Serikali iko sahihi, wewe ndiye huielewi kabisa dhana ya ushirikishwaji. Hata uchukue maprofesa kutoka Havard University ni lazima wakusanye maoni ya wananchi ili baadae wayachambue na kutaweka kitaalamu. Kama serikali ingetaka kufanya kama usemavyo basi hata kusingekuwa na sababu ya kuwa na uwakilishi au kuchukua maoni kwenye miswaada na tume mbalimbali. Mawazo kama yako ndiyo hupelekea miswaada wakati mwingine kuwekewa muda mfupi sana wa kupokea maoni ya wananchi, kwa sababu inawezekana hata bungeni wameshawajua kwamba hamna time na mambo hayo, kiasi kwamba hata mngepewa Mwezi mzima hakuna mwenye time, watu wako bize na mipira, betting, Diamondi vs Kiba etc. Matokeo yake sheria ikipita na pengine kodi imepandishwa ndiyo watu wanashtuka na kulalamika. Tabia hii ya jamii kukwepa uwajibikaji kwenye masuala muhimu ya maendeleo ya nchi, na kuamini kwamba ni kazi ya serikali na wao haiwahusu ndiyo chanzo kikubwa cha kukosa maendeleo,hasa pale tunapokuwa na viongozi wasiokuwa wawajibikaji.