya rais hiyo!

Mwendazake alivuruga kabisa mifumo na protokali za kiutawala! Ndiyo maana amewaharibu kabisa kwa mifano yake mibaya!
 
Sijaoa
1. ACP au CP....... Hamduni si alipandishwa na kuwa Kamishina wa Polisi

2. Kwahiyo uchunguzi huo ni tofauti na Rais Samia
Sijapata kuona wizi wa kishamba namna hii! Hata asiyekwenda shule, anajua kuwa jamaa walipiga! Nashauri! Wizara ya fedha ifanyiwe overhaulin
 
In other words amepiga mkiani badala ya kichwani
Hana mamlaka wa kupiga kichwani. Mwenye mamlaka hayo yuko DSM. Waziri Ummy huko Shinyanga leo naye kaishia kupiga mkiani.
 
Back
Top Bottom