Watoto huwa wanacheza michezo hatari sana!

Watoto huwa wanacheza michezo hatari sana!

Kuna Mchezo nakumbuka tulikua tunachukua Kuti tunatoa zile Chelewa alafu ule Mti wake unaseleleka nao katika Kilima huku umepanda, hicho kilima chenyewe kina Vipande vya Miti imechongoka kama yote.... unarudi Nyumbani Nguo yote katika Mattercall imechanika, nikikumbuka vile vipande vya Miti vilivyochongoka kwakweli Mungu hawa Watoto anawasimamia sana
 
Hahaha, utoto bhana. Yani sisi tulikuwa tunachezea baiskeli katika mteremko mkaliii na wakati wa mvua, tukipokezana. Ukianguka unaona poa tu unainuka mwingine anafuata, kumbe tulikuwa tunatafuta kifo.. hahaha

Naungana na mdau anesema MUNGU tu ndiye alikuwa akitulinda.
 
Back
Top Bottom