Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Watoto wa kishua hamuwezi kuielewa hii picha

Wale ambao hawajui kucheza...hawana ufundi...udambwi dambwi...walikua wanakaa beki....mafundi ndo ma strikers ....na mpira hauna formation... So kunakuwa na mabeki na washambuliaji...na ukubwa wa timu inategemea na wachezaji waliojitokeza
 
nakumbuka kiwanja chetu cha mtaa kilichukuliwa na wakubwa kwa mda baada ya uwanja wao mkubwa kuchukuliwa kufanyiwa mikutano ya kidini pande za kawe home,, sasa wakawa wanatunyanyasa kila ikifika saa kumi tu, wanakuja kutufukuza wacheze wao.. tukaunda tume ya kuwaondoa hawa ma bro,, tukakubaliana twende beach tukachukue mbigili za kutosha tukazimwage uwanja mzima mpaka magolini.. tukaenda tukajaza mifuko na mifuko, tukazimwaga usiku zote,,, kimbembe kesho yake, wakubwa wanakuja kucheza hawajatukuta wakaona mtelezo,, sie tumekaa tunawaangali tu,, maana wengine walikua na viatu wengine hawana,, wengine walioanguka wanakutana nazo,, mpira haukuchezeka siku hiyo, wakaanz kutusaka tukazoe miba tuliyoimwaga uwanja mzima. hakuna aliyekubali kama kamwaga mbigili.. na wao ndo ikawa mwisho wao kucheza pale wakahamia uwanja mwengine,, vijana tukarudi tukaanza kuzitoa mojamoja japo hatukuzimaliza,, ila shuhuli nasi ilitupata ya kuchomwa nazo maana hatukuzimaliza,, zilikuja kuisha kwa kutuchoma, unaiokota unaenda kuitupa..
Jamaniii
 
Hakujawahi kuwa na starehe duniani kama mchezo huu wa mpira wa makaratasi/sembo/chandimu kwa vijana wa kiume waliokulia kiumeni, mimi katika kumbukumbu zangu nilikuwa na mashuti sana, nilikuwa nikiitwa "Kimti" enzi zangu, na kikubwa nilichokuwa najivunia ilikuwa ni mbio na uwezo wa "kunyoosha" na kwa uwezo huo niliwasaidia sana wenzangu kupata makombe ya kuku! Kuna siku nilikodiwa mahali kwenye mashindano ya kombe la kuku nikawa mamluki kiaina, basi kama dakika 5 tu baada ya kipyenga kupulizwa kuanzisha mtanange nikanyoosha shuti likagonga mwamba wa goli (goli la mti) ukaanguka lakini goli likaingia, ilileta utata mpaka mechi ikavunjika, refa akapigwa na mimi nilikimbizwa na wachezaji wa timu pinzani na mashabiki wao mpaka nyumbani, Mungu alinisaidia hawakunikamata! Kiukweli mchezo wa mpira wa miguu wa utotoni kwa mpira wa makaratasi ilikuwa ni starehe ambayo ninaijutia kuikosa siku zote katika maisha yangu!

Vipaji katika hatua hii ya ukuaji huchukuliwa kama uhuni na wazazi/walezi wengi huvipuuzia na kuvipiga vita.
 
Kuna tabia tulikuwa tunagombaniswa hasa na majamaa ambao ni wakubwa kuliko sisi.

Tunagombanishwa watoto tunaolingana umri au kukaribiana.

Mmoja anaambiwa mtukane fulani, halafu huyo uliyemtukana anachochewa na kuambiwa eti unatukanwa na fulani, unamuogopa nini kwa anaweza kukufanya nini, mpige.

Hapo mnajazwa upepo halafu mnaanza kuzipiga ngumi mwishiwe mnatika manundu kwa kuumizana halafu mkitaka kulia mnasifiwa hadi majikuta hamlii japo mnaumia kwa maumivu[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Hiii naijuaa
 
Hiki cheo nilikitumia kwa uaminfu mkuu..kuna siku nimeingia sculi j3 kaptula imejaa mafuta ya maandazi weekend ckufua....nikamwita RAIA mmoja nkamwambia anipe ya kwake alaf namfuta jina LA wasumbufu. Axee mstarini kwenye ukaguzi alichapwa za kutosha mwili mzima mtaalamu nimetulia tuu
Nae alikuwa zezetaa
 
