Watoto wako walibadilisha vipi maisha Yako...!

Watoto wako walibadilisha vipi maisha Yako...!

Mtoto wangu wa kwanza nampata baada ya wiki 2 kumaliza mtihani wa form 6, nilitia ujauzito wakati nipo A level, ukweli usiopingika mimba ile ilinifanya nikaharibu form 6, palikuwa hapasomeki, shule hapaendeki, mpaka mwl. Wangu wa fizikia ananitafita baada ya kuona nimekuwa mtoro sana, alinioenda sababu form 5 nilikuwa napasua saa physics, alikuwa ananitegemea, ila baada ya ile mimba shule ikaanza kulegalega(hapo katikati kuna mengi)

Mtoto akazaliwa, matokeo yakatoka nina 4, siwezi kwenda chuo, bimkubwa akaniweka chini, akielewa yaliyotokea, habari za mimba alikuja kuzipata mimba tayari ina miezi kama 7-8 hivi(too late, hili suala la kuficha ukweli ndio liliniponza na shule)
Bimkubwa akataka niende chuo(diploma) akanikabidhi na ada kabisa, baada ya kufikiri kwa kina nikaghairi kwenda chuo, nikarudi kwa bimkubwa nikamueleza uhalisia tayari nina mtoto ninapaswa kusimama kama baba, hivyo siwezi kwenda chuo, hii pesa ya ada naifanyia biashara kisha nikikaa sawa nitajisomesha, hiyo sababu ya kwanza ambayo nilimueleza, ya pili ilikuwa moyoni, haina nguvu kama ya kwanza lakini pia nilikuwa najisikia kauvivu kuanza diploma, wakati wenzangu wapo degree, lakini kibaya zaidi wale ambao nilimaliza nao la 7 wako mwaka wa pili, sababu mie form 1 nilisoma mara 2, ya kwanza nilimpiga mwalimu wakanitimua, nikaenda kuamza upya, hivyo wale wenzangi wanakuwa mwaka wa 2 na ndio kwanza diploma.

Bimkubwa akakubali kishingo upande, nikaanza biashara, home kulikuwa na tv hizi, nikapata Playstation 2, lakini pia kuna banda nilinunua kipindi nipo A level kwa ajili ya kufungua saluni(A level nilikuwa nasoma huku napiga mishe mishe hasa za udalali wa simu na deals nyingine halali) kibanda kile nikaghairi, nikamkodisha muuza chips, nikawa nakunja elfu 6 yangu daily, na zile ps2, nikawa navuta sh 10 mpaka 20, kinachoingia naangalia mtoto na kingime nahifadhi, nikanunua pikipiki ya kwana, ya pili, nikarudi chuo hapa yakaanza maseke pikipiki ikaibiwa, Playstation wakaja askari kuzibeba, nikaenda kuwaletea noma na ujeuri wangu, nikazipata nikauza.. Nikanunua pikipiki used kama 2 hivi na ile ya zamani zikawa 3, maderwva kwa kuwa nipo chuo, hela hawapeleki, service hawafanyi, nikaja nikayauza kwa hasara.

Kuhusu ulezi mwanangu nilimchukua akiwa na miaka mi3-4 hivi nikaishi nae, akaja akaanza la kwanza, mpaka la 3 ndio mimi nikaoa mwanamke mwingine, sikumuoa mzazi mwenzangu, sababu niliona ana akili za kushikiwa toka mwanzo niligundua mama yake mzazi ni mpenda hela hivyo mie alikuwa hanikubali, niliamua kumuoa sababu tu kwao alikuwa akinyanyasika kisa kazalia home, niliamua nimpe heshima, aheshimike.
Ila alijitela nahisi maneno ya mama yake yalimuingia, wakati nataka kwenda kumalizia mahari, akaanza ooh, sijui tutafute maisha kwanza, kimeenda kimerudi, kumbuka hapo nilishatanguliza kama laki 7 hivi katika mahari ya milioni 2, nikampa kauli moja unataka ndoa ni sasa, hutaki basi sahau kuolewa na mimi, nikamuuliza "TUTAFUTE MAISHA KWANZA, TULIYAPOTEZEA WAPI"

hapo nikafunga file lake mpaka nilipokuja kuoa mke wangu huyu wa sasa.
Nimelea mwanangu kwa mapenzi mpaka anafika la 3, mama yake anakuja kumchukua ampeleke shule, kenge yule toka kamchukua mtoto, hajataka kumleta kwangu likizo yoyote ile, kila nikimtaka mtoto ni sababu tu, mpaka hivi sasa kaingi darasa la 6, na inaonesha anamjaza sumu mtoto kuhusu mimi baba yake, alishambadili ma dini, akaulizwa kwanini umefanya hivyo eti baba yake alinikataa 😂 na katika watoto wangu woote, huyu ndio alinikaa kumoyo kutokana na stori yake ndefu, ila huyu mwanamke anafanya kila kitu kiwe kichungu kwangu.
Nilipofikia nimeweka mikono juu, mtoto akipokea sumu za mama yake sawa, akiwa mdadisi akasimuliwa na watu wema kwao juu ya mazuri na upendo wangu kwake na akaijua thamni ya mdingi wake sawa pia.


