Watoto wa wapiga kura wanakosoma VS Watoto wa wapigiwa kura wanakosoma

Watoto wa wapiga kura wanakosoma VS Watoto wa wapigiwa kura wanakosoma

Wanasiasa/Viongozi wa serikali ambao wanaongoza kutokana na chama chao cha siasa kushinda uchaguzi.

Hao ndio wanaoweka sera katika kufanya taifa liendelee kizazi mpaka kizazi.

Serikali iliyopo madarakani viongozi wengi watot wao wanasoma Feza kwa mfano watoto wa Magufuli,Mwigulu,Bagaile in short almost watoto wa viongozi wote wanasoma Feza. Siyo kitu kibaya.

Hapa inadhibitisha wanapenda shule nzuri. Ila cha kushangaza sera zao mbovu shule za serikali ambazo watoto wa wapiga kura wao ndo wanasoma ni majanga.

Jamani hizi shule naziita yatima maana hata maneno ya kuzielezea yananiisha. Mtajionea kwenye hizi picha. Gape ni kubwa.

Watakaokuelewa ni wachache sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mnaosubiri elimu bure hayo ndio matunda. Kuzaa, uzae wewe, kulea utegemee serikali. Mimi na kipato changu kidogo najitahidi sana kuwekeza kwenye elimu ya watoto wangu. Nanyi wengine, Aidha muungane na mimi au mkubali matokeo.
Yaleyale ya m/kiti wako na kauli zake kuhusu tetemeko Bukoba.
Wenye nchi yenu tambeni.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nigeria hio mkuu.

dodge
Safi sana, kuliko kukaa kwenye vumbi kwanini tusijenge viti na meza za matofali ni permanent, kuliko madawati yanayoharibika, na kulingana na idadi za watoto nafasi haitoshi kuweka viti na watu.
 
Sidhani Kada kama za Ualimu wanaweza kusomesha Watoto wao shule kama Feza.
 
Wanasiasa/Viongozi wa serikali ambao wanaongoza kutokana na chama chao cha siasa kushinda uchaguzi.

Hao ndio wanaoweka sera katika kufanya taifa liendelee kizazi mpaka kizazi.

Serikali iliyopo madarakani viongozi wengi watot wao wanasoma Feza kwa mfano watoto wa Magufuli,Mwigulu,Bagaile in short almost watoto wa viongozi wote wanasoma Feza. Siyo kitu kibaya.

Hapa inadhibitisha wanapenda shule nzuri. Ila cha kushangaza sera zao mbovu shule za serikali ambazo watoto wa wapiga kura wao ndo wanasoma ni majanga.

Jamani hizi shule naziita yatima maana hata maneno ya kuzielezea yananiisha. Mtajionea kwenye hizi picha. Gape ni kubwa.

Tibaigana!
 
Kunatofauti kati ya elimu bora inayopatikana kulipia na bora elimu inayotolewa bure na serikali ya Magufuli,Wanyonge wamechagua elimu bure,Magufuli ni rais na mtetezi wa wanyonge ila hajasema kwamba hata yeye ni mnyonge kiasi cha mwanae kusoma bure,kupanga ni kuchagua,wanyonge tumechagua bure so hata watoto wetu wakikaa mia tatu chumba kimoja as long as wanasoma bure hamna shida maana lazima wawepo watumikishwa na watumimisha
 
Tutembee kifua mbere....hao wa feza wanasoma kwa niaba ya watoto wetu !
Watakuja kuwaajiri na kuwatawala...BADO TUPO KWENYE FUNGATE LA UHURU... AMEEN
Daa nimejikuta ninacheka ila inahuzunisha sana.
 
