Watoto wa kambo na mayatima huwa wanapitia maisha magumu sana

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Siyo wote ila kuna baadhi ya wazazi\walezi wanaishi vizuri na watoto ambao siyo wao kiasi kwamba usipoambiwa siyo wazazi wao huwezi kamwe kujua.

Nimewahi kushuhudia kisa cha mtoto wa yatima katika familia fulani, yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili hivyo ikabidi achukuliwe na ndugu wa marehemu, baada ya muda mfupi dogo akaanza kunyanyasika,

Nakumbuka siku hiyo ametoka shule na wenzie lakini cha ajabu akapokelewa na kipigo kizito hadi damu ikawa inamtoka puani, wakati huo akaambiwa asafishe vyombo wakati watoto wengina wa nyumba ila walikuwa ndani wanakula, inasikitisha sana.

Kwa wale wanaoishi vizuri na watoto ambao syo wao Mungu awabariki sana, na wengine wanaowanyanyasa watoto yatima au watoto wa kambo hakika nawaambieni, Mungu anawaona, badilikeni.

Kwa wale waliolelewa na Mama\Baba wa kambo watakuwa wamenielewa.

Nb. Eeeh Mwenyezi Mungu nakuomba uwafanyie wepesi watoto wote wanaopitia vipindi vigumu maishani. Amen
 
kuishi na mtoto wa kambo nayo ni changamoto sana. mfano una watoto wako wanne ,wa kambo akawa wa tano
ukitaka kumtuma mmojawapo dukani ,hakikisha unatuma miongoni mwa wale wa kwako wanne, ukimtuma yule wa kambo ,atalalamika kuwa yeye tu ndo anatumwa
hivyo inahitajika akili kuishi nao pia
inabidi uwape upendeleo fulani hivi ili mambo yaende sawa
 
Mtoto wa mwenzio muone kama mtoto wako
 
images.jpeg
 
Binadamu ni tofauti sana , roho mbaya sijui inatokea wapi ?

Unamtesa mtu dunia ya kupita tu hii . kama mwanaume ogopa sana kuoa mwanamke mwenye roho mbaya wanaanza kukataa ndugu taratibu mpaka mtoto wa kambo au yatima.
 
Siyo wote ila kuna baadhi ya wazazi\walezi wanaishi vizuri na watoto ambao siyo wao kiasi kwamba usipoambiwa siyo wazazi wao huwezi kamwe kujua.

Nimewahi kushuhudia kisa cha mtoto wa yatima katika familia fulani, yeye alifiwa na wazazi wake wote wawili hivyo ikabidi achukuliwe na ndugu wa marehemu, baada ya muda mfupi dogo akaanza kunyanyasika,

Nakumbuka siku hiyo ametoka shule na wenzie lakini cha ajabu akapokelewa na kipigo kizito hadi damu ikawa inamtoka puani, wakati huo akaambiwa asafishe vyombo wakati watoto wengina wa nyumba ila walikuwa ndani wanakula, inasikitisha sana.

Kwa wale wanaoishi vizuri na watoto ambao syo wao Mungu awabariki sana, na wengine wanaowanyanyasa watoto yatima au watoto wa kambo hakika nawaambieni, Mungu anawaona, badilikeni.

Kwa wale waliolelewa na Mama\Baba wa kambo watakuwa wamenielewa.

Nb. Eeeh Mwenyezi Mungu nakuomba uwafanyie wepesi watoto wote wanaopitia vipindi vigumu maishani. Amen
sijawahi kuelewa roho mbaya ya kiasi hicho mtu anaitoa wapi tena unakuta ni mtoto wa marehemu ndugu yake.
 
haya mambo haya, mengine hata hayazungumziki, inabidi kubaki nayo kifuani tu, ila kwel kuna baadii ya waume na wake wana roho za ajabu sana.
 
Back
Top Bottom