Watoto wafundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery school

Watoto wafundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery school

Watoto wanatakiwa wafundishwe Kiswahili toka vidudu mpaka phd. Watu wengi wanafeli sio kwasababu vilaza ila lugha ya Kiingereza inawavuruga
 
Kazi kweli kweli
vevotz_162433944430492.jpg
 
Tulipoanza form one tulikuwa tunaona kama mauzauza. jumlisha sasa plus. Term ya kwanza ilikuwa ngumu angalau term ya pili tuli catch up. Kwa kweli hili jambo tumeongea sana huku lakini kama vile wahusika wanafunga masikio. Wote wakubwa watoto wao wako International school.
 
Wasalaam wakuu

Hivi ni kwanini watoto wetu wasifundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery?

Huu mfumo wa kuwafundisha kwa kiswahili mpaka la saba halafu waanze tena kufundishwa kwa kiingereza kuanzia form one ni mgumu mno

Mtoto akifundishwa kwa kiingereza tokea nursery school inamjenga anakuwa na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kiingereza vizuri tu.

Watoto wafundishwe kwa kiingereza toka nursery school, hicho kiswahili kama kina faida basi wafundishwe kwa kiswahili tokea nursery mpaka chuo.

Serikali inakwama wapi kubadili huu mfumo wa elimu?

Wanasemaga samaki mkunje angali mbichi

Au mnaonaje wananzengo?
Sijui kama watakuelewa, lakini ni hoja nzuri, itamjengea mwanafunzi msingi wa lugha hiyo ambayo ndio itumikayo kwa masomo. Matokeo mabaya ya mitihani(mbali na kupanua magoli) tatizo ni lugha na si ugumu wa masomo.
 
Ukitaka mtoto aongee na kuelewa kiingereza vizuri kwa mazingira ya elimu ya Sasa mpaka uwe na pesa,bila hivyo mtoto ataishia kuwa na umahiri wa kujibu maswali na siyo kuongea kimombo...
Umahili wa kujibu maswali nacho kwa sasa si kipimo cha uelewa. Maswali mengi majibu ni ya kujaza vibox, hata mjinga awezae bahatisha.
 
Mkuu swala la kutafuta pesa ni Jambo jingine,unaweza tafuta pesa ukapata Ila isiweze kusomesha watoto wako tokea nursery shule za English medium

Fikiria Mara mbili mbili unapo changia mada
Kama haitaweza, tafuta tena. Kusomesha elimu bora ni gharama.
 
Mkuu labda unamaanisha kiasi gani Cha pesa?
Pesa ya kutosha, elimu nzuri ni gharama. English medium primary, day, kwa mwaka gharama ya chini kabisa nchini ni kuanzia 1m. Boarding ni kuanzia 2m.
 
Pointi ovu coreksheni mkuu

Mimi nawaza wafundishwe kiswahili kuanzia chekechea mpaka chuo kikuu, kiingereza liwe somo la kawaida, mwanafunzi anaelewa sana akifundishwa kwa lugha anayoifahamu vizuri (maza tongu au neshono langueji) ukimfundisha kwa lugha ya kigeni kama ilivo sasa anakua na kazi tatu; kuskiliza, kutafsiri kwenda kwenye maza tangi au neshona langueji alafu ndo aelewe ndo kinachowapata wanafunzi wa sekondari zetu na vyuo

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
Mkuu swala la kutafuta pesa ni Jambo jingine,unaweza tafuta pesa ukapata Ila isiweze kusomesha watoto wako tokea nursery shule za English medium

Fikiria Mara mbili mbili unapo changia mada
Mkuu kama pesa unayo je utashindwa nini kumpeleka kwenye shule nzuri?
 
Wasalaam wakuu

Hivi ni kwanini watoto wetu wasifundishwe masomo kwa kiingereza toka wanapoanza nursery?

Huu mfumo wa kuwafundisha kwa kiswahili mpaka la saba halafu waanze tena kufundishwa kwa kiingereza kuanzia form one ni mgumu mno

Mtoto akifundishwa kwa kiingereza tokea nursery school inamjenga anakuwa na uwezo mkubwa wa kuongea na kuandika kiingereza vizuri tu.

Watoto wafundishwe kwa kiingereza toka nursery school, hicho kiswahili kama kina faida basi wafundishwe kwa kiswahili tokea nursery mpaka chuo.

Serikali inakwama wapi kubadili huu mfumo wa elimu?

Wanasemaga samaki mkunje angali mbichi

Au mnaonaje wananzengo?
mhn! watoto wanaelewa vizuri wakiwa wanafundishwa kwa lugha za mama zao! hata hivyo elimu si lazima kiingereza pekee yapo mambo mengine zaidi ya lugha ambayo mwanafunzi anahitaji kujifunza.
 
Nilishajiuliza hili swala sana
Kuna faida gani ya kuanza na kiswahili alafu akifika form 1 anakutana na lugha ingine kabisa?
Na ndo mana unakuta form 4 wengi wanafeli ishu huku serikali tofauti na private,ishu sio tu walimu bali lugha ni mtihani
Unataka mtoto aandike essay aelezee kitu fulani,hiyo lugha ya kuandika hiyo essay amejifunza wapi wakati kwenye msingi amesoma kiswahili?
Elimu yetu ni kama ipo msukuleni vile[emoji1]
Na kuhusu lugha hasa ya kuzungumza na kujieleza inapatikana primary (English) misingi yote ipo umo.
 
Na kuhusu lugha hasa ya kuzungumza na kujieleza inapatikana primary (English) misingi yote ipo umo.
Yes! wataalam wanakwambia lugha mtoto anafundishwa na kuimaster miaka 7 ya mwanzoni toka azaliwe,
 
Back
Top Bottom