Hii stori ya mtoa mada inafanana ya dogo mmoja Yuko kwenye early 30's Ni jirani yangu
[emoji117]Mwaka huu February kapoteza mtoto wa kiume masaa 6 tu baada ya kuzaliwa, tukazika fasta.
[emoji117]Mwaka Jana September alikua na binti alikua na mimba ya miez 6 ya mapacha (ultrasound ilionyesha)
Miez 8 kaumwa tumbo balaa, hospital wakasema watoto washafariki ikapid apigwe kisu kuwatoa kuokoa Maisha ya mama.
[emoji117]Mwaka juzi Kuna binti alikua hampendi, alikuja kumpa mimba bahat mbaya, kamwambia binti aitoe Hana mpango nae. vinginevyo akizaa wasijuane, binti akakataa kata kata.
Mimba imebebwa mpk miez 9, hospitali binti kafariki pamoja na mtoto wkt wa kujifungua.[emoji26]
[emoji117]Mwaka 2016 Nakumbuka alikuja kupata kesi ya kumpa mimba mwanafunzi,
kabla wazazi na serikali haijajua mchakato mzima ikabidi mzigo uflashiwe chap (nilishiriki kutoa safehouse ya binti kujificha mpk alipopona kabisa, binti wa watu nusu afe. Najuta na SITORUDIA ULE UPUMBAVU TENA[emoji26])
Ukiangalia hiyo Ni series ya watoto 4 dogo kawapoteza, huu msiba wa February ulimkumbusha mengi ya nyuma mpk anajuta kuitoa ile mimba ya kwanza ya yule mwanafunzi. Huenda Ndo alikua mwanae
Nafuatilia comments pia,
Naweza ambulia chochote Cha kumshaur.
Hii kitu iskie TU kwa mwenzako,
Dogo Sahv Kila mwanamke akikutana nae anamwagia ndani TU liwalo na liwe kujaribu bahati yake