Watoto wafundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery school

jiwe gizani

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2021
Posts
380
Reaction score
507
Wasalaam wakuu

Hivi ni kwanini watoto wetu wasifundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery?

Huu mfumo wa kuwafundisha kwa kiswahili mpaka la saba halafu waanze tena kufundishwa kwa kiingereza kuanzia form one ni mgumu mno

Mtoto akifundishwa kwa kiingereza tokea nursery school inamjenga anakuwa na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kiingereza vizuri tu.

Watoto wafundishwe kwa kiingereza toka nursery school, hicho kiswahili kama kina faida basi wafundishwe kwa kiswahili tokea nursery mpaka chuo.

Serikali inakwama wapi kubadili huu mfumo wa elimu?

Wanasemaga samaki mkunje angali mbichi

Au mnaonaje wananzengo?
 
Nilishajiuliza hili swala sana
Kuna faida gani ya kuanza na kiswahili alafu akifika form 1 anakutana na lugha ingine kabisa?
Na ndo mana unakuta form 4 wengi wanafeli ishu huku serikali tofauti na private,ishu sio tu walimu bali lugha ni mtihani
Unataka mtoto aandike essay aelezee kitu fulani,hiyo lugha ya kuandika hiyo essay amejifunza wapi wakati kwenye msingi amesoma kiswahili?
Elimu yetu ni kama ipo msukuleni vile😄
 
Elimu yetu ni kama ipo msukuleni vile[emoji1]
Ni kweli mkuu
 
Wasalaam wakuu

Hivi ni kwanini watoto wetu wasifundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery?

Huu mfumo wa kuwafundisha kwa kiswahili mpaka la saba halafu waanze tena kufundishwa kwa kiingereza kuanzia form one ni mgumu mno

Mtoto akifundishwa kwa kiingereza tokea nursery school inamjenga anakuwa na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kiingereza vizuri tu.

Watoto wafundishwe kwa kiingereza toka nursery school, hicho kiswahili kama kina faida basi wafundishwe kwa kiswahili tokea nursery mpaka chuo.

Wanasemaga samaki mkunje angali mbichi

Au mnaonaje wananzengo?
Angalia wazazi wanaosomesha watoto wao English medium schools kama wanatatizo hili. TAFUTA PESA TU
 
Ukitaka mtoto aongee na kuelewa kiingereza vizuri kwa mazingira ya elimu ya Sasa mpaka uwe na pesa,bila hivyo mtoto ataishia kuwa na umahiri wa kujibu maswali na siyo kuongea kimombo...
Sio tu pesa,hata nyumbani kama mnaongea kiingereza mtoto anaweza kucatch up,mie nimesoma kayumba ila mzungu hanitoi jasho,bibi alihusika sana home kunikomalia kila nikitoka shule
Alikua ananikazania na story books na kunisemesha mpaka tukaanza kuelewana
 
Mkuu swala la kutafuta pesa ni Jambo jingine,unaweza tafuta pesa ukapata Ila isiweze kusomesha watoto wako tokea nursery shule za English medium

Fikiria Mara mbili mbili unapo changia mada

Utakuwa hujaelewa maana ya kutafuta fedha, sio kutafuta tu.... tafuta na uzipate.
 
Sio tu pesa,hata nyumbani kama mnaongea kiingereza mtoto anaweza kucatch up,mie nimesoma kayumba ila mzungu hanitoi jasho,bibi alihusika sana home kunikomalia kila nikitoka shule
Alikua ananikazania na story books na kunisemesha mpaka tukaanza kuelewana
Jamii zetu zinajulikana zilivyo,hilo ulilosema ni mtu mmoja Kati ya watu mia ndo hufanya hivo, ni familia chache tu ndo zinazoelewa hilo,familia nyingi tena hizo hizo za wasomi hakuna kitu wanafanya Cha maana ili kumsaidia mtoto Kila kitu anaachiwa mwalimu afanye...
 
Mkuu uchumi wa watz ni mdogo Sana hizo ajira zenyewe ziko wapi za kutufanya tuwe na pesa za kuwapeleka watoto wetu English medium?

Mkuu mimi nilikuwa nakupa mwongozo pale tu uliposema, "unaweza kutafuta pesa ukapata ila usiweze kusomesha watoto kutoka nursery".

Hivyo basi, nilijikita kwa yule aliyetafuta na kuzipata.... huko kwa fukara sina cha kusaidia ila usimfariji mwambie tu ukweli kuwa pesa ni muhimu.
 
Mkuu namaanisha unaweza pata pesa ya kukidhi mahitaji mengine tu na sio ya kuwasomesha watoto toka nursery shule za English medium
 
Elimu yetu inahitaji maboresho sana, lugha ikiwa ni moja wapo....English inakuja kuwa lugha ngeni kwa mwanafunzi kujifunza na kuiweza kuimudu , aongee na aandike English iliyonyooka sio kazi rahisi ilitakiwa aanze tangu nursery.

Kuna mwanafunzi wa form four nilikua nampa a,b,c za kusoma kwa ajili ya practical, nikamuelekeza akasome baadhi ya specimen kama maize seed and bean seed ambazo tayari walikua washafundishwa, baada ya dakika akarudi kuniuliza kati ya maize na beans ipi ni maharage...
Sijajua bado huyu shida ni lugha tu au kuna mengine.
 
Nilishajiuliza hili swala sana
Kuna faida gani ya kuanza na kiswahili alafu akifika form 1 anakutana na lugha ingine kabisa?
Na ndo mana unakuta form 4 wengi wanafeli ishu huku serikali tofauti na private,ishu sio tu walimu bali lugha ni mtihani
Unataka mtoto aandike essay aelezee kitu fulani,hiyo lugha ya kuandika hiyo essay amejifunza wapi wakati kwenye msingi amesoma kiswahili?
Elimu yetu ni kama ipo msukuleni vile[emoji1]
Sijui tunakwama wapi aiseeh, na issue sio kwamba hawajui au hawaelewi kilichosahihi kufanyika laah asha wanajua kila kitu sema tuu hawataki
 
Back
Top Bottom