Una ubinafsi usiostahili. Mkulima asiye na hata kipato kidogo unachopata wewe afanye nini?
Wewe uliposoma hadi kufikia kwenye hicho kipato kidogo, wazazi wako pia walikuwa wabinafsi kiasi chako?
Sikuzongi kwa kuwa na msimamo wako huo wa kutaka wanao wapate elimu nzuri, lakini itakuwa jambo jema sana kama watoto wa wasiokuwa na uwezo kama wako nao wakapata fursa nzuri za kupata elimu.
Tatizo hapa sio uwezo wa kufanya hivyo kama taifa, ni uzembe tu wa watu wanaokabidhiwa majukumu haya ya kuhakikisha watoto wote wanapata fursa nzuri kwenye jambo mhimu kama hili la elimu.
Ni hawa "tunaowapigia kura" kama mada inavyosema, ndio kikwazo kikubwa katika jambo hili.