King Jody
JF-Expert Member
- Oct 8, 2022
- 1,834
- 3,456
Siyo wote ila kuna baadhi ya wazazi\walezi wanaishi vizuri na watoto ambao siyo wao kiasi kwamba usipoambiwa siyo wazazi wao huwezi kamwe kujua.
Nimewahi kushuhudia kisa cha mtoto wa yatima katika familia fulani, yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili hivyo ikabidi achukuliwe na ndugu wa marehemu, baada ya muda mfupi dogo akaanza kunyanyasika,
Nakumbuka siku hiyo ametoka shule na wenzie lakini cha ajabu akapokelewa na kipigo kizito hadi damu ikawa inamtoka puani, wakati huo akaambiwa asafishe vyombo wakati watoto wengina wa nyumba ila walikuwa ndani wanakula, inasikitisha sana.
Kwa wale wanaoishi vizuri na watoto ambao syo wao Mungu awabariki sana, na wengine wanaowanyanyasa watoto yatima au watoto wa kambo hakika nawaambieni, Mungu anawaona, badilikeni.
Kwa wale waliolelewa na Mama\Baba wa kambo watakuwa wamenielewa.
Nb. Eeeh Mwenyezi Mungu nakuomba uwafanyie wepesi watoto wote wanaopitia vipindi vigumu maishani. Amen