Watoto wa wapiga kura wanakosoma VS Watoto wa wapigiwa kura wanakosoma

Watoto wa wapiga kura wanakosoma VS Watoto wa wapigiwa kura wanakosoma

View attachment 1337183
Kuna Jamaa mmoja alifuta michezo Mashuleni..akachanganya Chemistry&Physics...

Akafuta kilimo na ufugaji ...alifanya mambo ya ajabu ajabu sana miaka ya 2000s...
Nadhani ilikuwa kabla ya 2000? Huyo unayemzungumzia atakuwa ni Mungai tu, sidhani kuwa kuna mwingine.

Elimu yetu imevurugika sana, na matokeo yake yanaonekana dhahiri nyakati hizi.
 
Mkuu sijijui, sidhani kweli kwamba wewe umesoma shule maalum Mzumbe kwa haya uliyoandika hapa juu kunijibu.

Kwanza umenisoma lakini hukuelewa nilichoandika; pili unaniweka mimi kuwa sehemu ya CCM na wala hata hayo niliyoandika sionyeshi mahali popote kuitetea CCM.

Kwa hiyo, hiyo elimu uliyopata huko kwenye shule maalum naona huitendei haki hata kidogo.

Ukitaka tujadili kwa kina hili swala la elimu ili ujue msimamo wangu juu ya jambo hili ninalojua wazi ndio msingi mkuu wa kila kitu kwa nchi yetu niko tayari sana, kwa sababu mjadala huo utakuwa ni kwa manufaa yetu sote, huenda na wengine pia.

Lakini kwa hapa ulivyoingia kichwa kichwa na kunijibu bila hata ya kuelewa nilichochangia, huitendei haki elimu unayosema umeipata wewe pamoja na kwamba wazazi wako hawakuwa katika hali ya kukupeleka kwenye hizo shule za wenye hela. Umekurupuka tu na kumwagika.

Kwa maoni yangu, wewe ndio ungekuwa mfano mzuri wa kutetea watoto ambao baba zao hawana uwezo wa kuwasomesha watoto katika hizi shule za wakubwa. Sasa sielewi msimamo wako huu hasa unatokana na nini.

Kwa kifupi, kama nilivyoeleza hapo mwanzo: elimu ni haki ya waTanzania wote bila kujali matabaka haya wanayotuwekea hawa waliopo madarakani. Hili ni jambo mhimu sana.

Kwa hiyo, tukikubaliana kwamba elimu ni haki ya kila raia wetu serikali inao wajibu wa kuhakikisha kwamba haki hiyo inapatikana kwa kila mtoto, bila kujali uwezo wa wazazi wake wa kumsomesha mtoto huyo.

Serikali inao wajibu wa kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango na katika mazingira yatakayomwezesha mtoto aipate elimu hiyo vizuri; yaani pawe na miundombinu wezeshi na walimu wa kutosha kuitoa elimu hiyo.

Hii haina maana kwamba serikali ikataze hao wenye uwezo wao hata hao wakulima watakaotaka kujinyima kila kitu kuwahudumia watoto wao kuwapeleka huko kwenye hizo shule za wakubwa.

Jambo mhimu hapa ninalosisitiza, ni serikali ihakikishe elimu inayoisimamia katika shule zetu za umma zinazosomesha watoto wetu maskini itolewe kwa haki na kwa usawa na kwa viwango vinavyotakiwa. Hili ni jukumu la serikali ambayo tunaipa nyenzo zote za kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Sasa, kama utanisoma na kunielewa hapa kwa mawazo haya, na bado ukataka kuniwekea 'lebo' za uCCM au chama chochote cha siasa, nitasema wewe huna akili kichwani.

