Watoto wa marehemu Mzee Augustino Ilomo wamuomba RC Iringa kuingilia mgogoro wa mirathi

Watoto wa marehemu Mzee Augustino Ilomo wamuomba RC Iringa kuingilia mgogoro wa mirathi

DogoWaNjombe

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
3,284
Reaction score
7,708
0936e4fc-4977-44bd-b180-a5053505c1a0-780x470.jpg
Sarah Agustino Ilomo, mmoja wa watoto wa aliyekuwa mfanyabiashara maarufu wa Iringa, marehemu Mzee Augustino Ilomo, amemuomba Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Kheri James, kuingilia kati mgogoro wa mirathi unaotishia kupoteza mali zote zilizoachwa na baba yao.

Sarah anadai kuwa, licha ya juhudi mbalimbali zikiwemo za kisheria, mchakato wa kugawa urithi umegeuka chanzo cha maumivu baada ya baadhi ya mali kuuuzwa kwa njia anazodai kuwa za udanganyifu, bila ridhaa ya watoto wote wa marehemu.

Amesema Mzee Ilomo, aliyefariki dunia mwaka 2016, alikuwa mfanyabiashara mkubwa wa usafirishaji wa abiria na huduma za hoteli kupitia kampuni yake ya Living Light.

Aliacha watoto 12 na mali zikiwemo nyumba saba—moja jijini Dar es Salaam na sita mjini Iringa—viwanja viwili (Igumbilo na Kilolo), magari matatu (Land Rover Discovery, Toyota Pickup na Canter) na zaidi ya Sh milioni 160 benki.

Awali, amesema familia ilimteua mdogo wa marehemu, Michael Ilomo, kuwa msimamizi wa mirathi, hata hivyo, miezi sita baadaye mama wa kambo (jina limehifadhiwa) alitengua uteuzi huo bila maridhiano.
Kwa mujibu wa Sarah, kabla taratibu za mirathi hazijakamilika, baadhi ya watoto wakiungana na mama wa kambo wameshauza nyumba tano, magari yote matatu na viwanja viwili bila kushirikisha wengine.

Kinachotia hofu zaidi, anasema, kuna mpango wa kuuza nyumba mbili pekee zilizobaki, ikiwemo jengo la ghorofa nne lililokuwa hoteli ya Living Light na kwa sasa linatumika kama hosteli za wanafunzi wa kike wa Chuo Kikuu cha Ruaha, pamoja na nyumba nyingine iliyo katika mtaa wa kibiashara wa Uhindini mjini Iringa.

Sarah anadai nyumba hizo zinataka kuuzwa ili kulipa deni la zaidi ya Sh milioni 460, linalotokana na mkopo wa Sh milioni 250 uliodaiwa kuchukuliwa na mama wa kambo kwa sababu zisizojulikana, deni ambalo limeongezeka maradufu.

“Nyumba tano zimekwishauzwa na sasa wanachotaka ni kuuza hizi mbili zilizobaki ili kulipa deni hilo. Tutakimbilia wapi watoto wa marehemu kama nyumba hizo pia zikiuzwa?” alihoji Sarah kwa uchungu.
Anadai mauzo hayo yamefanyika kwa kutumia nyaraka za kughushi, zikiwemo za wosia, kampuni na hati za umiliki.

Anaeleza kuwa wosia wa baba yao, ambao awali ilidaiwa umehifadhiwa kanisani, haukuwasilishwa kwa familia kwa muda mrefu, na baadaye wakabaini nyaraka zimeghushiwa ili kuonyesha ni watoto wachache pekee wananufaika.

Sarah pia ameeleza kuwa fedha zilizokuwa benki zimepotea bila maelezo, na juhudi za kufuatilia hazijafanikiwa.

“Tunazo taarifa za wazi za nyaraka feki na mauzo kabla mirathi haijakamilika, lakini hakuna hatua zinazochukuliwa. Mali za marehemu zinaendelea kuuzwa pamoja na kulifanyia kazi suala hilo kwenye mamlaka mbalimbali,” amedai.

Kwa niaba ya baadhi ya watoto wa Mzee Ilomo, Sarah amemuomba Rais Dk Samia Suluhu Hassan, kupitia Mkuu wa Mkoa wa Iringa, kuingilia kati ili kulinda haki za watoto wa marehemu.

Lakini pia amewaomba wadau wengine watetezi wa haki za binadamu kikiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kuwasaidia kupata haki zao zinazoendelea kupotea.

“Tunaomba msaada wa haraka, vinginevyo tutapoteza kila kitu tulichoachiwa na baba yetu,” amesisitiza.
 
Marehemu angeaanda maelekezo mapema, famailia inaenda kupigwa hela
Maelekezo au wosia? Vyote hivyo havina maana kwa vile vinabatilishwa mahakamani ikitokea kuna wasiokubaliana na mgawanyo,!!
 
  • Thanks
Reactions: Lax
Maelekezo au wosia? Vyote hivyo havina maana kwa vile vinabatilishwa mahakamani ikitokea kuna wasiokubaliana na mgawanyo,!!
Duh, kumbw hali ndo ipo hivyo , sasa wosia una maana gani? Maana mali si ni za marehemu ndo mwenye jukumu la kugawa? Au hii mifumo tumeipokea kishingo upande?
 
