wee msen£$%^ weee
hawa jamaa umewajuaje?
duhh! noma kichizi
sasa ngoja nikupe mkanda mzima ulivyokuwa
MALIMA aka mzee COSBY au COZBY alikuwa ni mtoto wa magomeni mapipa kuleee nyuma ya ofisi za wilaya na alikuwa na mshikaji wake anaitwa COASTER au COSTA
Hawa jamaa walikwenda ITALI enzi zile MARADONA ndio anachezea NAPOLI na walipobiga bao wakatuma pesa kwa mjomba wao awanunulie nyumba na ndio ile nyumba waliokuwa wamepangisha wale Malaya
Sasa 1989 alima aliporudi mambo safi na ndio alirudi na lile Guruwe Jeusi lilikuwa na mastika kibao ya BOB MARLEY na wakawa poa sasa ikaja tripu ya pili ambayo ilidibi COSTA urudi shamba dogo ndipo noma likatokea kwa sababu waliibiwa New Delhi tena kwenye maskani ya watoto wa Kibongo - Pahar Ganj, pale Green Guest House...kama kuna watu wana nyeti zaidi watakupeni mkanda mzima...hao itakuwa jamaa zake FMES hao akija mwenyewe atakuambieni
Anyway yule anko alipoona kuwa jamaa hawana hati ndipo akawachenjia na hapo ndipo wataalam wa International Relations wanakuambia wa THE "WATERSHED MOMENT" na wakaanza kulaumiana na eventually haata urafiki wenyewe ukaisha
By the way nasikia yule ANKO alishavuta sijui kama kweli
Hapo mzee COSBY akaamua kurudi tena shamba na kule kama kawaida mzigo inabidi uutesti mwenywe kama huwezi basi unamkodisha testa ...sasa kama ndio ushaondoka bongo kiguu juu sasa kuna cha kumpa pesa tesa? eventually kaanza kuutesi mwenyewe na mwishowe naye akawa JUNKI
Wakati huo tena kule Migo migo wanawake wa kiswahili wanampakazia COSTA watoto left and right na nasikia naye aliamaua kutiimua...si unajua tena sie waswahili...yakitushinda basi ndege ndio rafiki yetu mkubwa na mara ya mwisho ilikuwa about 10 years ago niliskia alionekana BURUDA
ile nyumba sijui iliishia wapi
Of couse naikumbuka sana ile fulana na jezi ya JOHNSON ya LAKERS na hiii inanipelekea kumzungumzia SUBJECT no 2 kwenye hiyo post yako bwana MSAFIRI
MSAFIRI alikuwa mweupe hivi na mfupi na mpenzi wa mpira ile kinoma....nitakuwa nakuongopea sijui aliishia wapi lakini ninachokua alikuwa na washikaji zake wanauza mitumba hivyo hata zile spea si zipte zilikuwa zinatoka viwanja na kwa sababu deri la mitumba likifunguliwa yeye huwa yupo so kila siku yeye ni mtu wa kupendeza tuu sijui kama aliacha tabua ya kuninginiza kitambaa matakoni kwenye jeans
HAMIDU MACHUA aka DALAMINI
Hamidu ndio alishalowea kule Cape town na mshikaji wake HIMIDI alipopigwa palanja UK aliamua kumjoin...inshort ninavyojua mimi habri za mwisho za MACHUPA ni kua alifungua BED AND BREAKFAST kwenye mji mmoja unajiwa CARTHAGENA ...eti target ilikuwa ni wale wanaofanya ECO-TOURISM wakati mwenyewe nadhani unajua whats up?
Once again dont be decievd Machupa ni mtoto wa TEMEKE kama wengine na kwao ni TABORA in short ni MNYAMWEZI ambaye kalelewa na wazaramo na sasa hivi ni raia wa RSA! inshort hatembei na ile kadi ya CCM
Cant knock the brothers Hustle
MALAYA:
Uliowataja yule migoko alikuwa anaitwa PAMELA alipata bwana wa KIDHUNGU na alivuta huu mwaka wa pili
Anty Mele naye alivuta
Bubu nasikia alikwenda Ujerumani na mDHUNGU wake
and having said that Unakumbuka lile booty la DINA anty yake BANDORA?
Costa namkumbuka.
Nilikutana na mdogo wake Himidi, anaitwa Ahmed, mwaka jana kama sikosei. Nafikiri anaishi NY. Halafu walikuwa na dada yao aitwaye Kulthum alikuwa na utege fulani hivi. Mh mh...unamkumbuka?
Hivi unajua mdogo wake na Machupa (Chipeta) walimpiga shaba Sauzi? Hii inanikumbusha kuna dogo mmoja hivi aitwaye Ilamenya. Huyu dogo aliuzaga Pick-up ya dingi yake na akazamia Sauzi. Mshikaji alivyorudi, alikuwa na grill mdomo mzima. Basi alikuwa anakenua meno muda wote, kama mwehu, ili watu waone grill zake. Nasikia mshikaji wali mgun down pia.
Halafu George Gordon yuko wapi siku hizi?
Yule magoti bubu alikuwaga bomba sana. Hivi unamkumbuka Jumanne (J), mdogo wake na Daruweshi? Huyu mshikaji alimaliza mambo kwa bubu kwa kumdanganya kuwa atampatia visa ya kwenda marekani. Nakumbuka mshikaji alichukuaga fomu za kuomba visa za marekani na kujaza info za yule magoti. Basi bubu kwa kutojua akadhani hiyo ndo visa yenyewe. Akasaula!
Halafu J alikuwa na uchungu na mtoni wakati wengi wetu tulikuwa hatuna hata wazo la kuanza. Nakumbuka mshikaji akiona pipa (hata kama ni Air Tanzania) angani alikuwa anachanganyikiwa. Kila siku alikuwa anasema "one day yes!" Basi tukawa tunamwambia aanze kutembea kwa miguu taratibu tu atafika...Pwani, Tanga, Arusha, Nairobi...mpaka atafika tu.... Ukweli ni kwamba, mshikaji alichangia kutuingizia vijana wengi, pale kijiweni business, idea ya kuja mtoni. Kila akija kijiweni ndio zilikuwa story zake. Matokeo yake wengi tukajawa na jazba na kutimua, halafu mshikaji akakwama Bongo. Anyway, tetesi ni kwamba siku hizi mshikaji ni jambazi la kutumia silaha.
Namkumbuka yule mnywaranda Dina. Duh alikuwa na kiuno cha dondora. Hata yule dada yake (mama bandora) alikuwa hivyo hivyo tu. Vipi Masha Makata unamkumbuka? Huyu dada we acha tu! Sijui yukowapisiku hizi? Halafu mama yake si ndo alikuwa Miss Tanzania wa kwanza kabisa (miaka ya 60?)