Mbona msikitini hamna viti Wala madawati na shekh anaeleweka? Nenda udsm ukite darasa moja wako elfu miatano mwl nenda saut education darasa moja wako elfu tatu, tafuteni hoja za maana, sio kutuletea picha za akina lowasa
Mie nilidhani unasema University of Newcastle,au liverpool au Minnesota, etc kumbe unafanya reference kwenye hizo hizo wanazosoma watoto wa wanyonge,au wewe unadhani chuo lecture theater moja kuwa na student 1500 per session ni jambo la kawaida?Wanaccm Mungu awasaidie tu
 
Ndo nyinyi Mwl kajipinda kaamua kuagiza rimu moja japo watoto waje kufanya mitihani kila wiki Mwl asahihishe hayo majaribio kesho yake mnakuja hapa jf oooh walimu was shule mwembe mchachu wameagiza rimu jaman si tuliambiwa elimu bure hawa walimu wezi wanatuibia wanasiasa wakiskia kesho Mwl anapigwa bit utaskia marufuku kupokea rimu Mwl anasema hewala kiongozi wangu

Pepa inakuja ziro mia mbili wenzake wapo fedha shule inapiga division wani darasa zima

Mwl alietaman kuokoa mwanao anacheka anakwenda bank anakikanga ka posho kake

Keaho unarudi jf unasema walimu wa shule za serikali hawafaulishi kabisaaa
 
1580133814891.png

Kuna Jamaa mmoja alifuta michezo Mashuleni..akachanganya Chemistry&Physics...

Akafuta kilimo na ufugaji ...alifanya mambo ya ajabu ajabu sana miaka ya 2000s...
 
Una ubinafsi usiostahili. Mkulima asiye na hata kipato kidogo unachopata wewe afanye nini?

Wewe uliposoma hadi kufikia kwenye hicho kipato kidogo, wazazi wako pia walikuwa wabinafsi kiasi chako?

Sikuzongi kwa kuwa na msimamo wako huo wa kutaka wanao wapate elimu nzuri, lakini itakuwa jambo jema sana kama watoto wa wasiokuwa na uwezo kama wako nao wakapata fursa nzuri za kupata elimu.
Tatizo hapa sio uwezo wa kufanya hivyo kama taifa, ni uzembe tu wa watu wanaokabidhiwa majukumu haya ya kuhakikisha watoto wote wanapata fursa nzuri kwenye jambo mhimu kama hili la elimu.

Ni hawa "tunaowapigia kura" kama mada inavyosema, ndio kikwazo kikubwa katika jambo hili.
Una mlaumu bure tu.hadi miaka ya tisini hadi 2000 watu wote wenye akili walikuwa wanasoma shule za umma,na vilaza ndo walikuwa wakisoma private school,mimi pamoja na kuwa mtoto wa fukara nimesoma shule ya watoto wenye vipaji maalum ( special school) pale mzumbe from 1993 hadi 1999 na wazazi wangu pamoja na ufukara wao waliweza kumudu zile gharama,ila baada ya wanaccm kuona fursa ya kibiashara katika elimu,baada ya ccm kuanza kufikiria kukaa madarakani zaidi kuliko maendeleo ya nchi yetu,mkaamua kuanzisha shule zenu hizo za Feza,Badru Jonson,Savana,Imperial kisha mkaua shule za umma ambazo magufuli amekuja kuzizika kabisa kwa gia ya elimu bure,sasa kati ya huyo muhangaikaji na wanaccm nani mbinafsi?
 
Hao jamaa wasikuumize kichwa Jana walikuwa kwenye semina ya mnyika, Hivi hawajamsikia dogo wa gambajiga aliyepata wani ya point Saba?
Mmoja out of how many? wewe nae mjinga,yaani wanafaulu kumi out of 100 then unaenda unajipiga kifua?
 
Una mlaumu bure tu.hadi miaka ya tisini hadi 2000 watu wote wenye akili walikuwa wanasoma shule za umma,na vilaza ndo walikuwa wakisoma private school,mimi pamoja na kuwa mtoto wa fukara nimesoma shule ya watoto wenye vipaji maalum ( special school) pale mzumbe from 1993 hadi 1999 na wazazi wangu pamoja na ufukara wao waliweza kumudu zile gharama,ila baada ya wanaccm kuona fursa ya kibiashara katika elimu,baada ya ccm kuanza kufikiria kukaa madarakani zaidi kuliko maendeleo ya nchi yetu,mkaamua kuanzisha shule zenu hizo za Feza,Badru Jonson,Savana,Imperial kisha mkaua shule za umma ambazo magufuli amekuja kuzizika kabisa kwa gia ya elimu bure,sasa kati ya huyo muhangaikaji na wanaccm nani mbinafsi?
Mkuu sijijui, sidhani kweli kwamba wewe umesoma shule maalum Mzumbe kwa haya uliyoandika hapa juu kunijibu.

