😂Daah!! Umenikumbusha habari za kuambiwa " mama kanunua mtoto".
Binafsi sio mama lakini watoto wa ndugu zangu nimelea Lea ( yaani kukaa nao kwa muda kadhaa).
Katika kukaa nao nikagundua kumbe ulezi sio tu kuwapikia watoto, kuwafulia kama ambavyo nilikuwa nafikiriaga, kumbe ulezi unaenda mbali zaidi Hadi katika uchunguzi wa kitabia wa watoto. Lazima mzazi uwe mchunguzi wa tabia za watoto wako, ufatilie mienendo Yao ya Kila siku, kuanzia marafiki zake shuleni, Mtaani n.k.
Mpe mtoto nafasi ya kujieleza na kupima mambo, weka meza ya majadiliano nae / nao, pima uwezo wao wa kufikiri, isiwe ni amri tu kuanzia asubuhi Hadi jioni.
Kwahiyo nimejifunza baadhi ya mambo kutokana na kukaa nao kwa hizo nyakati.
Sio mpigaji wa watoto Kabsaa ila wakiniboa ntawafokea hataree!! Hilo najitahidi nibadilishe ili nikijaaliwa wakwangu nisifoke sanaa.