Tangantika
JF-Expert Member
- Aug 12, 2018
- 5,586
- 7,087
Mbeya mfano kuna Benhamini mkapa , Nuru nyingine moja nimeisahau.Hizo shule za serikali zinazofundisha kwa kingereza ni zipi mkuu?
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mbeya mfano kuna Benhamini mkapa , Nuru nyingine moja nimeisahau.Hizo shule za serikali zinazofundisha kwa kingereza ni zipi mkuu?
Ni kweli b inategemea nyumbani man mazingira gani.Sio tu pesa,hata nyumbani kama mnaongea kiingereza mtoto anaweza kucatch up,mie nimesoma kayumba ila mzungu hanitoi jasho,bibi alihusika sana home kunikomalia kila nikitoka shule
Alikua ananikazania na story books na kunisemesha mpaka tukaanza kuelewana
Hapo ni wazi kuwa tatizo ni lugha.Elimu yetu inahitaji maboresho sana, lugha ikiwa ni moja wapo....English inakuja kuwa lugha ngeni kwa mwanafunzi kujifunza na kuiweza kuimudu , aongee na aandike English iliyonyooka sio kazi rahisi ilitakiwa aanze tangu nursery.
Kuna mwanafunzi wa form four nilikua nampa a,b,c za kusoma kwa ajili ya practical, nikamuelekeza akasome baadhi ya specimen kama maize seed and bean seed ambazo tayari walikua washafundishwa, baada ya dakika akarudi kuniuliza kati ya maize na beans ipi ni maharage...
Sijajua bado huyu shida ni lugha tu au kuna mengine.
Ving'amuzi/Visimbuzi/Vising'ombe 🙂 au viite vyovyote upendavyo, siku hizi vipo hata kwenye kaya tajiri mpaka maskini. Siyo tena kipimo cha "ushua" kama ilivyokuwa zamani. Amri hiyo ya kupiga marufuku vipindi vya Kiswahili, hasa kwa mtoto anapokuwa na umri wa miaka sufuri (0) mpaka mitatu (3); na miaka mitatu (3) mpaka sita (6), huweza kumfanya mtoto kujifunza mwenyewe Kiingereza kwa mtindo wa uzamiaji ("immersion"). Shuhuda ziko nyingi Uswazi na vijijini watoto ghafla wanaanza kutema ung'eng'e kutokana na kuangalia katuni tu za Kiingereza.Hadi TV ilikua marufuku kuangalia vipindi vya kiswahili
Kumbe hujui asilimia kubwa ya watoa maamuzi shule za English medium ndiyo biashara zao, sasa wakibadili mfumo si watakosa wateja? Ninachokiona hapa ni ubinafsi uliopitiliza wakati wenyewe watoto wao wanawapeleka nje ya nchi kusoma.Sijui tunakwama wapi aiseeh, na issue sio kwamba hawajui au hawaelewi kilichosahihi kufanyika laah asha wanajua kila kitu sema tuu hawataki
Woow😍Hili ndio wengi hawajui. Mm mwenyewe nimejua kimombo sababu nyumbani wazazi walikua hawaongei kiswahili. Ukiongea kiswahili hakujibu chochote na yeye anakutuma kwa kimombo. Japo nilisoma kayumba. Hadi TV ilikua marufuku kuangalia vipindi vya kiswahili, hadi leo mm huwezi ukanikuta nafatilia vipindi au habari za kiswahili
Huo ung'eng'e anaoutema mtoto baada ya kuangalia katuni anaelewa maana yake? au anadaka tu yes..no...yes.....hapo atakariri baadhi ya maneno tuu halafu kuyaandika kwa usahihi atajuaje?Ving'amuzi/Visimbuzi/Vising'ombe 🙂 au viite vyovyote upendavyo, siku hizi vipo hata kwenye kaya tajiri mpaka maskini. Siyo tena kipimo cha "ushua" kama ilivyokuwa zamani. Amri hiyo ya kupiga marufuku vipindi vya Kiswahili, hasa kwa mtoto anapokuwa na umri wa miaka sufuri (0) mpaka mitatu (3); na miaka mitatu (3) mpaka sita (6), huweza kumfanya mtoto kujifunza mwenyewe Kiingereza kwa mtindo wa uzamiaji ("immersion"). Shuhuda ziko nyingi Uswazi na vijijini watoto ghafla wanaanza kutema ung'eng'e kutokana na kuangalia katuni tu za Kiingereza.
