Watoto ni chanzo kizuri sana cha taarifa. Unapokuwa kazini wao wanazurura mitaani

Watoto ni chanzo kizuri sana cha taarifa. Unapokuwa kazini wao wanazurura mitaani

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Joined
Feb 18, 2012
Posts
15,892
Reaction score
16,476
Good afternoon jamiiforums

Hivi unafahamu ya kwamba watoto wadogo hao unaowaona kama bado hawaijui dunia vema wanaweza kuwa wanajua mambo mengi sana yanayoendelea mitaani kuliko watu wazima?

Wakati wewe upo kazini, watoto hawa wanazurura mitaani hivyo wanakutana na mambo mengi sana. Ukiwa unapiga story na dogo yoyote yule usipende kumkatishakatisha mkuu, utakosa uhondo. Wanawake wa Dar wanakwambia utakosa ubuyu. Upo nyonyo?

Wakati wewe unaenda kunywa beer kwa yule demu wako pale bar iliyopo umbali wa KM 6 kwa kutumia gari yako aina ya Harrier, yeye mtoto akiwa na wenzie anaweza kuzurura umbali hata wa 12 KM kwa miguu na kukutana na watu pamoja na mambo mengine mengi tu ambayo wewe unayeondoka nyumbani saa 12 alfajiri kwenda kazini kwako huko Kariakoo/Posta na kurudi saa 5 usiku usiyajue.

Zamani wakati nipo mdogo, tulikuwa tunaendesha vidubwana fulani hivi tulikuwa tunaviita ringi. Ringi zikiwa zimefungwa na kamba pamoja na matairi mabovu ya magari watoto wengi wa 1980s wameendesha.

Nilikuwa ninakaa eneo moja linaitwa Keko lipo huku Dar. Mimi na watoto wenzangu tulikuwa na uwezo wa kuendesha zile ringi kuanzia hapo eneo la Keko mpaka uwanja wa taifa (Sasa hivi wanaita uwanja wa Uhuru) kisha tukaenda mpaka Tandika Sokoni tukiwa tumevaa kandambili tu na bukta huku juu tukiwa tumetupia tshirts.

Tulikuwa tunazurua na kukutana na mambo mengi sana sema kutokana na akili za kitoto za wakati ule tunachukulia ni kawaida sana. Tulikuwa tunaweza kukutana na baba pamoja na mama fulani ambao ni majirani zetu wanaongozana pamoja huko Temeke, wanatununulia pipi au koni kisha wanatugombeza "Yaaani nyie watoto mnakuja mpaka huku" na kutuamuru turudi nyumbani haraka laa sivyo watatusemelea kwa mama zetu.

Tulikuwa tunachukulia kawaida lakini baada ya akili kuja kupevuka miaka kadhaa mbele ndio unakuja kugundua kumbe wale baba na mama fulani walikuwa ni mtu na mke wa mwingine ambao walikuwa ni wapenzi/wanachepuka.

Mtoto anaweza akawafahamu majirani ambao hata wewe baba mtu hauwajui na ndio maana siku zote ukiwa uaenda kumtembelea rafiki yako na ukapoteza ramani, wewe waulize tu watoto eti mnapajua kwa baba fulani, yaaani chaaap tu wanakupeleka.

Watoto wanatambuana haraka lakini ukienda kumuuliza mtu mzima mwenzie inawezekana hawamjui huyo baba Mariam kwa maana wote wanaondoka alfajiri kwenda kazini na kurudi usiku sana lakini waototo wao muda wote wapo wanazurua huku na kule.

Ninaomba kumalizia kwa kusema, linapokuja suala la ukusanyaji wa taarifa kwa ulinzi wa familia/mtaa wako kamwe usidharau wanachokisema watoto wadogo. Wasikilize kwa umakini sana kwa maana wanaweza kukupa clues za maana na ukabaki mdomo wazi (Jaw Widening Clues)

USISAHAU: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.
 
Kuna mtoto wa kama miaka minne hivi nilimuuliza unasoma darasa la ngapi? Akanijibu yupo darasa la tano.Huyu nae anaweza kutupatia taarifa sahihi?Na anazurura kweli....
Anaweze kukupa taarifa sahihi kulingana na umri wake ndio maana kuna watu wazima wa hovyo pia na watoto waerevu
 
Dunia ya leo imebadilika, hakuna mzazi anawaachia watoto kuzurura hovyo, watoto wengi wanacheza ndani ya mageti yao, ukatili dhidi ya watoto na wizi wa watoto unatisha especially maeneo ya mjini
 
Watoto wanazurura sana pasipo kujali wanaenda umbali gani. That's my point.
Kwa hiyo wazazi wanakosa kufanya wajibu wap ipasavyo, nyakati hizi sio salama kuwaacha watoto wazurure, kuna wakati nilienda kusalimia rafiki maeneo ya Mbezi beach, nilipofika maeneo ya mtaani kwake nikakuta watu wamejaa wengi, kuuliza kulikoni wakasema kuna mtoto wa kiume ameokotwa pembeni ya fensi akiwa hajitambui na anaonekana ameingiliwa kinyume, nikapenya kuangalia, yule mtoto ni kama wa miaka sita au saba, baada ya watu kuusambaza taarifa ikajukikana huyo mtoto anatoka mtaa wa tatu na huwa anazurura kila kona, polisi walikuja, sikujua kilichoendela lakini ni tukio ambalo lilimsikitisha kila mtu

Wazazi lazima kuwalinda watoto, hakuna usalama huko nje
 
Usalama wa watoto ni jukumu la kila mtanzania hapo mtaani unapokaa ila linaanza na mzazi mwenyewe.

Uswahilini ni sehemu hatari sana kwa malezi ya mtoto. Nimekaa uswahilini miaka 25 hivyo ninapajua vema.

Rafiki zangu niliosoma nao shule ya msingi wengi wao wanatumia sana mihadarati.
 
Hao watanzania wenye jukumu la kuwalinda watoto ndio wanaowafanyia ukatili, sio ndugu wala jirani anaeaminika kwa nyakati hizi, na hili sio tatizo la uswahilini tu, ni tatizo la kila sehemu mpaka vijijini

Mzazi ukishindea kumlinda mtoto wako usitegemee walimwengu wamlinde
 
Back
Top Bottom