Watoto wa siku hizi hawatoi ushirikiano wa kulala na wageni vyumbani mwao

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011


Enzi zetu chumbani mnalala na bibi, shangazi, dada wa kazi ukiwa na bahati unaweza kuwa na kitanda chako mwenyewe. Hawa wageni wanaweza kukaa miezi sita na maisha yaliendelea.

Hawa watoto wa siku hizi vyumba vyao ni kama private home. Hata mzazi huruhusiwi kuingia. Umwambie bibi amekuja utalala nae, hata kama kuna kitanda cha ziada kama picha hapo juu. Utaona sura itakavyombadilika.

Ninadhani social media zinachangia pia. Wengine hawalali wanakesha Instagram. Sasa bibi asubuhi atakwambia kuwa mwanao alikesha kwenye simu.

Yaani siku hizi inabidi ujenge chumba cha wageni. Ile budget ya vyumba vitatu vya kulala utamshuhudia mama yako analala sebuleni kwenye nyumba uliyojenga mwenyewe.
 
Hahahaha hatari ila haipendezi kulala na watu wengine kitanda kimoja au chumba kimoja,kama una utaratibu wa wageni ni bora uwe na mjengo mwingine pembeni kwa ajili ya wageni tu au kama una ukwasi wa kutosha unapiga floor mbili kwa ajili ya wageni.
 
Hahahaha hatari ila haipendezi kulala na watu wengine kitanda kimoja au chumba kimoja,kama una utaratibu wa wageni ni bora uwe na mjengo mwingine pembeni kwa ajili ya wageni tu au kama una ukwasi wa kutosha unapiga floor mbili kwa ajili ya wageni.
Ndugu yangu mshahara wenyewe huu wa darasa la 12, baada ya makato unabaki na laki mbili. Kiwanja ulinunua kwa mkopo na umefanikiwa kupandisha vyumba vitatu leo Diva anasema anataka privacy yake.
 
Zama zimebadilika...

Malezi ya siku hizi sio kama zamani! wazee waliotoka kijijini na ku-fight kupata maisha mazuri walikuwa wanaelewa maana undugu na hawakuwa wachoyo kwani wanajua walipotoka. sasa vijana wa siku hizi kidogo mambo mengi na tofauti!

Ila pia dunia imebadilika, unaweza mkaribisha mtu kwako kumbe ana lake jambo!

Kazi kweli kweli!
 
Ndio maana mm nimetega kamera vyumba vya watoto wangu wote wa kike na kiume.....
lazima niwacheki in a close range.....
sipendi surprise kabisa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…