Samahani sana mkuu Sijijui kama hili litakuudhi, lakini sina njia nzuri zaidi ya hiyo ya kufikisha ujumbe wangu kwako.
Kweli nilikurupuka nilisoma tu sentesi ya kwanza then nikajibu baada ya kukuweka kwenye praise team group lakini hata hivyo baada ya kwenda kusoma post yako ile niliyoiquote nadhani tuonaongea lugha moja
 
We hujui maana ya public services. Pia huelewi nn watu wanaongea. Kama serekali inayokusanya kodi katika nchi haiwezi kutoa huduma bora kwa jamii si iondoke madarakani? Huu ni mfano mmoja tu wa elimu, mtoa mada akionesha ukosefu wa maji safi na salama wewe utasema umechimba kisima chako? Vipi kuhusu barabara utajenga za kwako pia? Unafkiria vibaya kabisa katika ubongo wako.
Wewe endelea kufikri vizuri kwa kuisubiri serikali ikusomeshee watoto. Kwenye hayo mengine sins neno, lakini kwa watoto wangu, nitaubeba msalaba wangu mwenyewe. Serikali itanikuta njiani kunisaidia na nitashukuru sana!
 
Umenena baab kila mtu apambane na elimu ya wanae, acha lialia waendelee kulialia tu wandae kizazi cha kutumwa
Mnaosubiri elimu bure hayo ndio matunda. Kuzaa, uzae wewe, kulea utegemee serikali. Mimi na kipato changu kidogo najitahidi sana kuwekeza kwenye elimu ya watoto wangu. Nanyi wengine, Aidha muungane na mimi au mkubali matokeo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanasiasa/Viongozi wa serikali ambao wanaongoza kutokana na chama chao cha siasa kushinda uchaguzi.

Hao ndio wanaoweka sera katika kufanya taifa liendelee kizazi mpaka kizazi.

Serikali iliyopo madarakani viongozi wengi watot wao wanasoma Feza kwa mfano watoto wa Magufuli,Mwigulu,Bagaile in short almost watoto wa viongozi wote wanasoma Feza. Siyo kitu kibaya.

Hapa inadhibitisha wanapenda shule nzuri. Ila cha kushangaza sera zao mbovu shule za serikali ambazo watoto wa wapiga kura wao ndo wanasoma ni majanga.

Jamani hizi shule naziita yatima maana hata maneno ya kuzielezea yananiisha. Mtajionea kwenye hizi picha. Gape ni kubwa.

Lakini shule nyingi za serikali siku hizinatoa Divion 1

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona msikitini hamna viti Wala madawati na shekh anaeleweka? Nenda udsm ukite darasa moja wako elfu miatano mwl nenda saut education darasa moja wako elfu tatu, tafuteni hoja za maana, sio kutuletea picha za akina lowasa
Je Sera na miongozo ya Elimu inataka chumba kimoja cha darasa kiwe na wanafunzi wangapi?
Kumbe miaka hii hadi vyuo vikuu kuna madarasa na yanatumia mwongozo wa primary na secondary!!
 
Huyu hapaswi kuwa mwalimu ana hasira.
[emoji3596][emoji3596][emoji3596]
tapatalk_1580186010846.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Atataja Ilboru, Mzumbe, n.k ambazo zina mchujo hatari, hata kidato cha tatu mwabafunzi asipofikisha wastani anarudishwa kwa DEO - kwenye sec. ya Kara yake.
siku hizi hamna cha mzumbe wala ilboru,hawa maharamia wa ccm wameshaua shule zote za umma ili shule zao zipate wateja
 
Nadhani ilikuwa kabla ya 2000? Huyo unayemzungumzia atakuwa ni Mungai tu, sidhani kuwa kuna mwingine.

Elimu yetu imevurugika sana, na matokeo yake yanaonekana dhahiri nyakati hizi.
ilikuwa baada ya 2000.sisi tuliosoma before 2000 tunajua vilaza walikuwa wakisoma private schools huku vipanga wakisoma shule za umma,vipanga sana tulisoma Mzumbe,Ilboru,Kirakara,msalato,Tabora boys na Girls
 
Kuna vipaumbele vya taifa na vipaumbele vya ccm,kuongeza ujinga miongoni wa wanyonge pamoja na wizi wa mali za umma ni sera za siri za ccm ili waendelee kutawala.
Halafu wanajinasibu km wao ni wazalendo tena wengine namba moja
 
Back
Top Bottom