Watoto wa viongozi wakuu wa nchi walipwe ili kuwatia moyo

WATOTO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIPWE ILI KUWATIA MOYO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.

Lakini ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa na watoto wa viongozi wa taifa letu tukufu.

Watoto wa Marais Walipwe.
Watoto wa Makamu wa rais Walipwe.
Watoto wa Spika wa bunge walipwe
Watoto wa Waziri Mkuu walipwe!
Watoto wa Jaji Mkuu walipwe.
Watoto wa Ma-IGP walipwe.
Watoto wa Wakurugenzi wakuu wa TISS walipwe.

Wapewe Mishahara hata milioni moja au mbili au tatu hivi kwa mwezi. Hayo ndio maendeleo.
Wazazi wao wanatumikia nchi hilo nani atabisha? Wazazi wao wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kuhangaikia nchi, nani anabisha? Wazazi wao wanatukanwa na wananchi wakati mwingine bila kosa nani anabisha?

Walipwe! Walipwe! Tuwalipe! Kodi ni zetu na wao ni viongozi wetu. Tunafurahi wakilipwa. Sisi tutawatumikia kama wao wanavyotutumikia ili kuiendeleza nchi.

Watoto wa viongozi jiandaeni. Tutawalipa kila mwezi.
Ni bora tuwalipe tuu kuliko mjilipe wenyewe kwa kificho. Hata tusipowalipa tunajua mtajilipa kivyovyote tuu.

Muswada upelekwe bungeni, kisha upitishwe. Watoto nao walipwe.
Ambao hawataki wahame nchi.

Tusiishie kuwalipa Wenza wao(waume na wake zao) twendeni mbele zaidi. Tuwe na jicho la mbali kama tai.

Mimi nimemaliza, hayo ni mawazo yangu. Kama hutaki hayo ni mawazo yako na kwangu sio shida.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
Naunga mkono hoja, walipweeee ila umenisikitisha kuwasahau baba na mama zao nao walipweeee!
Na kama kuna mpambe anapendwa sana na kiongozi nae alipwe.
Nchi tajiri sana hii. CCM oyee.
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Wakimaliza hapo wawalipe wajakazi wao, wajakazi wanafanya kazi kupitiiza kuhakikisha hawa miungu wanaishi vizuri, bao kodi zetu ziwalipe tu.
 
  • Kicheko
Reactions: EEX
Vipi kama ungekuwa upo kundi la wanaopendekezwa kulipwa[emoji848]
Sihitaji utajiri unaopatikana kwa kuwafanya wengine masikini. Nataka utajiri unaotokana na kuwatajirisha wengine. Huyo ndio Mimi and I'm going to make it[emoji120]
 
Kama haya ndo mawazo ya mtu mzima na pengine anaiongoza familia na huku akijua kuwa taifa limekosa hata umeme wa uhakika,maji Safi na salama,dawa,ajira,mfumko wa bei n.k halafu anaomba watoto wa viongozi walipwe ni upumbavu wa kiwango.Hao viongozi wao Wanawajibu gani kwa familia zao? mleta Uzi nakuona kama umetindikiwa afya ya akili vile.
 
Wewe ndiyo tunakushangaa wakati sisi wenye nchi tumeshakubari walipwe. Walipwe tu, hamna namna. Walipwe hata na michepuko yao.
 
Naunga mkono hoja. Na mademu/michepuko wa viongozi walipwe mishahara.

Pia wapewe na kinga ya kutoshtakiwa kwa makosa ya jinai pindi wanpokua kwenye kuhudumia viongozi wetu.
 
Kama vipi wachukue tu nchi yote waile
Maanantumechoka sasa
 
Kama haya ndo mawazo ya mtu mzima na pengine anaiongoza familia na huku akijua kuwa taifa limekosa hata umeme wa uhakika,maji Safi na salama,dawa,ajira,mfumko wa bei n.k halafu anaomba watoto wa viongozi walipwe ni upumbavu wa kiwango.Hao viongozi wao Wanawajibu gani kwa familia zao? mleta Uzi nakuona kama umetindikiwa afya ya akili vile.

Ahsante kwa maoni
 
WATOTO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIPWE ILI KUWATIA MOYO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.

Lakini ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa na watoto wa viongozi wa taifa letu tukufu.

Watoto wa Marais Walipwe.
Watoto wa Makamu wa rais Walipwe.
Watoto wa Spika wa bunge walipwe
Watoto wa Waziri Mkuu walipwe!
Watoto wa Jaji Mkuu walipwe.
Watoto wa Ma-IGP walipwe.
Watoto wa Wakurugenzi wakuu wa TISS walipwe.

Wapewe Mishahara hata milioni moja au mbili au tatu hivi kwa mwezi. Hayo ndio maendeleo. Wazazi wao wanatumikia nchi hilo nani atabisha?

Wazazi wao wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kuhangaikia nchi, nani anabisha? Wazazi wao wanatukanwa na wananchi wakati mwingine bila kosa nani anabisha?

Walipwe! Walipwe! Tuwalipe! Kodi ni zetu na wao ni viongozi wetu. Tunafurahi wakilipwa. Sisi tutawatumikia kama wao wanavyotutumikia ili kuiendeleza nchi.

Watoto wa viongozi jiandaeni. Tutawalipa kila mwezi. Ni bora tuwalipe tuu kuliko mjilipe wenyewe kwa kificho. Hata tusipowalipa tunajua mtajilipa kivyovyote tuu.

