Watu 10 maarufu zaidi kuwahi kutokea duniani

ongezea 21 fiston mayele
 
Basi hata Yesu hadithi yake inautata. Kwa Waislam alizaliwa chini ya mtende na aliitwa Issa na kwa Wakristo alizaliwa kwenye zizi la ng' ombe na kuitwa Emmanuel/ Yesu. Hapo basi kama unamuondoa Mariam kwa utata wa hizo hadithi basi muondoe pia Yesu/ Issa maana anautata wa hadithi pia. Mpaka leo wanabishania kwamba Issa ndo Yesu au ni watu wawili tofauti.
 
Che Guevara, Osama bin laden, Ponsio Pilato, Maria/Mariam, Queen Elizabeth II, Mao, John Kennedy, Fidel Castro, King Leopold II, Mansa Mussa, Alexander the great, Pharaoh, Paulus/Paul, Queen of Sheba, Patrick Lumumba, Mwl. Julius Nyerere na Xi Jinping
 
11. Pope John Paul II
12. Mother Teresa
13. Nelson Mandela
14. Desmond Tutu
15. Queen Elizabeth II
16. Dalai Lama.
 
Mkuu, akina Messi, Ronaldo, au Michael Jackson unawajua juu juu kwa sababu kuna viwanda vya habari kama Google, YouTube, TikTok, Insta n.k vinavyokuandalia habari zao na kukusogezea kila siku kwenye simu au Tv yako Mkuu.

Huna haja ya kusoma kitabu, picha zao na video zao zipo kila mahali.Lakini Maria na Yesu waliishi miaka 2,000 iliyopita ambapo hakukuwa na kamera, magazeti, wala mitandao.

Ili kuwajua, ni lazima upitie maandiko ya kale na historia. Labda nikuulize hili swali Mkuu, katika hao wote uliowataja ni nani ana jina gumu kufutika?

Messi akishastaafu, baada ya miaka 150 ijayo, vizazi vijavyo itabidi pia viunganishe taarifa na kuingia Google ili kumjua. Lakini jina la Maria litakuwa bado lipo kileleni kwa sababu limeandikwa kwenye vitabu vinavyosomwa kila siku.
 
Eleza kwanini huwapendi Yesu na Muhammad, walikukosea nini maana hawa wawili waliishi miaka Mingi Sana kabla ya ukoo wenu kuwepo.
Kama waliishi miaka mingi kabla ya ukoo wetu ndio Nini !?

Siwapendi cause wamewatapeli watu wengi duniani na kuwaaminisha vitu ambavyo havipo
 
The Prophet (Peace Be Upon Him), ni namba 1.
 
Ukiachana na story za wakristo na waislamu, historia inaonyesha Yesu alikuwepo, yaani kuna maelezo yake nje ya vitabu vya dini. Tofauti na Mariam yeye ni kama jina lake linapaishwa zaidi na Yesu. Hakuna alichokifanya yeye single-handedly. Kwahiyo jina la Yesu linajitegemea tofauti na Mariam. Uenda hata huyo Mariam mwenyewe sio mama wa Yesu. Alitengenezwa tu kwenye masimulizi
 
Mkuu,nje ya vitabu vya dini, anaelezewa kama mtu wa namna gani?
 
Umaarufu wa Maria siukatai point yangu ni kwamba kuna utata juu ya uwepo wake. Nje ya masimulizi ya dini ni mpaka uunganishe sana taarifa.
 
Mkuu,nje ya vitabu vya dini, anaelezewa kama mtu wa namna gani?
Historia inaonyesha Yesu alikuwepo. Aliishi Bethlehem, Nazareti na Misri. Alikua mtabibu wa mtaani, mwanaharakati na fundi seremala. Harakati zake za kutokubaliana na mienendo ya utalawa zilisababisha akamatwe na kuhukumiwa kifo.

Masuala ya kwamba alifufua watu, alibadilisha maji kuwa divai, alitembea juu ya maji, alifufuka n.k hayo ndio ya kiimani zaidi.
 
Duh! Hayo mwengine yawezekana wamembambikia tu.
 
Umaarufu wa Maria siukatai point yangu ni kwamba kuna utata juu ya uwepo wake. Nje ya masimulizi ya dini ni mpaka uunganishe sana taarifa.
Mkuu popularity huwa haimaanishi kuwa kila mtu anajua wasifu wako wa kihistoria, umaarufu ni ile situation ambayo jina lako tu likitajwa kila mtu anakuwa anajua nini maana yake.

Ukienda kwa mtoto wa darasa la pili au mzee wa kijijini ukisema jina la Maria mama wa Yesu, hawahitaji kuunganisha taarifa yoyote ili wamjue, wanajua hapo hapo unamzungumzia nani. Huo ndio umaarufu wenyewe.
 
Umefeli huwezi kulinganisha mtume Mohamed na vitu vya kijinga toa hao wavuja jasho no2 na no 3 mtendee haki jamaa
 
Kuna watu naona walipaswa wawepo kwenye hiyo list na hawapo kama
1. Nelson Mandela
2. Osama Bin Laden
3. Mohamed Ali
4. Mike Tyson
5. Vasco Da Gama
6. Barack Obama
....
....
....
 
Sijakataa umaarufu wake ninachotaka kusema ni kwamba bado story ya mariam inahitaji clarification kuthibitisha kama kweli alikuwepo. Katika dini zote kuna maelezo yake ambayo yanajipinga kiasi kwamba kimantiki unaona haiwezekani huyo mtu akawepo.

Mfano upande mmoja tunaambiwa alijifungua chini ya mtende upande mwingine tunaambiwa alijifungua kwenye zizi la ng'ombe. Upande mmoja tunaambiwa kuanzia ujauzito mpaka anajifungua alikua bega kwa bega na mumewe yosefu upande mwingine yosefu hatajwi kabisa na tunaambiwa wakati anajifungua alikua pekee ake na misaada mingine kama maji alipewa na Mungu mwenyewe. Haiwezekani akawa mtu mmoja huyo.

Mariam mama wa Yesu ni yupi kati hao wawili? Haiwezekani mama wa Yesu akawa hajulikani kabisa na huyo Mariam ametumika kama muhusika wa kubuni tu? Hata Yesu mwenyewe kuna maelezo yametofautiana kila upande lakini huo utofauti bado hauondoi mantiki ya uwepo wake kama ilivyo kwa mariam

Umaarufu for the sake of umaarufu hata fictional character anaweza kuwa nao mfano Adam na Hawa wanajulikana kila chocholo duniani lakini hawawezi kujumuishwa kwenye watu maarufu zaidi kuwahi kutokea kwa sababu uwepo wao bado unahitaji clarification kuthibistisha kama kweli waliwahi kuwepo hapa duniani.

Binafsi naona mariam ni kama muhusika wa kubuni. Lakini mawazo yangu sio msahafu. Ikionekana pasipo na shaka kwamba mariam aliwahi kuwepo basi ana sifa zote za kuingia kwenye top 3 kama watu maarufu zaidi kuwahi kuwepo duniani
 
Umefeli huwezi kulinganisha mtume Mohamed na vitu vya kijinga toa hao wavuja jasho no2 na no 3 mtendee haki jamaa
Dhumuni langu halikua kuweka usawa wa kidini. Mohamad bado sio popular kwenye maeneo mengi sana duniani ambayo dini ya uislamu haijafika. Tofauti na hao wemgine ambao wanafahamika kila chocholo. Ungeeleweka zaidi kama ungesema ni vigezo vipi vya kumfanya akae namba za mbele.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…