Watoto, vitoto, mijitu au vinyamkera ni majina ambayo munabandika wale hamukabaliani nao. La muhimu ni hili JF ni ya sisi zote, ni vyema mutangulie kukubali hayo.
Ningependa Kuuliza hivi, Ukimkuta baba muzazi amelala sebuleni uchi, utafanya nini?
Bila shaka najua utasema utatafuta cha kumfunika. Hapa Chit chat ni kama sitting room, watu wote wako hapa, vijibabu, watoto, mabibi na wengine. Naomba wale munajisikia eti JF ni yenu,eti hewa mumechafuliwa....mujadala bora una msingi na siyo ovyo, changia, lete maoni yako sio kuwa tusi wenye haukubaliani nao.
Nimemukuta baba uchi nikamfunika baba bado anateta sanaaaaaaaa.
kama ningemkuta baba uchi kwenye bedroom ninge ondoka humo haraka sana. Wengi ambawo wanashambulia na kushangilia matusi kwa wengine hapa uki angalia kwa undani utakuta ni wale wale unaowapata kwa jukwa la mapenzi na mahusiano.Wenyeji yaaani. Jameni huko ndo bedroom yenu, uchi wenu huko hatujali na hatutajaribu kuwafunika.
Maana mutu akiingia humo ako tayari kutongoza au kutongozwa, kugegeda na mengine yenye hamuna haja ya kutaja.Nyinyi ambawo ni wenyeji wa jukwa hilo,tafathadhali hapa chit chat ni pa wote , bedroom yenu ni huko mukitaka kwenda tanga, ""hapa tulienda bar", party za chupi nyeupe na kwingineko muendeleze maneno yenu ni sawa kabisa, bora tuu mutupe nafasi kuchangia hapa, ni haki yetu, sio kuchafua hewa. Humo unakuta Vijibabu, mabibi na mabinti ambawo wanakaa kupotea, lakini hiyo ndo raha yao na hiyo ni haki yao. However a country must have a conscience!!!!. Mimi nikimkuta babu anajivinjari na binti umri wangu sio vyema...lakini wacha ni waachie hayo hapo.
Lengo langu la kuandika hapa ni kwa wale wanajisikia JF ni yao. Naomba tafathali JF siyo yenu,bora tumejiunga tuna haki ya kuchangia mada yeyote bora tufanye hivo kwa heshima, bila matusi. Nikisema hivo sio kumaanisha nauunga mkono mwenye alianzisha ile mada ambaye imezua utata lakini, I may not agree with what you say, but as sure as hell i will defend you right to say so!! Na kama una maoni tofauti na yangu, tujadiliane hapa kwa njia ya heshima!!!!