DOKEZO Watoto chini ya miaka mitano na Wajawazito wamekuwa wakitozwa pesa katika Kituo cha Afya Mundindi

DOKEZO Watoto chini ya miaka mitano na Wajawazito wamekuwa wakitozwa pesa katika Kituo cha Afya Mundindi

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Naomba kuwasilisha malalamiko kuhusu changamoto zinazowakabili wananchi wanapopata huduma za afya katika Kituo cha Afya Mundindi.

Kuna madai kwamba watoto walio chini ya umri wa miaka mitano na wanawake wajawazito wamekuwa wakitozwa fedha za matibabu, licha ya utaratibu wa Serikali kutoa huduma hizo bila malipo kwa makundi hayo. Tunapojaribu kuhoji suala hili kwa uongozi wa kituo, hasa Mganga Mkuu wa kituo, tunadai kuwa tumekuwa tukijibiwa kwa ukali na lugha isiyofaa, huku akidai kuwa huduma hizo bure ni kauli za kisiasa tu.

Hali hii imekuwa kero kubwa kwa wananchi kiasi kwamba baadhi yetu tumelazimika kusafiri zaidi ya kilomita 35 kwenda Hospitali ya Lugarawa kutafuta huduma za afya.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kutoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa sera za Wizara ya Afya, hasa kuhusu huduma za bure kwa watoto walio chini ya miaka mitano na wajawazito, ili wananchi wapate huduma stahiki bila vikwazo.
 
Mnakazana kutiana mimba mnataka matibabu bure? Mimba sio emergency unapotia Mwanamke mimba ujiandae kuilea usipende vya bure mwanaume pambana.
 
Yani bao lako, starehe zako ! Alafu unalalamika serikali ikulipie?

Sikia, nchi hii hakuna huduma ya bure ! Japo huko majukwani wanasiasa watakuambia ni bure !
Lazima ulipie kidogo, tofauti na private hospital!

Punguza kulombana hovyo kama huna uhakika wa kipato na malezi
 
Mnakazana kutiana mimba mnataka matibabu bure? Mimba sio emergency unapotia Mwanamke mimba ujiandae kuilea usipende vya bure mwanaume pambana.
Nani kwa kwa mbia ni vya bure?kwa nini serikali hii haramu inatukata kodi kila sehemu ya pale tunapojipatia kipato chetu.Nchi zilizoendelea hizo huduma huwa ni bure
 
Jielezee vizuri sijui kama viongozi wa awamu ya sita hata wanapajua Mundindi..ni wapi?taja kata,tarafa,kijiji,wilaya na mkoa.
 
Wananchi wanaotumia huduma katika Kituo cha Afya Mundindi tunakabiliwa na changamoto kubwa, watoto walio chini ya umri wa miaka mitano pamoja na wajawazito wanatozwa fedha za matibabu licha ya kuwepo kwa utaratibu wa huduma za bure kwa makundi hayo.

Tunapojaribu kuhoji suala hilo kwa Mganga Mkuu wa kituo, hukutana na majibu makali na lugha isiyoridhisha. Tumeambiwa huduma za bure kwa watoto chini ya miaka mitano ni "mbwembwe za wanasiasa."

Hali hiyo imekuwa kero kubwa kwa wananchi, ambapo baadhi yao wamelazimika kusafiri zaidi ya kilomita 35 kwenda Hospitali ya Lugarawa kutafuta huduma za afya.

Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili na kutoa ufafanuzi kuhusu kama utaratibu wa sera ya Wizara ya Afya kuhusu huduma za bure kwa watoto chini ya miaka mitano na wajawazito umebadilika.

Tunaomba msaada kwa sababu wananchi tunapata mateso makubwa katika kupata huduma za afya.
 
Back
Top Bottom