Muswada upelekwe bungeni, kisha upitishwe. Watoto nao walipwe.
Ambao hawataki wahame nchi.

Tusiishie kuwalipa Wenza wao(waume na wake zao) twendeni mbele zaidi. Tuwe na jicho la mbali kama tai.

Mimi nimemaliza, hayo ni mawazo yangu. Kama hutaki hayo ni mawazo yako na kwangu sio shida.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam

Umesahau koo zao pia zina umuhimu mkubwa maana bila hizo koo wasingekuwepo[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Naunga mkono hoja, ila malipo hayo sio kwa ajili ya kuwatia moyo bali ni compensation of loss of parental love and parental quality time with their children and kupunguza mateso ya ridicule kwa wazazi wao, wao ndio waathirika.

P
Waalimu na Madaktari wao hawapatu hizo adha!!!

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Ndiyo Walipwe walipwe maana wanavuja Jasho kwa ajili ya kutetea Baba zao na wanapata Emotion Demage pia. Walipwe maana wanakaa mbali na Upendo wa Wazazi wao pindi wakiwa katika shughuli za kiserkali
Wanakuaje mbali,kwani Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri hawakai na familia zao,muda wote wapo kazini?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
 
Wanakuaje mbali,kwani Rais, Makamu wa Rais, Waziri Mkuu na Mawaziri hawakai na familia zao,muda wote wapo kazini?

Sent from my V2111 using JamiiForums mobile app
Hawakai mkuu Ikulu ni ofisi sio nyumba ya kuishi..

Kingine Ratiba yote ya Waziri ya mwaka mzima imeshaandaliwa na TISS pamoja na viongozi wote wa Juu na ziara zake zote ...

Kwahyo muda mwingi yupo wizarani na Kuzunguka Nchi nzima kwa Ziara..Je ni lini anakuwa na familia yake..
Jiulize muda anaopata labda ni ule anaoenda wizarani au anaoenda Bungeni..
Lakini wanae au familia yake iko Huko Lindi unafikiri ni lini hasa anakuwa Lindi..
 
Hawakai mkuu Ikulu ni ofisi sio nyumba ya kuishi
Wanakaa wapi?Ata Mimi Baba yangu alikuwa Mfanyabiashara anasafiri kila mara na kampuni zake zilikuwa zinalipa Kodi kubwa tu serikalini.Basi na sisi Watoto wa Wafanyabiashara tufikiliwe iyo posho ya upendo![emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Mkuu huo ni unyonyaji,sidhani ata katika mataifa tajiri kitu kama icho kipo,yeye aliomba kazi ya Urais akijua gharama zake kijamii,sasa iweje leo tumlipe yeye mshahara na maposho kibao achilia mbali 10% wanazotupiga kwenye miradi,alafu leo tumlipe na mkewe kwa kazi gani!maana Rais anapewa mpaka wapishi na watu wa Bustani,sasa huyo mkewe anafanya kazi gani zaidi ya kumliwaza mwandani wake?
Hizi double standard hazitakiwi nchini!

It was sarcasm mkuu usichukulie serious
 
WATOTO WA VIONGOZI WAKUU WA NCHI WALIPWE ILI KUWATIA MOYO.

Anaandika, Robert Heriel
Mtibeli.

Nimefurahi muswada wa kuwalipa wenza wa viongozi wa nchi. Ni uzalendo wa hali ya juu sana. Hii itachochea maendeleo makubwa ya nchi.

Lakini ninaishauri pia serikali, isiishie tuu hapo iende mbali zaidi kuchochea maendeleo ya nchi yetu kwa kuwalipa na watoto wa viongozi wa taifa letu tukufu.

Watoto wa Marais Walipwe.
Watoto wa Makamu wa rais Walipwe.
Watoto wa Spika wa bunge walipwe
Watoto wa Waziri Mkuu walipwe!
Watoto wa Jaji Mkuu walipwe.
Watoto wa Ma-IGP walipwe.
Watoto wa Wakurugenzi wakuu wa TISS walipwe.

Wapewe Mishahara hata milioni moja au mbili au tatu hivi kwa mwezi. Hayo ndio maendeleo. Wazazi wao wanatumikia nchi hilo nani atabisha?

Wazazi wao wanatumia muda mwingi nje ya familia zao na kuhangaikia nchi, nani anabisha? Wazazi wao wanatukanwa na wananchi wakati mwingine bila kosa nani anabisha?

Walipwe! Walipwe! Tuwalipe! Kodi ni zetu na wao ni viongozi wetu. Tunafurahi wakilipwa. Sisi tutawatumikia kama wao wanavyotutumikia ili kuiendeleza nchi.

Watoto wa viongozi jiandaeni. Tutawalipa kila mwezi. Ni bora tuwalipe tuu kuliko mjilipe wenyewe kwa kificho. Hata tusipowalipa tunajua mtajilipa kivyovyote tuu.

Muswada upelekwe bungeni, kisha upitishwe. Watoto nao walipwe.
Ambao hawataki wahame nchi.

Tusiishie kuwalipa Wenza wao(waume na wake zao) twendeni mbele zaidi. Tuwe na jicho la mbali kama tai.

Mimi nimemaliza, hayo ni mawazo yangu. Kama hutaki hayo ni mawazo yako na kwangu sio shida.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Dar es salaam
yaani kati ya sheria ya ajabu iliyowahi kutolewa Tanzania, ni huu ushauri wa mama salma kikwete. mke wa waziri mkuu, mke wa rais, kweli anahitaji kingine chochote kile? kweli?
 
Back
Top Bottom