Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
umemaliza kila kitu,tutakifanyia kazi mkuu[emoji120]Pole sana mkuu naomba uangalie vitu hivi vitatu vinaweza kua chanzo.
Suluhisho ni...
- Rhesus factors kati yako na mkeo
- Matambiko/maagano katika ukoo wenu.
- Kuna mtu anakuchezea
Nendeni hospital
Nendeni mkaweke sawa matambiko ya koo zenu
Nendeni kanisani mkavunje maagano hayo.
Pole sana mkuu
hili nalo linawezekana kabisa mkuuHabari pole kwa changamoto
Hiyo ni Mizimu inabidi maombi ya kuvunja agano.
Inawezekana umefunga Ndoa na Majini, maali uliyopeleka ni kuwatoa kafara watoto wako , nakafara inafanyika mimba kuaharibika au Mtoto kufa baada ya kuzaliwa.
Mimba huwa zinachukuliwa na majini.
Tatizo lipo kwako nimesoma mada yako nimepata kitu haukai Na wanawake miaka 3 wanawake 5 . Hawa ni wanawake walioshika mimba Bado haujaweka wanawake wa pembeni.
Utakuwa unamikiwa na ulimwengu Mwingine na Ndio unaokufanya usidumu kwenye Mahusiano
asante mkuu,nawajibika kwa kila kitu kwa mama pamoja na watoto hadi pale Mungu anapowachukuaWanne alijifungua mtoto wa kiume mwaka mmoja uliopita na amekaa naye huku akimsumbua sana kwa homa za hapa na pale na wiki moja iliyopita nilipewa taarifa kuwa amefariki baada ya kuugua mfululizo
Maandiko yako yameniachia maswali mengi dhidi ya tabia yako, uwajibikaji kwa wanao na huyo aliyebeba ujauzito.
Anyway pole sana.
umeniwahi aisee. nilitaka nigusie jambo hili.Utakuwa unasumbuliwa na agano...
Kuna shida katika ukoo yaweza kuwa upande wa mama au baba...
Pole sana mkuuWakuu poleni na majukumu ya kujenga nchi..
Nimekuja kwenu kama mwana Jamii Forums nikiwa na uzoefu wa takriban miaka 10 na huu mtandao wetu pendwa unatusaidia kwenye mambo mbalimbali kwenye maisha. Nipo mkoani Dodoma kwa sasa ambapo nafanya biashara zangu na kupata riziki.
Nikiwa kama kijana na approach 30's nimekumbwa na matukio mfululizo ya kufiwa ama kuondokewa na watoto wangu punde tu wanapozaliwa wengine kabla ya kuzaliwa au hata muda mrefu baada ya kuzaliwa
Miaka ya hivi karibuni nilipita kwenye mahusiano na wasichana kadhaa, kati ya hao watano niliwapa ujauzito na mchanganuo wake ulikuwa kama ifuatavyo..
Wa kwanza alitoa mimba ikiwa na miezi minne ilimsumbua sana nusu na yeye aondoke na hakunipa taarifa juu ya hilo hadi nilipobaini na nikamuacha papo hapo.
Wapili aliharibikiwa mimba ikiwa na mwezi mmoja(huyu alikuwa na matatizo ya tumbo kabla ya kukutana na mimi alikuwa hashiki ujauzito hivyo alikuwa anajaribu kama amepona bila mimi kujua badala yake mimba ikaharibika).
Watatu alijifungua mapacha wanne kwa vipindi viwili tofauti na wote walifariki ndani ya wiki moja baada ya kujifungua.Yeye ni mwenyeji wa Tanga na ana uzao mzuri wa watoto mapacha.
Wanne alijifungua mtoto wa kiume mwaka mmoja uliopita na amekaa naye huku akimsumbua sana kwa homa za hapa na pale na wiki moja iliyopita nilipewa taarifa kuwa amefariki baada ya kuugua mfululizo.
Watano alishika ujauzito wa mapacha uliodumu kwa miezi sita na mimba ikaharibika pasi na kutegemea. Alichanganyikiwa sana maana alikuwa na matarajio mengi juu ya hao watoto pindi watakapozaliwa..
Kiujumla nimepoteza watoto 9 ndani ya miaka mitatu kwa sababu mbalimbali, hii kitu imekuwa ikinitesa sana na nashindwa kuelewa tatizo hasa ni nini na nini suluhisho lake maana napoteza viumbe wasio na hatia inaniumiza sana[emoji22]..
Naombeni ushauri wenu juu ya hili tatizo linalonikumba nifanyeje niweze kuepukana nalo na kama ni mpango wa Mungu kwanini kila siku mimi ukizingatia umri nao unakwenda wazazi wanataka wajukuu.
Naombeni msaada wenu wa mawazo na ushauri juu ya suala hili