Wale ambao hawajui kucheza...hawana ufundi...udambwi dambwi...walikua wanakaa beki....mafundi ndo ma strikers ....na mpira hauna formation... So kunakuwa na mabeki na washambuliaji...na ukubwa wa timu inategemea na wachezaji waliojitokeza
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
noma sana enzi izo nakumbuka tulikua tunachezea sana mpira wa karatasi (nyanka) kuna dogo mmoja wa kishua akaja na mpira wa gozi mzee ...tukatamania kichiz sema dogo anabania ...bei ulikua unauzwa 1300 tukasema kama vipi tujichange tulichanga kama wiki mbili ivi ikatosha hel ya kununulia gozi na bahat nzuri skuio ilikua ni jumapili kwenye gulio huwa wanapunguza bei ...

basi mzee tukanunua mpira ule tukamkabidhi daudi msenjelwa kwakua tulienda jioni zaid (mana jion zaidi ndo bei inapungua zaidi)
ikabidi mpira tumuachie daudi tutacheza kesho tukirudi shule

jumatatu shule kamakawa darasani muda auendi tunawaza kurudi tukachezee (tukapute) gozi

mda wa kurudi umefika ile kufika kwa kina daudi tunaona anatia huruma tu kumbe shule hajaenda ameshinda anachezea gozi tu mpaka akalipasua kwenye msumali wa paa la nyumba

tulimmaindi kichizi yan mpira umeharibika hatujaugusa hata kidogo hadi leo nikimkumbusha huwa tunaishia kucheka tu
Umenichekesha mpaka nimeliaaa,sipati picha mlivyomlaumu
 
Timu pinzani ikitaka kurudisha goli na kiza kiza kishaanza kuingia nang'oa goli moja halafu nduki lake sio la nchi hii
 
Kufaulu elimu ya msingi ilikua kama miujiza, kwanza hata haujui tofauti ya kufaulu na kufeli. Unachojua ni kumaliza darasa la saba tu. Kwanini msifurahie michezo hasa hasa soka?
Hakika kabisa mi nilikuwaga hata sijisomeiii yaan ni michezo tu ,mara rede,dama, Ukimwi, yaan ilikuwa balaa
 
Kuwa na ukurutu ilikuwa kawaida sana, tena kuoga ikikuwa mara moja moja.

Wakati wa kwenda shule ilikuwa ni mwendo wa kunawa kichwa, mikono na miguu tu.

Mtoto kuwa na machacha kwenye visigino vya miguu lilikuwa jambo la kawaida sana.
Halaf hapo unaenda zako peku mpaka shule basi mi nilikuaga navua viatu nami nitembee peku yaan naona wale wanaotembea peku wanafaidi kumbe wale wanatembea peku hawana viatu [emoji23][emoji23][emoji23] sio kwamba wamependa
 
Wale ambao hawajui kucheza...hawana ufundi...udambwi dambwi...walikua wanakaa beki....mafundi ndo ma strikers ....na mpira hauna formation... So kunakuwa na mabeki na washambuliaji...na ukubwa wa timu inategemea na wachezaji waliojitokeza
Kwa hiyo hapo mnaweza cheza 18 kwa 18 si ndio
 
noma sana enzi izo nakumbuka tulikua tunachezea sana mpira wa karatasi (nyanka) kuna dogo mmoja wa kishua akaja na mpira wa gozi mzee ...tukatamania kichiz sema dogo anabania ...bei ulikua unauzwa 1300 tukasema kama vipi tujichange tulichanga kama wiki mbili ivi ikatosha hel ya kununulia gozi na bahat nzuri skuio ilikua ni jumapili kwenye gulio huwa wanapunguza bei ...

basi mzee tukanunua mpira ule tukamkabidhi daudi msenjelwa kwakua tulienda jioni zaid (mana jion zaidi ndo bei inapungua zaidi)
ikabidi mpira tumuachie daudi tutacheza kesho tukirudi shule

jumatatu shule kamakawa darasani muda auendi tunawaza kurudi tukachezee (tukapute) gozi

mda wa kurudi umefika ile kufika kwa kina daudi tunaona anatia huruma tu kumbe shule hajaenda ameshinda anachezea gozi tu mpaka akalipasua kwenye msumali wa paa la nyumba

tulimmaindi kichizi yan mpira umeharibika hatujaugusa hata kidogo hadi leo nikimkumbusha huwa tunaishia kucheka tu
Aisee, hayo maumivu sijui yalikuwaje mkuu
 
Back
Top Bottom