Mwamuzi wa Tanzania
JF-Expert Member
- Apr 7, 2020
- 15,486
- 45,256
Habari!
Nimefuatilia habari za mikoa mbalimbali na wilaya zake, watoto wengi ambao wamepangiwa shule za sekondari kuanza kidato cha kwanza hawajaripoti shule mpaka leo. Yawezekana wapo wazazi ambao wanajichanga ili wawapeleke watoto wao shule na pia wazazi wengine hawana mpango wowote.
Yote kwa yote serikali ndio sababu kuu isikwepe wajibu wake.
Sababu hizi ndizo zilizopelekea mpaka sasa watoto wengi ambao wamepangiwa shule za sekondari kutokuripoti shule:
1. Umaskini
Pamoja na serikali kujinasibu kugawa elimu bure lakini kwa mwanafunzi wa kidato cha kwanza anapaswa kuandaliwa angalau kwa sh. Laki mbili za mahitaji yake muhimu ya shule. Serikali ya CCM ione aibu kwakuwa miaka zaidi ya 60 ya uhuru imetengeneza wamaskini wengi sana. Kuna Mtanzania laki mbili ya pamoja hawezi kuipata mpaka auze shamba lake ambalo linampa msosi.
2. Ukosefu wa ajira
Mzazi aliyeuza mali zake kumsomesha mwanae akidhani ataajiriwa ili aikomboe familia yake leo hii kijana kamaliza degree na hana ajira na kulima hataki kageuka mdhululaji mjini, hana faida kwa wazazi. Sasa mzazi kujitoa kafara kwa mtoto mwingine hawezi.
3. Udhaifu wa elimu ya Kitanzanja
Waliosoma kama hawajaajiriwa hawana utofauti na wasiosoma ndani ya jamii zao. Wazazi hawana msukumo wa kuwasomesha watoto wao.