Waue tu wanavyojisikia. Kina Mwashambwa wanashangilia kwa sababu wapinzani wao wanapungua, kwa kutekwa na kuuawa. Wanaouawa na kutekwa wanamuomba Mungu aingilie Kati. Huyo Mungu aliyeshindwa kuzuia mauaji ya kinyama Africa kusini kwa waafrica wasiyo na hatia hadi waliposhika silaha kupambana na mkaburu. Mungu aliyeshuhudia waganda wakikanyagwa na vifaru vya Malyamungu chini ya utawala Wa Amin, Mungu ambaye anaona watoto wadogo Wa kipalestina wakiuawa kila kukcha bila kufanya lolote. Hakika watakwisha. Watakuwa kila siku wakichomolewa kwenye mabasi na miili yao kutupwa porini huko alikokuwa akitupa wapinzani usiku yule DC wa Longido.
Bila kutafuta njia nyingine mtakwisha. Vinginevyo tangazeni kuachana siasa. Mtakwisha na kuacha familia zenu wapweke na kwenye mateso makubwa.
Ni vyombo vya serikali tu vinaweza kujiamini kumchomoa mtu kwenye Gari, kumtia pingu mbele za watu na kwenda kumuua porini. Kwa kuwa ni wao, hakutakuwa na upelelezi Wala wahusika hawatakamatwa kamwe.
RIP Mzee Kibao.
Hongereni kina Mwashambwa.