Royal Tour
JF-Expert Member
- Oct 11, 2011
- 252
- 459
Siku za hivi karibuni hasa kuanzia serikali ya awamu ya tano mpaka sasa, wananchi wameacha kuamini mifumo rasmi ya utoaji haki badala yake wanaamini viongozi wa kisiasa mfano wakuu wa wilaya, mikoa, mawaziri na watendaji katika vyama vya siasa katika kudai haki hasa ile inayojikita katika migogoro ya ardhi.
Katika migogoro ya ardhi bunge letu ambalo ndio chombo cha kutunga sheria kimeweka utaratibu wa kushughulikia migogoro ya ardhi kuanzia baraza la kata,baraza la ardhi na nyumba la wilaya,mahakama kuu mpaka mahakama ya rufani.
Chakushangaza ukitembelea katika ofisi za wakuu wa wilaya na mikoa utakuta mashauri ya migogoro ya ardhi yanasubiri utatuzi na wao wanajua wazi hawana mamlaka ya kuamua migogoro hiyo zaidi ya kushauri tu,utakuta mwananchi ana miaka miwili yupo kwa DC au RC anatafuta haki. Kwanini viongozi msiwaambie ukweli wananchi na kuacha kuwapotezea muda na kupoteza haki zao?
DC na RC ninyi ni wateule wa mheshimiwa rais ambao muda wowote mnaweza kutenguliwa au kuhamishwa kituo kingine cha kazi,je ikitokea hivyo hao wananchi mnaowaaminisha kutatua na kumaliza migogoro ya ardhi ambayo ipo mezani kwenu zaidi ya mwaka mtawasidiaje?
Hii ni hatari kama taifa wananchi kutoamini mifumo rasmi ya utoaji haki katika eneo la ardhi na kuamini watu ambao hawana nguvu Kisheria na huku wakati mwengine wanaweza kufanya maamuzi ambayo badala ya kusuluhisha wakachochea zaidi migogoro hiyo ya ardhi.
Kinachoonekana wananchi wanapenda zaidi matamko kuliko kufuata taratibu za kudai haki ambazo zimewekewa mifumo rasmi,yaani anataka kwenda kwa DC au RC ili aambiwe "hii ardhi au nyumba ni mali yako na sitaki kuona mtu anamsumbua" kwakweli hii tabia inakiuka utawala sheria ambao sisi kama taifa tumekubaliana kuufuata.
Nilikutana na mwananchi wa wilaya ya Kigamboni maeneo ya Dege aliniambia maeneo yao yalichukuliwa na kampuni ya kuuza viwanja kwa makubaliano kuwalipa baada ya kupima na kukata viwanja,badala yake aliuza viwanja pasipo kuwalipa wahusika. Wakaamua kupeleka malalamiko yao kwa DC ambaye sasa amehamishwa ili awasaidie kupata haki zao.
DC akamkamata mwenye kampuni akapelekwa kituo cha polisi lakini akapata dhamana baada ya kukubali kuwalipa wananchi,mwishowe hakufanya hivyo na sasa ni mwaka wa nne hakuna lolote wananchi wanahangaika kupata haki zao.
Niliwashauri waende mahakamani bado wanawasiwasi kama watapata haki zao na wanahofia shauri kuchukua muda mrefu lakini wapo tayari kupoteza muda kwa hao viongozi wa kisiasa kuliko mahakamani.
Nilikutana na mwengine alikuwa mjane alikuwa na mgogoro wa mgawanyo wa nyumba za mirathi akapata taasisi zinazotoa msaada wa Kisheria ili zimsaidie bure,shauri likaenda mahakamani likachukua muda kidogo. Akanipigia simu eti nimpe namba ya katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM akaonane naye ili amsaidie apate haki yake.
Kwakweli sikumpa hiyo namba maana nilifahamu fika anakwenda kupoteza muda na haki yake hatoipata,nikamueleza andelee kudai haki yake mahakamani lakini hakukubali. Alitaka nguvu ya matamko kutoka kwa viongozi wa kisiasa.
Wakuu wa mikoa,wilaya na wateule wengine wa rais msiwapotezee muda wananchi kupata haki zao kwenye migogoro ya ardhi.

Upvote
1