Watoto wa Mjini Dar


yale yaleee
 

He is more of "Baharia" in the sense of msafiri wa zamani zaidi ya sea man.

Speaking of mabaharia wa zamani, Jah Kimbute katika bio yake anadai alipata kupenda muziki wakati akiwa baharia mitaa ya udachi huko Marota, jamaa kweli au fix tu? Kuna mabaharia waliokaa bichi la Rotterdam wanamjua kwenye chama lile?
 
Chill out Mrembo,

Hayo maneno tu,GT unakuzuga muda mwingine tuna hitahi kitukingine zaidi ya seriousness ya politics.
Hapa kijiweni kama mtu anaku-annoy nyamaza
 

HNdio hiyo hiyo heoteli ya WATINDIKA ile kila ukipita pale wanajidai wao wa Zaire hawajui kiswahili tena iko nyuma ya hoteli ya RIKI HILL(by the way kati ya wachagga safi yule Riki safi sana )



Kusema ukweli kati ya Migo Migo na Temeke nadhani TEMEKE aka MKOA WA PWANI wale walitoa Mabaharia wengi zaidi lakini wengi wao hawakurudi walitokomea na wengi walikufa

Migo miko kulikuwa na mabaharia wengu lakini ukweli ni kuwa wengi wao walikuwa watu wa BWIMBWI tuuu...and please dont mention akina BAGHDELLA au BOB RICHARD

pamoja na tabia yetu ya kudharau watoto wa TEMEKE lakini kule mjomba kumetoa na Manunda wa kila namna. Ebwana ukishuka hapo Hillbrow, Jburg utakuwa watoto wa Temeke ndio waliojazana pale. Na zaidi utakuwa wengi wao ndio walishalowea na hata majina utakuwa wamebadili maana walipoona ulaya hakuingiliki na wale wanawake wa Kisaudi wenye miiili mikubwa tena bas, jamaa wakao na majina utasikia wanajiita akina DLAMINI

Watoto wa MIgo migo wengi walitoka kwenye femili ambazo waliweza kuchagiwa safari na wengi waliprudi mambo yalikuwa safi na ushahidi upo mpaka leo ukishuka kwenye maghetto ya pale new Delhi...maana le ndio ilikuwa line ya kwendea PASHAWAR na kule Pashawar ilikuwa waabe tuu ndio wanaokwenda.

Ahh we acha tuuu
 

Sawa kaka,

Halafu tunapata wapi moral authority ya kuongelea copyright violations?
 

very true

hilo nawapa respect watoto wa TEMEKE yaani halina ubishi hata kidogo

nadhani hasira zaidi zilikuwa walikuwa wanaona MITEMBA inaingia na kutoka wakati watoto wakishua walikuwa wanatengenezewa ma dischaji buku kule tegeta

wee acha tuu
 
Ha ha ha,Hii ndio ilikua DASLAM,
Walioshindwa kupanda meli waliishia kuuza MAGENDO (sigara) na kucheza mpira yanga na simba.

si kweli

walioshindwa meli waliiishia kwenda SHAMBA DOGO

get your facts right

biashara za magendo zilikuwa za wachagga waliokuja mjini pale kufungua maduka

umeona mzaramo au mndengereko gani akawa na akili ya kukaa kutwa nzima anasubiri watu waje kununu kitu dukani?
 
game theory,unamwambia pundit,kwamba box lenyewe la mitikasi? pundit hakuelewi maana yeye anaonekana ni mtu straight,no shortcuts.

mwafrika wa kike naona kama umechanganya thread,naona hili baraza halikufai
 
HNdio hiyo hiyo heoteli ya WATINDIKA ile kila ukipita pale wanajidai wao wa Zaire hawajui kiswahili tena iko nyuma ya hoteli ya RIKI HILL

Sana tu wanajazana kwa fundi viatu/ shu shaina chini pale....
 

kwa standard ipi umetumia kuandika kuwa hili baraza halinifai?
 

Muulize kama unamjua Athumani China (kiungo wa yanga zamani,yupo huko juu) alikua na mshikaji wake wanasaka pesa ya kupaa seaman book wakaona bora wauze sigara za magendo (wakati huo deal) 1984-5 mwenzie akaitoa yeye akaishia kucheza mpira yanga.
Labda nyinyi watoto wa KKOO mlikua njia nyingine ya kupata pesa
 

Sana tu sio lazima kila thread awe anazungumziwa Yona na Mkapa.....Hapa ni kama ulishawahi kuzuga mitaa ya kati, kufanya dili za hapa na pale ofisi mkononi, na kuwa mtu wa maskani ndo unakaribishwa....
Kama wewe ulikuja Dar kumsalimia mjomba wa TRA ukawa geti kali ili usifundishwe uhuni....wewe pitiliza tu....sio penyewe hapa.
 
nasikia piraeus,ugiriki kulikuwa na agent wa meli mgirki anaitwa lambros mpaka kiswahili anaongea
 

Mkuu nadhani umesahau kuweka maneno kuwa.... kama ulikuwa Dar muda mfupi baada ya uhuru wa Tanganyika. Au maneno kuwa ... kama wewe una umri zaidi ya miaka 50 basi changia hii thread.

Kwa misingi hiyo... hii thread inahitaji title mpya
 
Mkuu nadhani umesahau kuweka maneno kuwa.... kama ulikuwa Dar muda mfupi baada ya uhuru wa Tanganyika. Au maneno kuwa ... kama wewe una umri zaidi ya miaka 50 basi changia hii thread.

Kwa misingi hiyo... hii thread inahitaji title mpya

Dadaaa hili wala halihitaji age range.....kama utakuwa umeifuatilia, watu wameulizana watu, vitu na sehemu za aina mbalimbali na generations tofauti...kama kiulizwacho hakikutokea kwenye hood lako unakaa kimya unaipisha point ipite wewe unadakia ambayo inakuhusu...watu wanamove on...Just out of curiosity...unakuwa offended nini pindi watu wakiizungumzia Dar bila hata ya kufika Kibaha Picha ya ndege?
Kama ni hivyo sorry....
 
mama punguza munkhar,pumzika tu hii flow humu ndani,is beyond thee comprehension. many thanks
 

Ni wapi nimeandika kuwa niko offended? ... Hii ni thread kama zingine zozote hapa JF na nina kila haki ya kuchangia kile ninachoona kinafaa. Au sio?
 
mama punguza munkhar,pumzika tu hii flow humu ndani,is beyond thee comprehension. many thanks



Kipimo kipi hicho kimepima comprehension ya hii thread na ikaonekana kuwa iko beyond any point? Wewe changia tu thread kama ulivyokuwa unafanya mkuu, ukiona ninayoandika ni pumba.... una kila sababu ya kutosoma kila ninachoandika.

Mimi ninachangia context ya kile kilichoandikwa hapa kuanzia mwanzo wa hii thread hadi sasa hivi.

Many thanks
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…