Kwani Kiswahili nani aliwafundisha? Njia hiyohiyo hapo juu ya uzamiaji ndiyo ilitumika kumfanya mtoto ajue Kiswahili: kwa kusikia Kiswahili kila mahali.
Maria Montessori kaelezea hili KWA KIREFU.
Msome Maria Montessori hapo kwenye kiambatisho.Huo ung'eng'e anaoutema mtoto baada ya kuangalia katuni anaelewa maana yake? au anadaka tu yes..no...yes.....hapo atakariri baadhi ya maneno tuu halafu kuyaandika kwa usahihi atajuaje?
Sijui kingereza Mimi mkuu [emoji3]Msome Maria Montessori hapo kwenye kiambatisho.
Sijui kingereza Mimi mkuu [emoji3]
Poa poaKingereza kililetwa na meli mkuu.
Kwa Kiswahili, kitabu kinaitwa: AKILI YA SPONJI. Kwenye hicho kitabu Montessori anasema akili ya mtoto husharabu elimu na maarifa (ikiwemo lugha) kama vile sponji linavyofyonza maji.
Endelea kukisoma kitabu hicho HAPA kwa Kiswahili cha kutafsiriwa na kompyuta.
Kwa lugha myepesi unataka shule zote za msingi za serikali ziwe English mediaWasalaam wakuu
Hivi ni kwanini watoto wetu wasifundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery?
Huu mfumo wa kuwafundisha kwa kiswahili mpaka la saba halafu waanze tena kufundishwa kwa kiingereza kuanzia form one ni mgumu mno
Mtoto akifundishwa kwa kiingereza tokea nursery school inamjenga anakuwa na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kiingereza vizuri tu.
Watoto wafundishwe kwa kiingereza toka nursery school, hicho kiswahili kama kina faida basi wafundishwe kwa kiswahili tokea nursery mpaka chuo.
Serikali inakwama wapi kubadili huu mfumo wa elimu?
Wanasemaga samaki mkunje angali mbichi
Au mnaonaje wananzengo?
Uzalendo wa nini?Uzalendo kwanza...
Kushikilia, kusimamia na kutetea kile kinachohusu nchi yako kwa misimamo yote...Uzalendo wa nini?
Sawa basi lugha ya kufundishia isibadilike toka nursery kama ni kiswahili kitumike mpaka chuo huko Kama ndo huo uzalendo unaoutaka weweKushikilia, kusimamia na kutetea kile kinachohusu nchi yako kwa misimamo yote...
kiwe kibaya au kizuri...
Mmmh sidhani, alinifikirisha sana japo sikumuonesha chochote nikamjibu tu beans ndio maharage....Hapo ni wazi kuwa tatizo ni lugha.
[emoji122][emoji122]Suala siyo la kusomesha watoto English Media schools Bali ni wizara ipeleke mswada bungeni wa kubadili lugha ya kufundishia kwa ngazi zote za elimu!
Kiingereza ni lugha ya dunia nzima kwa Sasa na ndio lugha kuu ya teknolojia ambayo ndiyo inayotawala uchumi wa dunia. Kama nchi tusijidanganye na kiswahili chetu kwani tutaendelea kuwa maskini daima dumu! Chungulia hapo Kenya na Uganda ambao wanaotumia kiingereza kufundishia ngazi zote huku wakiongea kiswahili fasaha kushinda hata sisi!
Tunaking'ang'ania kiswahili ili iweje ilihali kwasasa ni mother tongue kwa watoto wetu wengi? Waziri abadili hii kitu haraka kama kweli tuna lengo la kuingia na kubaki uchumi wa Kati!
Pia ulifanya vizuri kumueleweshaMmmh sidhani, alinifikirisha sana japo sikumuonesha chochote nikamjibu tu beans ndio maharage....