Tambua kuna mzazi maskini kucha kutwa anahangaika kutafuta mkate wa familia yake,alipe kodi ya nchi na kodi lukuki za familia yake ,anaamka saa kumi usiku kuwahi masokoni kuchagua bidhaa za kuuza.Naunga mkono hoja, ila malipo hayo sio kwa ajili ya kuwatia moyo bali ni compensation of loss of parental love and parental quality time with their children and kupunguza mateso ya ridicule kwa wazazi wao, wao ndio waathirika.
P
Naunga mkono hoja, hata waume wa makatibu muhitasi nao walipwe fidia wake zao wanashinda ofisini na bosi muda mwingi, wakati wa Bunge sometimes hadi saa 6 usiku!, mke anafika home exhausted, hiyo kushindwa kutekeleza yale majukumu ya ndoa kikamilifu. Hivyo waume zao wanastahili compensation!.Hata wake za madereva wa viongozi walipwe waume zao wanatumia muda mwingi nje ya familia kuendesha viongozi
Ati nini?Hata familia za marafiki wa viongozi ziwe zinalipwa
Naunga Mkono Hoja na Imekaa vizuri Pia ila Uongeze na Watoto wa WKuu wa Mikoa Ma RPC na wakuu w jeshi ngazi za mikoa
Mkalime na mjiajiri
msigwaTusiishie hapo tu hata wakwe zao yaani ukioa au kuolewa kwenye familia ya kiongozi pia ulipwe, ndugu wajomba mashangazi mabinamu na wajukuu wote walipwe.
Mpaka wafanyakazi wa ndani na wafungua mageti na madereva pia walipwe na serikali tena.
Maoni yangu naomba yaheshimiwe.👆✌️
Dah!Halafu pia napendekeza Ili kutokomeza umasikini mijini masikini wote watokomezwe
Na wajukuu walipiwe ada za international schools sababu ndio viongozi wa keshoWATOTO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIPWE ILI KUWATIA MOYO.
Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.
Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.
Lakini ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa na watoto wa viongozi wa taifa letu tukufu.
Watoto wa Marais Walipwe.
Watoto wa Makamu wa rais Walipwe.
Watoto wa Spika wa bunge walipwe
Watoto wa Waziri Mkuu walipwe!
Watoto wa Jaji Mkuu walipwe.
Watoto wa Ma-IGP walipwe.
Watoto wa Wakurugenzi wakuu wa TISS walipwe.
Wapewe Mishahara hata milioni moja au mbili au tatu hivi kwa mwezi. Hayo ndio maendeleo. Wazazi wao wanatumikia nchi hilo nani atabisha?
Wazazi wao wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kuhangaikia nchi, nani anabisha? Wazazi wao wanatukanwa na wananchi wakati mwingine bila kosa nani anabisha?
Walipwe! Walipwe! Tuwalipe! Kodi ni zetu na wao ni viongozi wetu. Tunafurahi wakilipwa. Sisi tutawatumikia kama wao wanavyotutumikia ili kuiendeleza nchi.
Watoto wa viongozi jiandaeni. Tutawalipa kila mwezi. Ni bora tuwalipe tuu kuliko mjilipe wenyewe kwa kificho. Hata tusipowalipa tunajua mtajilipa kivyovyote tuu.
Muswada upelekwe bungeni, kisha upitishwe. Watoto nao walipwe.
Ambao hawataki wahame nchi.
Tusiishie kuwalipa Wenza wao(waume na wake zao) twendeni mbele zaidi. Tuwe na jicho la mbali kama tai.
Mimi nimemaliza, hayo ni mawazo yangu. Kama hutaki hayo ni mawazo yako na kwangu sio shida.
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Kabisa na wakiona hawatosheki wasikae kinyonge,wateme nyongo tutaenda hata kukopa huko Ma IMF na Ma WB. Sisi tunataka wawe na Complete Peace Of Mind ikibidi wasife na wakifa wasioze[emoji1787]