Watoto wakutwa wakisafiri chini ya basi kutoka Bukoba - Mwanza

Watoto wakutwa wakisafiri chini ya basi kutoka Bukoba - Mwanza

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Pichani watoto hawa wamekutwa wakisafiri uvunguni mwa basi la Happy Nation Bukoba - Mwanza:

Screenshot_20230207-214432.jpg

Hadi wanafumwa huko chini walikuwa wameshamaliza angalau kilometers 200.

Hawa ndiyo ile sampuli ya watoto wa wakulima tunaotaka kuaminishana kwa nguvu kuwa wazazi wao sasa wanaouza chakula nje. Kwamba kwa sababu hiyo hawana shida ya chakula ila mijini."

Hii ndiyo Tanzania ambayo viongozi wake wako busy wanatumbua na wengine kupora pesa bila ya aibu kupeleka China huku chawa wakikenua.

======
Watoto sita wenye umri kati ya miaka 12 na 16 wamekamatwa na Jeshi la polisi mkoani Geita wakisafiri wakiwa chini ya basi kutoka mjini Bukoba mkoa wa Kagera kwenda jijini Mwanza, jambo ambalo ni hatari kwa maisha yao.

Watoto hao wanaodai kuishi kwenye kituo cha mabasi Bukoba wamedai walilazimika kusafiri wakiwa chini ya gari ili waweze kufika Mwanza ambako wanadhani kuna unafuu wa maisha ikilinganishwa na Bukoba.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti leo Februari 7, 2023 wakiwa kituo cha polisi Geita wamedai kwamba waliingia kwenye basi la Happy Nation saa 9 usiku na kujificha kwenye “chassis” ya gari hadi asubuhi lilipoanza safari ya kwenda Mwanza.

“Kuna mwenzetu alisema yeye aliwahi kupanda chini ya gari kutoka Bukoba hadi Mwanza na hakupata shida akatuambia maisha ya huko ni mazuri ndio maana tulikubali kwenda lakini tulipofika hapa tukakamatwa na polisi wakatuleta kituoni,” amesema mmoja wa watoto hao.

Amesema alilazimika kuishi mtaani baada ya mama yake kufariki na bibi anaewalea ni mzee asiye na uwezo, hivyo kulazimika kutafuta pesa ili aweze kumtunza bibi na mdogo wake.

Watoto sita wakamatwa wakisafirichini ya uvungu wa basi la Bukoba-Mwanza
Mtoto mwingine (16) amesema aliacha shule baada ya kufeli mtihani wa darasa la nne. Amedai kwamba hana wazazi na amekuwa akiishi na shangazi yake lakini alipigwa na mjomba wake na kuamua kutoroka na kuishi mtaani.

“Kwenye gari chini kuna chuma mbili moja inachemka nyingine haichemki, hiyo moja ndio tunabebana huko chini kuna vumbi tuu kukiwa na mvua na upepo huumii lakini kukiwa na vumbi unaweza kugongwa hata na jiwe. Mimi nimeshapanda tena kutoka Bukoba hadi Mwanza,” amesema mtoto huyo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Geita, Safia Jongo amethibitisha kukamatwa kwa watoto hao na kusema watoto hao wamebainika kuishi mtaani huku wengine wakilelewa kwenye kituo cha watoto cha Hekima kilichopo Bukoba.

Jongo amesema watoto hao wamekosa malezi ya wazazi na wengine kutelekezwa na familia baada ya wazazi wao kufa na kwamba watoto hao wanatunzwa ili taratibu za kiustawi wa jamii zikamilike na kuwa wazazi wa watoto hao watachukuliwa hatua kwa mujibu wa sheria kwa kushindwa kuwa
 
Hawa ni makomandoo! Serikali inasubiri nini isiwapokee kwenye Jeshi la Wananchi na kuwapa mafunzo zaidi? Mtu unasafiri kilometer 200 chini ya basi linakwenda 120km/h umejishika na springi utashindwa nini vitani?
 
Hii ni aibu kwa taifa na ushahidi kuwa, kama taifa, tuna kazi kubwa kuwaondoa watu wetu kwenye umaskini wa kutengenezwa. Shame on us as a nation. Iko wapi asali nao warambe?

Kama taifa tuna rundo la wasiojitambua kutoka juu hata chini. Hata hili usishangae kuona chawa wakilihalalisha.
 
Hawa ni makomandoo! Serikali inasubiri nini isiwapokee kwenye Jeshi la Wananchi na kuwapa mafunzo zaidi? Mtu unasafiri kilometer 200 chini ya basi linakwenda 120km/h umejishika na springi utashindwa nini vitani?
Marekani ilifanya jaribio ikachukua watu wenye roho ngumu wenye kesi nzito ikawapa training ya kutegua mabomu kwenye vita ya pili ya dunia. Wakaunganishwa kwenye 101st Airborne Division walikuwa na maisha ya ovyo wenzao kwenye Division waliwaita 'The Filthy Thirteen'. Walipiga kazi vizuri ndio inspiration ya movie ya The Dirty Dozen
 
Na hao watoto wachukuliwee kiukweli wanaweza
 
nchi yetu inabaadhi ya madereva na makondakta wasio jua wajibu wao 😃unakuta basi lina makondakta wanne au wa tatu lakina wote wameshindwa kujua kama kuna abiria wameingia kimagendo✅✅

Abiria huingia ndani ya bus hawa walikuwa nje chini ya chassis. Hata kama ungekuwa wewe ungedhania vipi mtu kujibanza huko?
 
Hawa ni makomandoo! Serikali inasubiri nini isiwapokee kwenye Jeshi la Wananchi na kuwapa mafunzo zaidi? Mtu unasafiri kilometer 200 chini ya basi linakwenda 120km/h umejishika na springi utashindwa nini vitani?
Endapo SEAL(sea, air and land army) hawajatamka kitu kuhusu Hawa watoto usemavyo mkuu, wanakosea. Kigamboni hapo navy wanasomesha watoto wa maskini hewa ...makamanda kama Hawa wasichukuliwe .....wawachukue wawalee maana wameonesha uthubutu
 
Back
Top Bottom