Sky Eclat
JF-Expert Member
- Oct 17, 2012
- 57,761
- 216,011
Enzi zetu chumbani mnalala na bibi, shangazi, dada wa kazi ukiwa na bahati unaweza kuwa na kitanda chako mwenyewe. Hawa wageni wanaweza kukaa miezi sita na maisha yaliendelea.
Hawa watoto wa siku hizi vyumba vyao ni kama private home. Hata mzazi huruhusiwi kuingia. Umwambie bibi amekuja utalala nae, hata kama kuna kitanda cha ziada kama picha hapo juu. Utaona sura itakavyombadilika.
Ninadhani social media zinachangia pia. Wengine hawalali wanakesha Instagram. Sasa bibi asubuhi atakwambia kuwa mwanao alikesha kwenye simu.
Yaani siku hizi inabidi ujenge chumba cha wageni. Ile budget ya vyumba vitatu vya kulala utamshuhudia mama yako analala sebuleni kwenye nyumba uliyojenga mwenyewe.