Mbona wenzetu wahindi na ngozi nyingine tofauti na hii ya kimatumbi nadra kusikia migogoro ya mirathi
 
Maelekezo au wosia? Vyote hivyo havina maana kwa vile vinabatilishwa mahakamani ikitokea kuna wasiokubaliana na mgawanyo,!!
Mfano mzuri ni mzee Mengi aliandaa wosia kuwa mali zote zibaki kwa Jacqueline Ntiyabaliwe na watoto wake 2 mapacha, lkn mahakama iliutengua wosia huo.

Wosia wa Augustine Lyatonga Mrema pia ulitenguliwa. Alikuwa ameamuachiq mkewe aliyemuoa miezi 6 kabla ya kifo chake: nyumba 2 za Sinza pamoja na gari moja.
 
kwakuwa cc ni wa matumbi
Mfano mzuri ni mzee Asasi wa Iringa huko huko Iringa, ni miaka takribani 5 tangu afariki lkn hakuna mgogoro wowote.

Tatizo la ngozi nyeusi ni namna tunavyoupata utajiri wenyewe; ni kwa wizi, dhulma na uchawi. Haya ndiyo huacha laana kwa familia.

Kingine ni uvivu wa watoto na ndugu wa marehemu kutafuta vya kwao. Mfano huyu Sarah, yeye ni nini kinamuuma sana ikiwa mamake wa kambo, ambaye alikuwa akimpa usingizi mzee Ilomo ndiye anauza na kuzitumiq mali za mumewe? Anajua ni namna gani huyu mamake wa kambo alivyokuwa akijituma kitandani?

Kama huyu Sara anadhani ni rahisi kumpa mtu utamu mpk aweze kufikiri vizuri na kutajirika, basi naye afanye kwa mumewe au hawara yake.
 
Mfano mzuri ni mzee Asasi wa Iringa huko huko, ni miaka takribani 5 tangu afariki lkn hakuna mgogoro wowote.

lakini pia hata watoto wetu hawaambiwi na kushirikishwa namna utajiri ulivvyopatikana. wakiona baba/mama ana mali wao hujibweteke wakisubiri kifo cha baba/mama ili warithi.huwezi kurithi kitu usichokijua
 
Utajiri wenyewe wa hao wazazi unapatikana kwa njia batili; kama uchawi, kafara, wizi, rushwa na dhulma. Ndiyo maana wazazi wanashindwa kuwashirikisha watoto. Unakuta mtu ana supermarket yake, lkn akitumbuliwa kazini kwake na supermarket inakufa.

Kuna mtu ana duka kubwa sana, lkn kila siku duka lile linafunguliwa na kufungwa na yeye tu. Na siku akiugua na kulazwa anapiga marufuku duka kufunguliwa. Why?

Tuacche janja janja kwenye maisha.
 
Polen sana aisee

Mngehurumiana wote mkapata kwa umoja
 
Mfano mzuri ni mzee Asasi wa Iringa huko huko, ni miaka takribani 5 tangu afariki lkn hakuna mgogoro wowote.

Tatizo la ngozi nyeusi ni namna tunavyoupata utajiri wenyewe; ni kwa wizi, dhulma na uchawi. Haya ndiyo huacha laana kwa familia.

Kingine ni uvivu wa watoto na ndugu wa marehemu kutafuta vya kwao. Mfano huyu Sarah, yeye ni nini kinamuuma sana ikiwa mamake wa kambo, ambaye alikuwa akimpa usingizi mzee Ilomo ndiye anauza na kuzitumiq mali za mumewe? Anajua ni namna gani huyu mamake wa kambo alivyokuwa akijituma kitandani?

Kama huyu Sara anadhani ni rahisi kumpa mtu utamu mpk aweze kufikiri vizuri na kutajirika, basi naye afanye kwa mumewe au hawara yake.
Mada ya huzuni, lakini kwa comment hii nimecheka kifala sana😃😄😁😊
 
sisi baba yetuu mdogo akishirikiana na watoto wakambo akatala kutuzimq kiwanja cha mzee kuja kushtuka kha tukawahi.mahakamn fasta tukamstopisha asifanyr chochote baadae tukamwondoa

Aliandika mzee kawasaki watoto wakambo tukanza dili na watoto wakambo mahakaman watupe docs 😂
😆 😂 wakatuletea mkataba feki walinunua kilr kiwanja 2002...wakaulizwa kwahi sio cha babayenu mmenunuaje wakati mmesema mwamnzo megawiwa aisee

Nikawapa copy ya mkatabanwa mzee alionunua 1987,, wakaulizwa unafahamu hizi docs hizo hatujui

Wakanza kuchunguza saini za mzee wakaenda kwa mtoto wamarehemu akasema kweli huo ndio mkataba

😂 😆 😂 😆 wakaambiwa mtafungwa mjipangr hizi mali za babazenu na mtahawana sawa kama zingine mlivyogaiana

Schizo ukaishia hapo ...hamad miezi 3 mara papa serikali ikatangaza kuchukua enjoy na kulipa wahanga...wakatuita wakafanya evaluation tukapewa barua kusubiri.malipo wanagawa kwa awarmu wako watu kama 1890

Aise.mirathi sikia kwa watu.mnauwana
 
Back
Top Bottom