Khabari ni ndefu sana, ila kwa leo inatosha.
Pole Mungu ni mwema mtoto anakua itafika wakat atajua ukweli ni upi na uongo ni upi
 
Mwanangu wa pili, alinifanya niwaheshimu zaidi wanawake, akiwa kichanga hakumtaka mama ake, dada wa kazi wala mtu mwingine zaidi yangu.

Kanipigisha sana mikesha, hadi nikajua kua wanawake wanajukum gumu sana la ulezi hivo wanahitaji heshima ya pekee.
Hahah km nakuona mkuu 😄😄😄 ilivokuwa unazunguka kubembeleza
 
Pole Mungu ni mwema mtoto anakua itafika wakat atajua ukweli ni upi na uongo ni upi
Namuombea kwa mungu apate kujua ukweli, ila nae akikuwa na akili akameza sumu za mama yake kuwa baba mbaya, shauri yake.

Mungu anajua dhamira na upendo mkubwa nilionao moyoni mwangu juu yake
 
ERoni
Ushimen
Grahams
binti kiziwi
Kalpana
Liverpool VPN 😄mje mtupe experience zenu baada ya kupata watoto
Kweli nimezidi kuzeeka Babu yenu, yaani kuniita kote kule nilikuwa sijasikia 😜

Turudi kwenye mada,

Ujio wa watoto wetu na Bibi yenu ulininibadirisha baadhi ya mambo hususani mtazamo juu ya maisha Kwa ujumla

Kila nikifanyacho nimekuwa nikifanya huku nawafikiria wao zaidi

Nipo radhi nisile, ila wao na Mama yao nahakikisha wamekula kwanza

Nikipata shilingi laki 1, basi nitahakikisha elfu 80 imeenda kwao na shilingi elfu 20 ndiyo nabaki nayo Mimi

Nimejikuta nafanya Uwekezaji mwingi hasa kiuchumi Kwa kujinyima kwaajili ya kuwaandalia wao kesho yao

Naweza kukaa miezi 6 bila kununua shati jipya ili niwanunulie wao
 
Sijui ni kwa nini, yani kuna Me hata kumshika mtoto dk2 hawezi. Labda ni tumeumbwa tofauti.
Huwezi kujua ila yakikukita utajua! Kama mwanaume anapenda sana K, na hana mchepuko, raha yake aioge K. Ujio wa mtoto unaweka limit ya kupata K. Hapo ndipo mtanziko unapotokea. Hivi unajua mwanamke akikunyima k hata ndugu zake, nguo zake etc unavichukia! Ndiyo maana tunasema, michepuko inaokoa ndoa.
 
Huwezi kujua ila yakikukita utajua! Kama mwanaume anapenda sana K, na hana mchepuko, raha yake aioge K. Ujio wa mtoto unaweka limit ya kupata K. Hapo ndipo mtanziko unapotokea. Hivi unajua mwanamke akikunyima k hata ndugu zake, nguo zake etc unavichukia! Ndiyo maana tunasema, michepuko inaokoa ndoa.
Mwanamke akishika ujauzito had akiifungua Huwa na mabadiliko mengi kihisia sabbu ya madadiliko ya homoni mwanaume mjinga pekee ndo atafanya hiyo ni sabbu ya kuchukia mtoto
 
Huwezi kujua ila yakikukita utajua! Kama mwanaume anapenda sana K, na hana mchepuko, raha yake aioge K. Ujio wa mtoto unaweka limit ya kupata K. Hapo ndipo mtanziko unapotokea. Hivi unajua mwanamke akikunyima k hata ndugu zake, nguo zake etc unavichukia! Ndiyo maana tunasema, michepuko inaokoa ndoa.
Haiwezi kuwa sababu ya kutopenda kukaa/kumshika mtoto. Hayo ni mambo mengine tofauti kabisa.

Kwamba kwa vile wife anakunyima K unakuwa na hasira hadi hutaki mtoto?
 
Mwanamke akishika ujauzito had akiifungua Huwa na mabadiliko mengi kihisia sabbu ya madadiliko ya homoni mwanaume mjinga pekee ndo atafanya hiyo ni sabbu ya kuchukia mtoto
Huwezi kubadili kila nafsi ya mtu. Tupo hapa kuelimisha na kuelimisha ni pamoja na kujua chimbuko la tatizo. Mabadiliko ya mwanamke si wakati wa mimba hata kulea kunaleta mabadiliko pia.
 
Haiwezi kuwa sababu ya kutopenda kukaa/kumshika mtoto. Hayo ni mambo mengine tofauti kabisa.

Kwamba kwa vile wife anakunyima K unakuwa na hasira hadi hutaki mtoto?
Ndiyo maana unakuta wanaume wengine wajinga wanaua watoto wa kambo. Roma na Snura waliimba K ni K. Achana na nguvu ya K wakati Abdallah amechachamaa hasa kwenu vijana.
 
Back
Top Bottom