Watoto wa siku hizi hawajui kabisa enzi zetu uliweza kuchapwa kwa sababu zifuatazo...

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]ulikuwa billionaire kwa muda siku hiyo

Jr[emoji769]

Ndiyo hicho kilichoniponza. Ni yule yule niliyemwibia hela alikuja kugundua baada ya kurudi nyumbani, kwa sababu kati ya waliokuwa wanakula hizo Sungwi, alikuwa ni rafiki yangu anaitwa Joseph Bujiku, na ambaye alikuwa anasoma darasa moja na mtu aliyekuwa ameibiwa hela hiyo, mimi nilikuwa darasa la nyuma yao mwaka mmoja!
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Ukiumia kwenye mpira ukirudi nyumbani utachapwa.

Ukienda kuogelea baharini ukirudi nyumbani utachapwa

Usipo onekana saa ya kula utachapwa
kumbe wewe wa hapa pwani..... sisi ilikuwa mtoni, tena unachapwa kama maji yamefurika ukaenda kuogelea.
 
Ole wako ubebeshwe mdogo wako mgongoni kisha baada ya muda ukutwe umefungua kanga au mbeleko na mtoto yuko chini!
 
kijana wa kike na wa kiume mkikutwa tu mmesimama kwenye kona flani au njiani ktk hali ya kutia mashaka mnakula bakora
 
Ukipiga Mkwara wa kujiua hauchapwi ila usipojiua unachapwa...

Sent using Jamii Forums mobile app
Imekumbusha mbali, mimi na brother tulimfanyia ndivo sivyo mdada wa kazi akamwambia maza, tulipata mkongoto wa hatari bro akaona isiwe taabu akachukua dawa ya Thiodane eti anaenda kujiua,Maza akumfata machakani na akatupiga mkwala wote hakuna kumfuata tumwaache afe tutazika!So bro amekaa machakani mpk usiku wa saa mbili anaona kimya akaamua kujirudisha home ndo akakuta na faza keshatoka job na keshapewa mkasa wote.
Aisee walivomwoona amerudi walimgombania kama mpira wa kona na no msosi
Aisee hakuwahi tena kufanya au kujaribu ujinga km huo kamwe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kazi kweli kweli!
 
ukichapwa ukakimbilia nje ya nyumba utachapwa tena
ukila nyama au samaki ikaisha kabla ya chakula lazima uchapwe
ukisema nyumbani hatujala lazima uchapwe, ukakaribishwa na jirani kula sema nimeshiba!
 
Aisee acha kabisa ndugu yetu yeye tukiwa likizo kwa babu, siku moja asubuhi tunajiandaa kwenda shamba nyuma tu ya nyumba yeye akagoma na kutishia kujinyonga (sijui ugomvi ulianzia wapi na babu)
Babu akasema mwacheni ajinyonge nitazika.... Basi tukaenda shamba... Muda si mrefu tukasikia mtu anapiga kelele, kukimbia kufika home, jamaa ananing'inia ila kaweka mikono kwenye shingo kamba isimbane... Kumbe alitundika kamba kwenye kenchi akapanda juu ya kiti akajitia kitanzi, akakipiga kiti teke kikaanguka... Maumivu yalipozidi akijiokoa kwa kuweka mikono kooni na kupiga kelele
Babu alipokuja tukajua atapaniki na kusema tumshushe
Kwa mshangao wa wengi babu alikuja na mkwaju wa mpera... Jamaa alichezea kichapo mpaka akakojoa ndio tukamshusha... [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]sasa hivi ni boss mkubwa mahali... Siwezi hata kumkumbushia

Jr[emoji769]
 
ukichapwa ukakimbilia nje ya nyumba utachapwa tena
ukila nyama au samaki ikaisha kabla ya chakula lazima uchapwe
ukisema nyumbani hatujala lazima uchapwe, ukakaribishwa na jirani kula sema nimeshiba!
[emoji23][emoji23][emoji23]

Jr[emoji769]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…