Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Wale ambao hawajui kucheza...hawana ufundi...udambwi dambwi...walikua wanakaa beki....mafundi ndo ma strikers ....na mpira hauna formation... So kunakuwa na mabeki na washambuliaji...na ukubwa wa timu inategemea na wachezaji waliojitokeza
 
Jamaniii
 
Hakujawahi kuwa na starehe duniani kama mchezo huu wa mpira wa makaratasi/sembo/chandimu kwa vijana wa kiume waliokulia kiumeni, mimi katika kumbukumbu zangu nilikuwa na mashuti sana, nilikuwa nikiitwa "Kimti" enzi zangu, na kikubwa nilichokuwa najivunia ilikuwa ni mbio na uwezo wa "kunyoosha" na kwa uwezo huo niliwasaidia sana wenzangu kupata makombe ya kuku! Kuna siku nilikodiwa mahali kwenye mashindano ya kombe la kuku nikawa mamluki kiaina, basi kama dakika 5 tu baada ya kipyenga kupulizwa kuanzisha mtanange nikanyoosha shuti likagonga mwamba wa goli (goli la mti) ukaanguka lakini goli likaingia, ilileta utata mpaka mechi ikavunjika, refa akapigwa na mimi nilikimbizwa na wachezaji wa timu pinzani na mashabiki wao mpaka nyumbani, Mungu alinisaidia hawakunikamata! Kiukweli mchezo wa mpira wa miguu wa utotoni kwa mpira wa makaratasi ilikuwa ni starehe ambayo ninaijutia kuikosa siku zote katika maisha yangu!

Vipaji katika hatua hii ya ukuaji huchukuliwa kama uhuni na wazazi/walezi wengi huvipuuzia na kuvipiga vita.
 
Hiii naijuaa
 
Nae alikuwa zezetaa
 
Wale ambao hawajui kucheza...hawana ufundi...udambwi dambwi...walikua wanakaa beki....mafundi ndo ma strikers ....na mpira hauna formation... So kunakuwa na mabeki na washambuliaji...na ukubwa wa timu inategemea na wachezaji waliojitokeza
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Umenichekesha mpaka nimeliaaa,sipati picha mlivyomlaumu
 
Timu pinzani ikitaka kurudisha goli na kiza kiza kishaanza kuingia nang'oa goli moja halafu nduki lake sio la nchi hii
 
Kufaulu elimu ya msingi ilikua kama miujiza, kwanza hata haujui tofauti ya kufaulu na kufeli. Unachojua ni kumaliza darasa la saba tu. Kwanini msifurahie michezo hasa hasa soka?
Hakika kabisa mi nilikuwaga hata sijisomeiii yaan ni michezo tu ,mara rede,dama, Ukimwi, yaan ilikuwa balaa
 
Kuwa na ukurutu ilikuwa kawaida sana, tena kuoga ikikuwa mara moja moja.

Wakati wa kwenda shule ilikuwa ni mwendo wa kunawa kichwa, mikono na miguu tu.

Mtoto kuwa na machacha kwenye visigino vya miguu lilikuwa jambo la kawaida sana.
Halaf hapo unaenda zako peku mpaka shule basi mi nilikuaga navua viatu nami nitembee peku yaan naona wale wanaotembea peku wanafaidi kumbe wale wanatembea peku hawana viatu [emoji23][emoji23][emoji23] sio kwamba wamependa
 
Wale ambao hawajui kucheza...hawana ufundi...udambwi dambwi...walikua wanakaa beki....mafundi ndo ma strikers ....na mpira hauna formation... So kunakuwa na mabeki na washambuliaji...na ukubwa wa timu inategemea na wachezaji waliojitokeza
Kwa hiyo hapo mnaweza cheza 18 kwa 18 si ndio
 
Aisee, hayo maumivu sijui yalikuwaje mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…