Kwanza umenisoma lakini hukuelewa nilichoandika; pili unaniweka mimi kuwa sehemu ya CCM na wala hata hayo niliyoandika sionyeshi mahali popote kuitetea CCM.

Kwa hiyo, hiyo elimu uliyopata huko kwenye shule maalum naona huitendei haki hata kidogo.

Ukitaka tujadili kwa kina hili swala la elimu ili ujue msimamo wangu juu ya jambo hili ninalojua wazi ndio msingi mkuu wa kila kitu kwa nchi yetu niko tayari sana, kwa sababu mjadala huo utakuwa ni kwa manufaa yetu sote, huenda na wengine pia.

Lakini kwa hapa ulivyoingia kichwa kichwa na kunijibu bila hata ya kuelewa nilichochangia, huitendei haki elimu unayosema umeipata wewe pamoja na kwamba wazazi wako hawakuwa katika hali ya kukupeleka kwenye hizo shule za wenye hela. Umekurupuka tu na kumwagika.

Kwa maoni yangu, wewe ndio ungekuwa mfano mzuri wa kutetea watoto ambao baba zao hawana uwezo wa kuwasomesha watoto katika hizi shule za wakubwa. Sasa sielewi msimamo wako huu hasa unatokana na nini.

Kwa kifupi, kama nilivyoeleza hapo mwanzo: elimu ni haki ya waTanzania wote bila kujali matabaka haya wanayotuwekea hawa waliopo madarakani. Hili ni jambo mhimu sana.

Kwa hiyo, tukikubaliana kwamba elimu ni haki ya kila raia wetu serikali inao wajibu wa kuhakikisha kwamba haki hiyo inapatikana kwa kila mtoto, bila kujali uwezo wa wazazi wake wa kumsomesha mtoto huyo.

Serikali inao wajibu wa kuhakikisha elimu inayotolewa inakidhi viwango na katika mazingira yatakayomwezesha mtoto aipate elimu hiyo vizuri; yaani pawe na miundombinu wezeshi na walimu wa kutosha kuitoa elimu hiyo.

Hii haina maana kwamba serikali ikataze hao wenye uwezo wao hata hao wakulima watakaotaka kujinyima kila kitu kuwahudumia watoto wao kuwapeleka huko kwenye hizo shule za wakubwa.

Jambo mhimu hapa ninalosisitiza, ni serikali ihakikishe elimu inayoisimamia katika shule zetu za umma zinazosomesha watoto wetu maskini itolewe kwa haki na kwa usawa na kwa viwango vinavyotakiwa. Hili ni jukumu la serikali ambayo tunaipa nyenzo zote za kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Sasa, kama utanisoma na kunielewa hapa kwa mawazo haya, na bado ukataka kuniwekea 'lebo' za uCCM au chama chochote cha siasa, nitasema wewe huna akili kichwani.

Samahani sana mkuu Sijijui kama hili litakuudhi, lakini sina njia nzuri zaidi ya hiyo ya kufikisha ujumbe wangu kwako.
 
Wanasiasa/Viongozi wa serikali ambao wanaongoza kutokana na chama chao cha siasa kushinda uchaguzi.

Hao ndio wanaoweka sera katika kufanya taifa liendelee kizazi mpaka kizazi.

Serikali iliyopo madarakani viongozi wengi watot wao wanasoma Feza kwa mfano watoto wa Magufuli,Mwigulu,Bagaile in short almost watoto wa viongozi wote wanasoma Feza. Siyo kitu kibaya.

Hapa inadhibitisha wanapenda shule nzuri. Ila cha kushangaza sera zao mbovu shule za serikali ambazo watoto wa wapiga kura wao ndo wanasoma ni majanga.

Jamani hizi shule naziita yatima maana hata maneno ya kuzielezea yananiisha. Mtajionea kwenye hizi picha. Gape ni kubwa.

Kundi la wajinga ndio uchagua viongozi.
 
Mbona msikitini hamna viti Wala madawati na shekh anaeleweka? Nenda udsm ukite darasa moja wako elfu miatano mwl nenda saut education darasa moja wako elfu tatu, tafuteni hoja za maana, sio kutuletea picha za akina lowasa
Chuo na msingi ni tofauti
 
Back
Top Bottom